Rais Magufuli usitumie ganzi

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,624
3,653
Mh. Amirijeshi mkuu ninapendekeza kwa halmashauri yoyote kuanzia sasa itakayobainika kuwa na mtumishi hewa basi mkurugenzi wake awekwe kizuizini na apelekwe mahakamani tena ile ya mafisadi itakayoanza mwezi julai, alipe hasara zote kwa sababu aidha ni mzembe au anakula yeye hizo hela.

Leo tena katika halmashauri ya kinondoni wamebainika watumishi hewa 55 idadi kubwa zaidi kuliko ile ya awali ambapo walikua 34. Niliwahi kusema Mh. Rais nia yako ni njema lakini mbinu uliyotumia kubaini watumishi hewa inanipa mashaka, yaani haiwezekani watu waliobuni mpango haramu ndio wawaondoe hao wanaharamu.

Huyo mkurugenzi na idara inayohusika wakamatwe, wahojiwe, wawekwe kizuizini, wapandishwe kizimbani na wafungwe au wafilisiwe malizao zote maana hao walidhamiria kulinda wahujumu na hao sio majipu bali ni mabusha!

Mh.Rais usiwaonee huruma baba fumba macho usitumie ganzi
 
Ye yote aliyekula mshahara wa ghost worker anatakiwa kuwa rumande wakati akimsubiri Pilato.
 
Back
Top Bottom