Rais Magufuli, Usiyapuuze haya mambo

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Nafahamu mh rais ujumbe wangu utakufikia vyema aidha kusoma wewe mwenyewe au kupitia wasaidizi wako.

Nina uhakika 100% kuna watu ndani ya serikali yako wanakuhujumu, wewe una uchungu na maisha ya kimaskini tunayoishi watanzania wenzako hawaliwazi hilo, wana hasira na chuki kubwa sana dhidi yako, maana umewazibia mianya ya wizi, walizoea kuiba na kuona ndo sehemu ya maisha yao, ghafla mambo yamebadilika na sasa wengi wao wanaishi Kwa mishahara tu, hawawezi kukupenda hawa.

Nina amini kabisa mambo matatu yanayoendelea ndani ya taifa letu ni mkakati wa wabaya wako ili wananchi wakose imani na wewe ya kuwavusha ktk bahari ya umaskini.

(1)Bunge kuto onyeshwa" live "

(2)Sakata la sukari

(3)Kuzuia mafao ya wafanyakazi Kwa mifuko yote ya pensheni.

Mh rais, unaweza kuona ni jambo la kawaida sana kumbe limetuumiza Sana wananchi na litakigharimu Sana chama chako 2020.

Sisi bado ni maskini Sana, na hatuna uhakika wa kuishi miaka mingi, kuzuia mafao yetu ni ukatili usio na kifani, ikitokea mtu kufukuzwa kazi na hana mtaji hayo mafao ndo huwa kimbilio, sasa yanapozuiwa na mtu alipoteza muda wake wote kazini ataishi vipi?

Kuna wafanyakazi wa sekta za migodi, hawa hawana uhakika na ajira zao, mara nyingi kazi zao hazidumu, hawa nao wataishije?Nimeshuhudia watu wengi nikiwemo mimi mwenyewe mafao ya kujitoa yakisaidia Sana ktk kujikomboa na umaskini. Watanzania wanatekeleza kauli mbiu yako ya hapa kazi tu, kuwapokonya mafao yao ni kuwavunja moyo na kuwatumbukiza ktk shimo la dhiki kuu.

kodi wanalipa na mafao yao waporwe? kuwaambia wasubiri hadi miaka 55 ni kuwatapeli na kuwaibia jasho lao, kitu ambacho ni dhambi kubwa sana mbele za Mungu. Hawa SSRA walitaka kuzuia mafao haya tangu awamu ya nne wakakwama, Kwanini iwezekane ktk serikali yako? Zilikuwepo njama za kuto onyesha bunge live tangu awamu ya nne zikakwama, Kwanini zimefanikiwa ktk serikali yako?

Leo sukari imekuwa adimu na kupanda bei, kesho itakuwa mchele, mara unga na nk, mwisho wa siku maisha yatakuwa magumu mno, wafanyakazi, na wananchi wote wa hali ya chini wataanza kusema kuwa afadhali hata awamu ya nne.

Mh rais, Nakuomba Usiyapuuze haya mambo, huu ni mkakati na njama za kuharibu utendaji wako uliotukuka,rudisha fao la kujitoa, dhibiti sukari, ruhusu bunge lionekane Kama zamani, kauli ya waziri mkuu eti watanzania wanashinda kwenye TV kuangalia bunge wanashindwa kufanya kazi na ni wavivu siyo kweli, kwanza si kila mtanzania ana hobi na siasa, pili hakuna mtu mjinga wa kushinda kwenye TV akaacha kutafuta pesa.

Mh rais nawasilisha.
 
Pole mkuu,nampenda magu,ila kwa mambo hayo matatu hakika akuwe makini,hainiingia akilini kabisa
 
Alianza kusema viongozi ni majipu, sasa anaona wafanyakazi na wafanyabiashara nao ni majipu.
Baadae ataona kila mtu ni jipu. Asipojirekebisha uchumi wa nchi utaanza kuporomoka kwa kasi, na CCM pia.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kweli hayo yanaumiza sana!! Au anataka kujenga kiwanda cha sukari kwa pesa zetu? Hapana haiwezekani! Hasira za wafanyakazi na kilio cha masikini wanavyoteseka havitamuacha kamwe! Kama kweli yeye ndio amesema wazuie mafao amekosea sana na ametukosea sana!! Kama huwa wanasoma hapa ajue kuwa tunasikitika sana na Uamuzi wake huo.......mnyonge akakope wapi wakati hela yake anayo? Si apewe akapambane na maisha mtaani???
 
huu ni uhuni MTU alipwe mafao yake hata akiwa amefanya kazi miezi miwili..maana amechangia kwa jasho....

lingine...aongeze mishahara kwa wafanyakazi hususani walimu... asidhani 2020 ni mbali
 
Hakuna yeyote anayemhujumu kwani yeye hana akili ya kufikiri?. Kwanini mnapenda makosa ya mtu kumbambika mwingine?eti anahujumiwa! Kwani sukar ni nani aliyepiga marufuku uagizwaji na kwamba vibali vyote atatoa yeye, issue ya bunge live ni maamuzi ya baraza la mawaziri, unamjua kiongozi/ mwenyekiti wa baraza la mawaziri wewe!
 
Mnaomtupia lawana raisi magufuli kwa jitihada zake ni wapuuzi na marofaa! Fikiri kabla ya kupost unanikwaza sanaaa! Nchi ilipokuwa ni lazma kwanza turudi nyuma hatua nyingi kwani ilikuwa pabaya sanaa!!! Namshukuru mungu daima magufuli ataendelea kufanya vizuri kwani mungu yuko pamoja nae! We post utumbo piga kelele lakn fahamu kuwa unaowafikishia ujumbe ni waelewa zaidi yako mpuuzi!!
 
mkuu anapotengeneza na kuboresha nchi hasikosolewe bali apewe moja na mbili ya kuboresha zaidi, sawwwaaaah!
 
Mnaomtupia lawana raisi magufuli kwa jitihada zake ni wapuuzi na marofaa! Fikiri kabla ya kupost unanikwaza sanaaa! Nchi ilipokuwa ni lazma kwanza turudi nyuma hatua nyingi kwani ilikuwa pabaya sanaa!!! Namshukuru mungu daima magufuli ataendelea kufanya vizuri kwani mungu yuko pamoja nae! We post utumbo piga kelele lakn fahamu kuwa unaowafikishia ujumbe ni waelewa zaidi yako mpuuzi!!
Mchungaji mbona unaongea maneno yasiyo na staha
 
Serikali ilishasema mafao haya ya kujitoa yataendelea kutolewa mpaka hapo mbadala wake utakapopatikana (Unemployment Benefit) zingine zote ni uzushi mtupu, hiyo mifuko isiwasingizie SSRA waambieni wawape waraka kutoka SSRA inayowakataza kulipa hayo mafao
 
Back
Top Bottom