Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,340
120,871
Wanabodi,
Utangulizi
Katika chaguzi zote zilizopita tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini, hakuna uchaguzi mwingine wowote uliokuwa na upinzani mkubwa kama uchaguzi uliopita wa ,wala 2015, ambapo mgombea wa upinzani kwa jina la Ukawa, Mhe. Edward Lowassa, amepata idadi ya kura nyingi kuliko hata kura zilizomuingiza rais Jakaya Kikwete madarakani ile 2010, ambapo pia ni kwa mara ya kwanza, Mgombea wa upinzani amepata jumla ya kura nyingi Zaidi kuliko Mgombea wa CCM upande wa Zanzibar kwa mujibu wa kura za NEC, hivyo unaweza kupata picha ya nini yangekuwa ni matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kwa upande wa ZEC kama matokeo yasingefutwa!.

Kuna Watu Hawakumchagua Magufuli Kwa Kuamini CCM ni Ile Ile, Hivyo Walichagua Upinzani Ili Kuleta Mabadiliko!.
Kwenye uchaguzi huo, kuna watu ambao hawakumchagua mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli kutokana kuchoshwa na madudu ambayo CCM imelitendea taifa hili kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita, hivyo walichagua mabadiliko kwa imani kuwa tatizo la nchi hii ni CCM tuu, wakiamini siku zote kuwa CCM ni ile ile, hivyo hata ukimchagua Magufuli, utakuwa umeichagua CCM ile ile!, hii ilipelekea Magufuli kuendesha kampeni kwa ugumu sana kuinadi CCM kulikopelekea kuepuka kuitaja taja sana CCM, huku akinadi kwa mabadiliko ya kweli kwa kujinasibu na neno "Tanzania ya Magufuli", " Chagua Magufuli, chagua mabadiliko".

Magufuli Alijinadi Kuleta Mabadiliko ya Kweli na Baada ya Kuchaguliwa, Aliyaishi Maneno Yake Kwa Matendo.
Na kweli Magufuli baada ya kuchaguliwa aliyaishi maneno haya kwa kauli na matendo, kwani mara tuu baada ya kuchaguliwa, alifanya kweli bayana kwa kufanya mabadiliko ya kweli kwa kasi ya ajabu kulikopelekea baadhi ya wale ambao hawakumchagua rais Magufuli kwa kudhania ni kuichagua CCM ile ile, hivyo kwa kutaka mabadiliko, wakaichagua UKAWA iliyokuwa inahubiri mabadiliko, lakini baada ya matokeo ya mwisho, ya UKAWA kushindwa, na Magufuli wa CCM, kushinda, ilitarajiwa walioichagua UKAWA wajutie kushindwa kwa mgombea wao wa UKAWA hivyo kuwakosesha mabadiliko, wakitarajiwa wamchukia rais Magufuli kwa kuirejesha CCM ile ile, lakini hali imekuwa ni tofauti, badala ya wapinzani na waliochagua upinzani kumchukia rais Magufuli, ndio kwanza wanazidi sio tuu kumpenda na kumkubali, bali wengine hata kuamua kufuata!.

Wapinzani Wakoshwa na Utendaji Kazi wa Rais Magufuli wa "Hapa Kazi Tuu", Wamuunga Mkono na Soon Wataanza Kumfuata!.
Kufuatia utendaji kazi wa rais Magufuli na falsafa yake ya "hapa kazi tuu", akianza na zile amsha amsha za ziara zake za kushtukiza, mara atembee kwa miguu kutoka ofisi moja hadi nyingine!, na akikutana na madudu, anatumbua papo kwa papo!, zimewafanya wapinzania wamuaminie rais Magufuli katika muda mfupi kwamba ni mtu anayeleta mabadiliko ya kweli, hivyo wengi wao sasa sio tuu wanamuunga mkono kwa dhati rais Magufuli, na baadhi yao wanajutia kupoteza kura zao kumchagua Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa na kuichagua UKAWA kwa jinsi sasa wanavyomkubali rais Magufuli, kwa utendaji wake na kuleta mabadiliko ya kweli waliyoyataka, hadi kuamini kuwa angekuwa ni Lowassa, asingeyafanya haya yanayofanywa na Magufuli, hivyo kwa sasa, wapinzani wengi, wameishahama kambi ili kumsupport rais Magufuli kwa sababu anachokifanya ndicho kitu kile kile ambacho kingefanywa na UKAWA. Kuna wapinzani wengi wako upinzani kwa sababu wako tuu lakini sasa moyo wao ni CCM kwa Magufuli, na amini usiamini, very soon, tutashudia mass exodus kutoka upinzani kurejea CCM!.

Licha ya CCM Kuwa ni Ile Ile, Kwanini Magufuli Alichaguliwa?.
Kiukweli kuna wengi waliichoka CCM, lakini walimchagua Magufuli kwa sababu alionyesha tumaini jipya. Ila pia tukubali tukatae, kuna watu ambao walimchagua Magufuli kwa sababu tuu ni mgombea wa CCM. Kuna maeneo katika Tanzania hii, wanaamini kuwa kiongozi mzuri ni lazima atatoka CCM tuu, haswa yale maeneo yenye low literacy levels, hawana uwezo wa kufanya informed choices na informed decisions based on sera za chama fulani, kwa vile uelewa wao wa vyama vingi ni finyu sana, hivyo hawa walimchagua rais Magufuli kwa sababu tuu ni Mgombea wa CCM ambapo hata CCM ingesimamisha jiwe, jiwe lingepita!.

Watanzania Wengi ni Masikini wa Kutupwa!, Kwa Nini Maeneo Yenye Umasikini Uliotopea Ndizo Ngome za CCM?!.
Amini usiamini, maeneo yote yenye umasikini uliotopea, ndizo ni ngome imara za CCM, na maeneo yenye efuani kiuchumi ndiko angalau upinzani umechaguliwa!, hii ni kufuatia hali ya umasikini uliotopea, thamani ya kura yao ni ile t-shirt na kofia na shibe ya siku moja, hivyo waliichagua CCM kwa sababu ndicho chama pekee kilichokuwa na the capacity ya kugawa t-shirt, kofia na 'shibe' japo ya siku moja, kwa nchi nzima, hivyo hawa waliichagua CCM. Na kuna wengine wengi, waliichagua CCM kwa kuamini CCM ni ile ile, hivyo Magufuli ni mwenzetu, wakiamini atayaendeleza yale yale mambo ya ki CCM CCM!, "life as usual". Lakini baada ya rais Magufuli kuingia ikulu na kuleta mabadiliko ya kweli, kwa kuanza na utumbuaji, sasa kuna baadhi ya walioichagua CCM wakidhani ni CCM ile ile, na kumchagua Magufuli kwa kudhani ni "mwenzetu", sasa wanajuta!, huku wale ambao hawakumchagua, wanamfurahia!.

Waliomchagua Magufuli Wanaojuta, na Ambao Hawakumchagua Wanamfurahia!.
Miongoni mwa wajutaji wakuu wa kwanza ni hao watumbuliwa!. Hapa naomba kwanza naomba hapa tukubaliane in principal, kuwa majipu yote by nature ya nyadhifa zao, yote ni CCM!, hivyo ili ku maitain status quo, majipu yote yaliyotumbuliwa na wengine ambao hawajatumbuliwa, na majipu yoto yatakayokuja kutumbuliwa siku zijazo!, wote ni CCM!. Wote watakuwa walimchagua rais Magufuli wakiamini ni mwenzao, na kuna wengine ule utumbuaji wa mwanzo nao waliushangilia, na wengine wakiutangaza utumbuaji with smiling faces, hadi walipotumbuliwa wao!, hawa kiukweli kwa sasa wanajuta kumchagua Magufuli!.

Huku wale masikini wa kutupa walioishi kwenye lindi la umasikini uliotopea na wale wenye njaa waliotoa kura zao kwa shibe ya siku moja, bila kujua wanachagua nini, ndio sasa wanamfurahia na wanamshuru rais Magufuli kwa elimu bure, japo bado wananungunika na kulalamika jinsi wanavyozidi kupigika kimaisha, kwa hali ngumu, lakini wanamkubali sana rais Magufuli na kumuhesabu kwao kuwa rais Magufuli ni baniani mbaya, ila kiatu chake dawa, wanamkubali.

Rais Magufuli Afanya Makubwa Kwa Kofia Moja Tuu ya Rais wa Nchi!, Akivaa na ya Pili ya Mwenyekiti wa CCM, Jee Kutakuwa na Upinzani Tanzania?!.
Haya yote ambayo rais Magufuli anayafanya, anayafanya huku akiwa amevaa kofia moja tuu, ya Mkuu wa serikali, kama watu wanamkoma kwa hii kofia moja tuu ya urais, jee rais Magufuli atakapovishwa na ile kofia ya pili ya M/K wa CCM, can you imagine jee majipu watakomaje?!.

Magufuli akiushika uenyekiti wa CCM, na kufuatia CCM kuwa ndio the source of all evils befalling this nation, then rais Magufuli akikishika na chama, atakisafisha na madudu yote yatakwisha, just imagine, jinsi wafanya madudu wote waliokuwa wanakitumia CCM kama chaka la kujifichia kufanyia madudu yao, watakomaje pale rais Magufuli atakaposhika chama na kukisafisha?, hii inamaanisha CCM itanyooka, kama chaka la uovu wa nchi hii, mzizi wake ni CCM, hivyo hilo chaka litafyekwa, then na nchi yote itanyooka!. Wasiwasi wangu ni mmoja tuu kumhusu rais Magufuli atakafishika uenyekiti wa CCM, ataijenga CCM imara na kama atairudisha ile CCM ya Nyerere, CCM kurejea kuwa ni chama cha watu na sio CCM hii ya wenye pesa, ambayo kupata nafasi ya uteuzi vigezo sio tena unapesa kiasi gani, au naweza kuhonga au ku lobby vipi, bali sifa kuu za Uongozi ni uzalendo wako. uchapa kazi wako na uwezo wako wa uongozi, then kuna viongozi wengi wazuri walioikimbia CCM kutokana na madudu yake watarejea CCM!. Siajabu mkashangaa hata baadhi vigogo wa vyama vya upinzani, wakiviacha vyama vyao na wakirejea CCM. wengine ama wakirudi nyumbani walikotoka, na wengine wakijiunga CCM kwenda kusaka fursa na opportunities, hata Dr. Slaa anaweza kurudi kabisa kurejea CCM. CCM imara is not healthy at all kwa mustakabali wa upinzani nchini kwetu Tanzania, haswa kwa kuzingatia jinsi huu upinzani uliopo ulivyo ni fragmented opposition, hivyo naiona kabisa hatari ya uchaguzi wa 2020 kuwa uchaguzi wa chama kimoja cha pseudo multipatism, or semi single party, kwa kuturudisha kule kwenye chama kimoja kama enzi ya mwalimu baada ya wapinzani karibu wote kujiunga CCM.

Kuna Watu Wanamshagilia Rais Magufuli Machoni Tuu, Lakini Mioyoni Wanalia!.
Ukiachilia majipu tumbuliwa ambao wanajuta kutumbuliwa, wako wengine ambao wanaimba nyimbo za sifa machoni na mdomoni huku moyoni wakijuta kisirisiri kufuatia baadhi ya watumbuliwa kuwa ni watu wao, akiwemo mtangulizi wake, baadhi ya huu utumbuaji sio tuu unamuaibisha sana kumuonyeshea kuwa yeye alikuwa kiongozi dhaifu mno kiasi cha kulea madudu kibao yaliyogeuka kuwa majipu , na kinachomjutisha ni the manner ya baadhi ya utumbuaji, jinsi wanavyowatumbua baadhi ya wateule wake kwa masifa, kuwaaibisha na wengine kuwadhalilisha, tena kwenye kadamnasi ya watu, na kuna wengine wanaotumbuliwa, kiukweli hata hawana kosa lolote ku justfy utumbuaji wao zaidi ya chuki tuu za ukabila, udini na ukanda, which is not only very bad, but very dangerous thing, due to the presence kitu kinachoitwa "karma" ambacho kiukweli kabisa, hakina mswalie Mtume kama haki haikutendeka!, which will take care of this, hivyo kumfanya mtangulizi atahayari, kunyong'onyea na kujisikia amekuwa mdogo kama sisimizi!.

Hitimisho.
Jee wewe mwenzetu uko upande gani kwa haya anayoyafanya Mhe.Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, bado unaamini CCM ni ile ile hivyo hata Magufuli akishika chama, things will be the same again, au akishika na chama, kujenga CCM imara, CCM itanyooka, nchi itanyooka, Watanzania tutanyooka, na tutasonga mbele tukiwa chama kimoja?!.

Paskali
 
Mimi nimeshiriki kumuombea kura maeneo mbalimbali ya Nchi hii, online na Ardhini na nafurahishwa sana na anacho kisimamia, maana tulitukwana sana wakati tunamnadi, tuliwaambia wananchi kua mabadiliko ya kweli yapo kwa Magufuli, na mpaka sasa ameonyesha njia... TUNAMTKA AKAZE KAMBA ZAIDI
 
umeanza unafiki wako eti wametumbuliwa bila kosa we ndio bwege kweli bado lowasa muda wake wa kutumbuliwa umekaribia
 
Wanabodi,

Katika uchaguzi uliopita, ulikuwa na upinzani mkubwa, kuna watu ambao hawakumchagua Dr. John Pombe Magufuli kutoka na kuchoshwa na madudu ya nchi hii, wao walichagua mabadiliko kwa imani kuwa tatizo la nchi hii ni CCM, na siku zote CCM ni ile ile, hivyo hata ukimchagua Magufuli, utakuwa umeichagua CCM ile ile!, japo katika kampeni zake, Magufuli alisema Chagua Magufuli, chagua mabadiliko, hivyo baada ya kuchaguliwa ni kweli Magufuli ameleta mabadiliko, hivyo wale ambao hawakumchagua Magufuli kwa kutaka mabadiliko, wakaichagua UKAWA kwa kutaka mabadiliko, japo UKAWA haikushinda, aliyeshinda ni Magufuli, hiki anachokifanya Magufuli, ndicho kitu ambacho kingefanywa na UKAWA, hivyo wale wote ambao hawakumchagua Magufuli, sasa wanamkubali na kumshangilia, kwa sababu Magufuli anakifanya kile ambacho wao walikichagua!.

Na kuna watu walimchagua Magufuli kwa sababu ni mgombea wa CCM, hawa walimchagua kwa kuamini CCM ni ile ile, hivyo Magufuli ni mwenzetu, wakiamini atayaendeleza yele yale ya ki CCM CCM!, "life as usual". Baada ya Magufuli kuingia madarakani na kuanza utumbuaji, sasa kuna baadhi yao wanajuta!.

Miongoni mwa wajutaji wakuu wa kwanza ni hao waliotumbuliwa!. By nature ya nyadhifa zao, ili ku maitain status quo, majipu yote walimchagua Magufuli wakiamini ni mwenzao, na kuna wengine ule utumbuaji wa mwanzo nao waliushangilia, na wengine wakiutangaza utumbuaji huku wana smiling faces, hadi walipotumbuliwa wao!, hawa kiukweli wanajuta kumchagua Magufuli!.

Haya yote ambayo Magufuli anayafanya, anayafanya huku amevaa kofia moja tuu, ya Mkuu wa serikali, kama watu wanamkoma kwa hii kofia moja tuu, atakapovishwa na kofia ya pili ya mkuu wa chama, jee watakomaje?!. Magufuli akikishika na chama, kufuatia CCM kuwa ndio source of all evils zinazoikumba nchi yetu, then akikishika na chama, madudu yote yatakwisha, wafanya madudu wote watakoma na nchi itanyooka!.

Akiachilia majipu ambao wanajuta, mwingine anayejuta ni Jakaya Mrisho Kikwete, huu utumbuaji sio tuu unamuaibisha sana kumuonyeshea kuwa yeye alikuwa rais dhaifu mmno kiasi cha kulea madudu kibao, bali jinsi anavyowatumbua baadhi ya wateule wake kwa masifa na kuwaaibisha na kuwadhalilisha, tena wengine hawana kosa lolote, lazima kunamfanya JK atahayari, kunyong'onyea na kujisikia amekuwa mdogo kama sisimizi!.

Jee wewe mwenzetu uko upande gani kwa haya anayoyafanya Magufuli, bado unaamini CCM ni ile ile hivyo hata akishika chama, things will be the same again, au akishika na chama, nchi itanyooka na tutasonga mbele?!.

Pasco

Mungu Pasco
Kwa mwendo huu wa Magufuli ninafikiri hata ukawa wasingeweza kushika kazi yake.
 
sikumchagua lakini Amenikosha!
naijutia kura yangu.
Chadema wangekuwa kama wewe, Taifa lingesonga mbele, Mwenyekiti wao kila siku analaumu tu. Muda wa kuonewa huruma kwa sababu ya kulalamika umekwisha , Mbowe anapaswa kutafuta njia mbadala ya kuwachota akili wajinga, hii ya kumlaumu JPM anapoteza muda.
 
Mbona Lowassa hajampa kura, na yuko anaisoma namba; kiongozi wake wa kampeni Bashir Awale katimuliwa yuko kenya now, mkwewe yuko ananyea ndoo gerezani, mshirika wake Kitilya amekonda kama nini!
 
Paskali wewe ni very controversial person. Angalia post iliyotangulia
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Sim
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...


Deo sio controvesial, bali kila bandiko linajitegemea na kujitosheleza, ila huu ni uthibitisho kuwa sina upande, niko totally impartial, kwenye mazuri, napongeza, kwenye madudu nabomoa, nakosoa na kushauri!.

Pasco
 
Mimi nimeshiriki kumuombea kura maeneo mbalimbali ya Nchi hii, online na Ardhini na nafurahishwa sana na anacho kisimamia, maana tulitukwana sana wakati tunamnadi, tuliwaambia wananchi kua mabadiliko ya kweli yapo kwa Magufuli, na mpaka sasa ameonyesha njia... TUNAMTKA AKAZE KAMBA ZAIDI






Naona unajipigia "promo" ili walau akukumbuke kwenye ufalme wake.
 
Hii hoja wenzio walishaipinga kwamba anayoyafanya ni yale ambayo wapinzani walikuwa wanataka. Tena wanamchukia kweli kweli. Au hujawasikia wakilalamika Magufuli anaenda kinyume? Wanadai utumbuaji wake ni kudhalilisha watu.

Uwe ulimchagua au hukumchagua usithubutu kukutwa.
 
Mie sikumchagua magufuli, kura yangu ulienda ukawa. Kuanzia udiwani hadi urais.
Ila kinachonisikitisha viongozi wangu kupingana na raisi, napata shida kuona kama wangeyafanya hayo anayo yafanya raisi.

Napata shida kuona kama lowassa angekubali mkwe wake ashitakiwe

Nawapongeza wote walio mpa kura magufuli na kumfanya awe raisi wetu
 
Mie sikumchagua magufuli, kura yangu ulienda ukawa. Kuanzia udiwani hadi urais.
Ila kinachonisikitisha viongozi wangu kupingana na raisi, napata shida kuona kama wangeyafanya hayo anayo yafanya raisi.

Napata shida kuona kama lowassa angekubali mkwe wake ashitakiwe

Nawapongeza wote walio mpa kura magufuli na kumfanya awe raisi wetu
chadema wamepewa kazi ya kumsafisha mkwe wa lowasa ..teh teh lowasa kashawageuza chadema toy lake la kuchezea
 
Pasco, you are dead wrong. Wengi tulimchagua Magufuli kwa kukatishwa tamaa na upinzani ulioamua kuchukua timu ya mafisadi kutoka CCM ili warudi madarakani kwa mgongo wa upinzani. Na trust me, mpaka sasa tunaona tulifanya uamuzi sahihi, na hatujuti, tunashangilia, labda Magufuli abadilike baadae.
 
Aina ya watu kama Magufuli huwa wanakuja kushindwa wenyewe
na wakishindwa watahitaji msaada..na wakishasaidiwa ndo hapo
hujikuta 'wamekubali kuwalinda watu kiaina'

So watu wanamsubiri tu

wanaosema 'ndege mjanja hunasa tundu bovu' sio wajinga....


Ndo maana inashauriwa kuongoza watu kulingana na 'tamaduni zao'

kuna vit unaweza viona vidogo hadi vikutokee puani ndo utajua

Angalia now anashauriwa kumtumbua Kitwanga na anazuga hasikii
 
Back
Top Bottom