"Usipoziba Ufa Utajenga Ukuta" ni mithali au msemo unaotumika katika jamii wenye maana ya kufundisha au kufikisha ujumbe hasa kwa kile kitachotokea baada ya mhusika kutotekeleza au kutoshughulikia jambo fula analowajibika nalo.
Hapa Tz Rais huchaguliwa na wananchi kwa njia kura maana ndo katiba inavyowataka wananchi wafanye hivyo. Kabla Rais chaguliwa hajakabidhiwa madaraka ya nchi, huapishwa tena hicho kiapo anakila mbele ya kadamnasi huku wageni kedekede toka nchi mbali mbali wakimshuhudia. Nayeye (Rais) huapa kuilinda katiba kwa nguvu zake zote bila kuenda kushoto wala kulia; yaani atalazimika aidha anapenda au hapendi kutekeleza na kutimiza yote yaliyoandikwa kwenye katiba.
JPM aliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katiba ambayo inatambua na kukubali uwepo wa vyama vingi vya siasa, tena katiba inayoviruhusu hivyo vyama kufanya mikutano ikibidi na maandamano huku police wakilinda hiyo mikutano au maandamano ya hivyo vyama. Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa taarifa ya lini na wapi vitafanyia mikutano hiyo.
Je, ni kwanini Rais JPM anakataza mikutano ya vyama vya siasa eti mda wake umeisha? je ni wapi katiba inasema kwamba uchaguzi ukiisha ns mikutano ya kisiasa itakoma hadi mwaka wa uchaguzi? Je Rais akivunja katiba raia wao watavunja nini?
JPM kwa CDM ni rahisi sana kuujenga UKUTA maana materials wanayotumia yanapatikana kila kona ya nchi tena ni ya bure hayahitaji hela yoyote. Ila kwako (Rais) ni rahisi mno kuuziba ufa maana materials yanapatikana kwa urahisi ila kwa gharama kiduchu tu. Ila ukiacha uendelee itakubidi kuja uujenga UKUTA, je ni nani atakusaidia kukuletea materials ambayo kwanza ni vigumu kuyapata tena bado gharama yake haibebeki. Kumbuka JK alishakataa kuulizwa lolote/ chochote juu ya serikali wala chama; sasa je Rais wangu JPM uko tayari kuacha kuziba ufa ns kuja kujenga UKUTA; je unajua itakugharimu kiasi gani na kwa mda
gani? je miaka yako 5/10? itakutosha kuumaliza huo UKUTA au utamwachia mrithi wako huo mzigo?
Mie nadhani ni vyema kwako Rais kufyatua viwanda acha wapinzani wafyatue mkutano huku sisi wananchi tukifyatua watoto. Maana ukikimbizana na wapinzani ifikapo 2020 wote mtafanana kwenye kampain; wakati wewe utakuwa unajitetea kwanini tz ya viwanda haipo wao kwa upande mwingine wakiahidi.
JPM ziba tu kaufa yatosha sana na utakuwa Rais bora kabisa tena kwajinsi usivyopenda ufisadi yaani wewe ndo tumaini lililopo sasa la Watz, tupe tz ya viwanda Rais wetu.