Rais Magufuli una ujasiri jukwaani tu

Tuliahidiwa kushuka kwa vifaa vya ujenzi kinyume chake sasa ndo bei juu kwa kuongeza kodi. Hii sasa ndo hapa kazi siyo?
Wengine hata vikishuka hamjui Na uwezo WA kujenga haupo. Kwa tarifa fupi Tu bei cement Dar August 2015 ilikuwa 13500 kwa sasa inauzwa kati ya 10000 na 11000 kwa reja reja. Ishuke kwa kiwango gani.au ni mkumbp tu
 
Claim yako ni nzuri sana ila inahitaji data ili iwe ni kweli au la. Halafu hizo percentages zako umezipataje? Halafu taasisi za serikali na siziso za serikali kama MCT sijui kwa nini hawafanyi tafiti katika masuala kama haya ili kuisaidia nchi.
 
Zamani nilikuwaga naudharau umonitor wa darasani, ila sasa nauheshimu.
 
Jamani msimseme JPM, mwenyewe alishasema kuongoza nchi ni kazi kweli kweli, si mlimsikia mrisho mpoto akiimba ,

[Verse 1 – Mrisho Mpoto]
Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu
Tulipoficha mundu za kupondea wezi
Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne
Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango
Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni
Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje

Sizonje chumba hiki naomba usiingie
Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa
“USIYEMTAKA KAJA”
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia

JPM anahitaji msaada wa watu wake wa karibu a.k.a watu wa idara.
 
Tunaambiwa kuwa budget ya mwaka ni mtetezi wa wanyonge na watu hali ya chini. Je kuna ukweli wowote kuhusu hili?
 
Thread hii imeshamaliza kila kitu
 
Kama ndo hivyo basi tujitoe katika hili jinamizi la demokrasi na tuishi kwa kutumia falsafa yetu wenyewe.
 
Tunaambiwa kuwa budget ya mwaka ni mtetezi wa wanyonge na watu hali ya chini. Je kuna ukweli wowote kuhusu hili?
Mkuu ukiangalia hii budget ndio imechukua hata kile kidogo cha wanyonge mtasikia mdaa si mrefu.. hivi huko kwako sukari inapatikana kwa 1800
 
Ukiwa niwakusifia hii thread inachoma sana

Unajuaje kama inachoma...wewe ndiye uliyeandika sasa how do you know kuwa inachoma? Yaani unaandika wewe halafu una-judge mwenyewe, uandishi gani wa aina hii???!!! Huo ni uanaharakati, na unafahamu sifa za wanaharakati... Ok unasema ikiwa ni wa kusifia tu...je, inakuwaje kwa yule wa kushutumu, kulalamika na kuponda each and everything???
 
Wengine hata vikishuka hamjui Na uwezo WA kujenga haupo. Kwa tarifa fupi Tu bei cement Dar August 2015 ilikuwa 13500 kwa sasa inauzwa kati ya 10000 na 11000 kwa reja reja. Ishuke kwa kiwango gani.au ni mkumbp tu
Unafikiri watanzania wote waishi dar? Usikurupuke tu. Na pia vifaa vya ujenzi si cement tu. Ongezeko la kodi from 10% up to 25%
 
Kwa sasa anafanya ziara za kushtikiza makanisani. Bandarini na Mihimbili kushapona.
 
Claim yako ni nzuri sana ila inahitaji data ili iwe ni kweli au la. Halafu hizo percentages zako umezipataje? Halafu taasisi za serikali na siziso za serikali kama MCT sijui kwa nini hawafanyi tafiti katika masuala kama haya ili kuisaidia nchi.
Nyie mnaotafutaga 'data' sahihi ndio mnaotuleteaga shida tu! Hivi wewe huuoni umaskini ulivyotamalaki nchini mpaka upewe data sahihi! Ama kweli Nyerere alikuwa sahihi aliposema 'Tanzania itajengwa na wenye moyo!'
 
Ungesoma alichoandika yeye
 
Unafikiri watanzania wote waishi dar? Usikurupuke tu. Na pia vifaa vya ujenzi si cement tu. Ongezeko la kodi from 10% up to 25%
Hata wale waliokua wanacheza kale ka nyimbo ccm ni ile ile wamepotea kabisa wamebaki wakina Lizabona na wakudadavua nao pumzi zinakata sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…