Uchaguzi 2020 Rais Magufuli umetutia sana Moyo vijana wako kwenye suala la ajira

Wanabodi,

Huwa siandiki uzi kama sijapata hisia/kuwiwa kuandika ,siandiki kiushabiki ila napenda kushusha nyuzi nikiwa kama kijana mzalendo wa Taifa la Tanzania na mpenda maendeleo.

Huwa napenda ku- declare' kuwa mimi ni mwanachama hai wa Chama cha Mapinduzi lakini sio msifia chochote ili bora liende lakini napenda ku-analyse vitu na kuangalia vina maslai gani kwa taifa.

Kama kijana mzalendo napenda kuungana na watanzania wengine kutambua kazi nzuri iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kipindi hiki tulichowapa dhamana ya uongozi kwenye taifa hili.

Huwa sipendi kuyaelezea waliyoyafanya maana kuna nyuzi nyingi humu zinaelezea maendeleo na mikakati pamoja na miradi mikubwa yenye tija kwa taifa iliyokamilika na ambayo bado iko mbioni kukamilika,hakika hili ni jambo jema sana na Hongera CCM ,Heko Rais Magufuli.

Nautambua uwezo wako shupavu wa kulivusha taifa letu la Tanzania kwenye hiki kipindi cha miaka mitano,kwenye majanga mbalimbali yaliyotokea yakiwemo ajali za majini,hali ya nchi pamoja na hili janga la corona,haikua rahisi kama Taifa kuvuka kwenye vipindi hivi vya mapito.

Mhe Rais ,kama kijana ambae nafahamu hali za vijana wenzangu hasa hasa wale wahitimu kwa kipindi cha miaka mitano toka mwaka 2015-2020 kulikua na changamoto kubwa sana ya ajira .

Na nilipanga niandike uzi wa kuelezea jinsi vijana wanavyohangaika huku na kule kwenye suala hili mtambuka.

Sitaki kujikita sana ndani ndani kwenye vitabu vya muasisi wa Taifa hili la Tanzania akiongolea kuhusu ajira na elimu lakini wote tunajua Mwalimu Nyerere alithamini na kusisitiza sana watu wafanye kazi (ajira).

Mhe Rais,Tuongee ukweli na bahati nzuri wewe ni mpenzi wa MUNGU na ni msema kweli,Serikali imekua muajiri nambari moja kwenye Taifa hili.

Serikali imekua ikitoa ajira almost 80% kwa vijana na watu wote,na imekua ikifanya hivi kwenye idara zake nyingi zikiwemo ajira za majeshi (polisi,jwtz,magereza,zimamoto ,idara ya uhamiaji etc).

Pia Serikali kwa miaka yote imekua ikitoa ajira nyingi kwa madaktari,wahandisi ,waalimu wa msingi na sekondari n.k

Nisingependa kutaja idara zote ambazo Serikali huwa inaajiri lakini Mhe Rais kwa kipindi toka mwaka 2015 mpaka sasa Serikali haijawahi kutoa zile ajira za wengi,kwa maana nyingine tumekua na idadi ya wahitimu wengi wa vyuo vikuu na vyuo vingine toka mwaka 2015 mpaka sasa .

Hii ni kusema tuna graduates wa intake kama 5 au 6 toka mwaka 2015 ambao wengi wao wako mtaani na wameshindwa kujiajiri na wala hawajaajiriwa na sekta binafsi.

Nimesikiliza kwa makini Mkutano wako wa kampeni leo pale segerea,na ukaongelea kipaumbele chako cha kwanza ambacho ulikifanya cha "Kudumisha Amani na Usalama", ukaongelea hali ilivyokua wakati unaingia madarakani ,kwamba hakukua Hali nzuri ya Usalama na ukatoa mifano ya kuuwawa kwa askari kibiti na lile tukio la Ubungo la majambazi kuiba NMB Mhe Rais nikupongeze hapo ulifanikiwa na umefanikiwa sana, HATUNA ujambazi wala wizi wa kutumia silaha tena,hali ni shwari na tunajisikia kweli tuko kwenye nchi yetu.(KONGOLE SANA).

Mhe Rais,kwenye suala la ajira kiukweli kabisa ndani ya kipindi hiki toka 2015 mpaka sasa serikali ni HAIJAFANYA vizuri kwenye hii sehemu.

Kuna sababu nyingi,labda serikali ilikua ina vipaumbele vingine vya haraka sana vya kufanya ndani ya miaka hii mitano,mfano huwezi kuanza na kipaumbele cha Ajira kwa vijana wakati kuna kipaumbele cha haraka cha Amani na usalama wa Raia.

So kwa mantiki hiyo naelewa kwa nini Serikali yetu haikutoa kipaumbele cha AJIRA kwa vijana kwenye miaka hii mitano ya uongozi wako.

Mhe Rais Magufuli, nimesikiliza maneno yako haya ya leo kwa umakini sana na nikayatafakari jioni ya leo ,naomba niyarudie hapa kwa kunukuu ...

" Vijana wanakosa Ajira,Vijana wanadharaulika,Wengine wamemaliza kusoma hawapati Ajira"
"Miaka mitano inayokuja nataka suala la ajira NILISHUGHULIKIE kwa nguvu zote,kama tunaweza kupandisha uchumi,kujenga Flyover,siwezi kushindwa suala la ajira kwa vijana".

Mhe Rais Magufuli, maneno haya na ahadi hii ulikua unaisema ukiwa unamaanisha na naamini imetoka ndani ya sakafu ya moyo wako, na inaonesha wazi unajua kila jambo linaloendelea kwa vijana wako wahitimu wa Tanzania.

Vijana waliosoma kwa kodi za watu maskini,vijana ambao wana matumaini ya kuingia kwenye soko la ajira,vijana ambao umesema wanadharaulika,Tafadhali usiwaache hawa vijana Mhe Rais.

Tumeashuhudia nafasi nyingi za kazi zilizokua zinatangazwa kupitia UTUMISHI ,na tumeona UMATI wa watu wengi wakijitokeza pale DUCE kwa ajili ya usahili .

Juzi juzi tumeona msururu mrefu wa vijana pale uwanja wa mkapa tena wahitimu wakiwa wanagombea kuingia kwenye usahili wa nafasi za muda za NEC,Mhe Rais hii inaonesha vijana wako wana ARI ya kufanya kazi kwa bidii ndo mana wanastahimili kukaa kwenye foleni ndefu za kungojea usahili.

Huku kwenye sekta binafsi Mhe, taasisi binafsi zinawatumia vijana hawa kwenye INTERNSHIPS na VOLUNTEERING zisizo na mwisho,kweli kuna kujitolea kwenye kupata ujuzi wa kazi lakini kuna makampuni yanawatumia hawa vijana kwenye shida zao kwa KUWANYONYA nguvu zao na kutowapatia japo kifuta jasho.

Mhe Rais sisemi uchukue vijana wote utoe AJIRA kwao,la hasha bali Serikali yako tukufu inaweza ikaandaa mikakati ya kutosha kwenye hili suala mfano Serikali iandae Mazingira wezeshi ya vijana kujiajiri,Serikali iandae program za kuwanoa vijana kwenye suala la ajira,pale TAESA wanajitahidi ila sio sana.
Serikali iangalie fursa za ajira kwa vijana wake pia nnje ya Tanzania mfano kiswahili kinakua sana africa na duniani kwa ujumla na tuna wahitimu wengi watalaamu wa kiswahili.

Mhe Rais madamu umesema unajua kwamba "Vijana WANADHARAULIKA basi fanya kitu kwa kundi hili "

Serikali yako tukufu iandae hata miswada iende bungeni ikawe sheria kuhusu mazingira wezeshi ya ajira kwa hawa vijana wako.

Mhe ,kama tulivyokomaa kwenye kupandisha uchumi wa nchi yetu basi tukomae hawa vijana wawe pia kwenye daraja la kati kwenye upatikanaji wa ajira na mazingira wezeshi ya ajira (Favourable).

Na umesema leo suala hili la ajira UTALISHUGHULIKIA kwa NGUVU zote basi sisi hatuna shaka na wewe.,MUNGU akupe nguvu kwenye hili,ulikumbuke na vijana wa Tanzania watakukumbuka sana.

Ulikua na mambo mengi sana,programs nyingi sana zipo kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili na umekua nazo bize sana kwenye kuhakikisha zinatekelezwa basi sasa ni muda muafaka wa kutumia miaka mitano inayokuja kushughulikia japo kwa asilimia 70 suala la Ajira kwa vijana.

Mhe Magufuli hakuna kama wewe,hakuna chama dume na bora kama CHAMA CHA MAPINDUZI katika kuongoza nchi.

Kama kijana mzalendo wa nchi hii sioni chama kingine cha kuwapa ridhaa ya kuongoza taifa hili kubwa kama chama chetu Tawala cha CCM.

Nirudie tu kwa kauli yako ya leo umenitia sana moyo na umetupa moyo na umerudisha matumaini kwenye vile vipande vipande vya mioyo ya vijana iliyokua imepasuka kwa ajili ya mahangaiko na husstles za kutafuta ajira kwa miaka mitano.

Naamini pasi na shaka haukusema hili la leo ili vijana tu wakupe kura,nimeona kwa macho yangu na kuamini moyoni ulilisema hili ukiwa UNAMANISHA toka ndani ya MOYO wako.,kiukweli kwa serikali kutotoa ajira kwa kipindi cha miaka mitano kimefanya kuwe na jam' kubwa sana ya wahitimu huku mitaani.

Kama serikali ingalitoa ajira toka mwaka 2015 ,tungekua na angalau haueni' kwenye soko la ajira.,kusingekua na mlundikano wa wahitimu,imefikia hatua mpaka baadhi ya watendaji wa juu wa serikali yako wanatonesha vidonda vya wahitimu hawa kwa kauli zao zisizo na staha pasi kujali Mioyo ya vijana hawa iliyopondeka pondeka.

Nimalize kwa kusema Mhe Rais Magufuli umetupa Tumaini Jipya leo kwa vijana wote wa kitanzania kwenye suala hili la ajira na Kwa niaba ya vijana wote wa Taifa hili nakuombea Afya njema na Ulinzi wa MUNGU uwe pamoja nawe kwenye kufanikisha Maono yako kwa Taifa hili.

MUNGU ibariki Tanzania.

MUNGU Ibariki Africa.

Kwa maoni na ushauri usisite kumuandikia Muandishi kwenye barua pepe godjohn8@gmail.com

CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEE.....!
Hakuna sababu ya kumuamini, aende tu jamani, wengi hatumtaki.
Kama anataka kuamini aachw uchaguzi uende fair,saa nane mchana tu tayari tutakuwa tunakula ugali tukijua tulichofanya.
TUMECHOKA
 
HAMA NCHI
 
HAMA NCHI
Kuna wajinga flani hudhani hii nchi mali yao kwahyo wenzao hawana haki ya kutoa maoni. Wala kutoa ushauri.
Wewe unaweza kuwa miongoni mwa wajinga ninaowazungumzia hapa.
Alaf kuna wajinga wengine hudhani uzalendo maana yake ni kumtetea rais aliyeko madarakani na chama chake au uzalendo ni kuwashambuliwa watu walioko nje ya chama kilichoko madarakani, wewe unaweza kuwa miongoni mwa wajinga hao..
Alaf tena kuna wapumbavu ambao hutaka anayesema kinyume na wao basi auwawe haraka sana au aadhibiwe vikali, hawa hudhani wao wataishi milele hawafi. Madaraka yanapita, comfort zones zinapita ila Tanzania itabaki na kizazi kingine
 
Wanabodi,

Huwa siandiki uzi kama sijapata hisia/kuwiwa kuandika ,siandiki kiushabiki ila napenda kushusha nyuzi nikiwa kama kijana mzalendo wa Taifa la Tanzania na mpenda maendeleo.

Huwa napenda ku- declare' kuwa mimi ni mwanachama hai wa Chama cha Mapinduzi lakini sio msifia chochote ili bora liende lakini napenda ku-analyse vitu na kuangalia vina maslai gani kwa taifa.

Kama kijana mzalendo napenda kuungana na watanzania wengine kutambua kazi nzuri iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kipindi hiki tulichowapa dhamana ya uongozi kwenye taifa hili.

Huwa sipendi kuyaelezea waliyoyafanya maana kuna nyuzi nyingi humu zinaelezea maendeleo na mikakati pamoja na miradi mikubwa yenye tija kwa taifa iliyokamilika na ambayo bado iko mbioni kukamilika,hakika hili ni jambo jema sana na Hongera CCM ,Heko Rais Magufuli.

Nautambua uwezo wako shupavu wa kulivusha taifa letu la Tanzania kwenye hiki kipindi cha miaka mitano,kwenye majanga mbalimbali yaliyotokea yakiwemo ajali za majini,hali ya nchi pamoja na hili janga la corona,haikua rahisi kama Taifa kuvuka kwenye vipindi hivi vya mapito.

Mhe Rais ,kama kijana ambae nafahamu hali za vijana wenzangu hasa hasa wale wahitimu kwa kipindi cha miaka mitano toka mwaka 2015-2020 kulikua na changamoto kubwa sana ya ajira .

Na nilipanga niandike uzi wa kuelezea jinsi vijana wanavyohangaika huku na kule kwenye suala hili mtambuka.

Sitaki kujikita sana ndani ndani kwenye vitabu vya muasisi wa Taifa hili la Tanzania akiongolea kuhusu ajira na elimu lakini wote tunajua Mwalimu Nyerere alithamini na kusisitiza sana watu wafanye kazi (ajira).

Mhe Rais,Tuongee ukweli na bahati nzuri wewe ni mpenzi wa MUNGU na ni msema kweli,Serikali imekua muajiri nambari moja kwenye Taifa hili.

Serikali imekua ikitoa ajira almost 80% kwa vijana na watu wote,na imekua ikifanya hivi kwenye idara zake nyingi zikiwemo ajira za majeshi (polisi,jwtz,magereza,zimamoto ,idara ya uhamiaji etc).

Pia Serikali kwa miaka yote imekua ikitoa ajira nyingi kwa madaktari,wahandisi ,waalimu wa msingi na sekondari n.k

Nisingependa kutaja idara zote ambazo Serikali huwa inaajiri lakini Mhe Rais kwa kipindi toka mwaka 2015 mpaka sasa Serikali haijawahi kutoa zile ajira za wengi,kwa maana nyingine tumekua na idadi ya wahitimu wengi wa vyuo vikuu na vyuo vingine toka mwaka 2015 mpaka sasa .

Hii ni kusema tuna graduates wa intake kama 5 au 6 toka mwaka 2015 ambao wengi wao wako mtaani na wameshindwa kujiajiri na wala hawajaajiriwa na sekta binafsi.

Nimesikiliza kwa makini Mkutano wako wa kampeni leo pale segerea,na ukaongelea kipaumbele chako cha kwanza ambacho ulikifanya cha "Kudumisha Amani na Usalama", ukaongelea hali ilivyokua wakati unaingia madarakani ,kwamba hakukua Hali nzuri ya Usalama na ukatoa mifano ya kuuwawa kwa askari kibiti na lile tukio la Ubungo la majambazi kuiba NMB Mhe Rais nikupongeze hapo ulifanikiwa na umefanikiwa sana, HATUNA ujambazi wala wizi wa kutumia silaha tena,hali ni shwari na tunajisikia kweli tuko kwenye nchi yetu.(KONGOLE SANA).

Mhe Rais,kwenye suala la ajira kiukweli kabisa ndani ya kipindi hiki toka 2015 mpaka sasa serikali ni HAIJAFANYA vizuri kwenye hii sehemu.

Kuna sababu nyingi,labda serikali ilikua ina vipaumbele vingine vya haraka sana vya kufanya ndani ya miaka hii mitano,mfano huwezi kuanza na kipaumbele cha Ajira kwa vijana wakati kuna kipaumbele cha haraka cha Amani na usalama wa Raia.

So kwa mantiki hiyo naelewa kwa nini Serikali yetu haikutoa kipaumbele cha AJIRA kwa vijana kwenye miaka hii mitano ya uongozi wako.

Mhe Rais Magufuli, nimesikiliza maneno yako haya ya leo kwa umakini sana na nikayatafakari jioni ya leo ,naomba niyarudie hapa kwa kunukuu ...

" Vijana wanakosa Ajira,Vijana wanadharaulika,Wengine wamemaliza kusoma hawapati Ajira"
"Miaka mitano inayokuja nataka suala la ajira NILISHUGHULIKIE kwa nguvu zote,kama tunaweza kupandisha uchumi,kujenga Flyover,siwezi kushindwa suala la ajira kwa vijana".

Mhe Rais Magufuli, maneno haya na ahadi hii ulikua unaisema ukiwa unamaanisha na naamini imetoka ndani ya sakafu ya moyo wako, na inaonesha wazi unajua kila jambo linaloendelea kwa vijana wako wahitimu wa Tanzania.

Vijana waliosoma kwa kodi za watu maskini,vijana ambao wana matumaini ya kuingia kwenye soko la ajira,vijana ambao umesema wanadharaulika,Tafadhali usiwaache hawa vijana Mhe Rais.

Tumeashuhudia nafasi nyingi za kazi zilizokua zinatangazwa kupitia UTUMISHI ,na tumeona UMATI wa watu wengi wakijitokeza pale DUCE kwa ajili ya usahili .

Juzi juzi tumeona msururu mrefu wa vijana pale uwanja wa mkapa tena wahitimu wakiwa wanagombea kuingia kwenye usahili wa nafasi za muda za NEC,Mhe Rais hii inaonesha vijana wako wana ARI ya kufanya kazi kwa bidii ndo mana wanastahimili kukaa kwenye foleni ndefu za kungojea usahili.

Huku kwenye sekta binafsi Mhe, taasisi binafsi zinawatumia vijana hawa kwenye INTERNSHIPS na VOLUNTEERING zisizo na mwisho,kweli kuna kujitolea kwenye kupata ujuzi wa kazi lakini kuna makampuni yanawatumia hawa vijana kwenye shida zao kwa KUWANYONYA nguvu zao na kutowapatia japo kifuta jasho.

Mhe Rais sisemi uchukue vijana wote utoe AJIRA kwao,la hasha bali Serikali yako tukufu inaweza ikaandaa mikakati ya kutosha kwenye hili suala mfano Serikali iandae Mazingira wezeshi ya vijana kujiajiri,Serikali iandae program za kuwanoa vijana kwenye suala la ajira,pale TAESA wanajitahidi ila sio sana.
Serikali iangalie fursa za ajira kwa vijana wake pia nnje ya Tanzania mfano kiswahili kinakua sana africa na duniani kwa ujumla na tuna wahitimu wengi watalaamu wa kiswahili.

Mhe Rais madamu umesema unajua kwamba "Vijana WANADHARAULIKA basi fanya kitu kwa kundi hili "

Serikali yako tukufu iandae hata miswada iende bungeni ikawe sheria kuhusu mazingira wezeshi ya ajira kwa hawa vijana wako.

Mhe ,kama tulivyokomaa kwenye kupandisha uchumi wa nchi yetu basi tukomae hawa vijana wawe pia kwenye daraja la kati kwenye upatikanaji wa ajira na mazingira wezeshi ya ajira (Favourable).

Na umesema leo suala hili la ajira UTALISHUGHULIKIA kwa NGUVU zote basi sisi hatuna shaka na wewe.,MUNGU akupe nguvu kwenye hili,ulikumbuke na vijana wa Tanzania watakukumbuka sana.

Ulikua na mambo mengi sana,programs nyingi sana zipo kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili na umekua nazo bize sana kwenye kuhakikisha zinatekelezwa basi sasa ni muda muafaka wa kutumia miaka mitano inayokuja kushughulikia japo kwa asilimia 70 suala la Ajira kwa vijana.

Mhe Magufuli hakuna kama wewe,hakuna chama dume na bora kama CHAMA CHA MAPINDUZI katika kuongoza nchi.

Kama kijana mzalendo wa nchi hii sioni chama kingine cha kuwapa ridhaa ya kuongoza taifa hili kubwa kama chama chetu Tawala cha CCM.

Nirudie tu kwa kauli yako ya leo umenitia sana moyo na umetupa moyo na umerudisha matumaini kwenye vile vipande vipande vya mioyo ya vijana iliyokua imepasuka kwa ajili ya mahangaiko na husstles za kutafuta ajira kwa miaka mitano.

Naamini pasi na shaka haukusema hili la leo ili vijana tu wakupe kura,nimeona kwa macho yangu na kuamini moyoni ulilisema hili ukiwa UNAMANISHA toka ndani ya MOYO wako.,kiukweli kwa serikali kutotoa ajira kwa kipindi cha miaka mitano kimefanya kuwe na jam' kubwa sana ya wahitimu huku mitaani.

Kama serikali ingalitoa ajira toka mwaka 2015 ,tungekua na angalau haueni' kwenye soko la ajira.,kusingekua na mlundikano wa wahitimu,imefikia hatua mpaka baadhi ya watendaji wa juu wa serikali yako wanatonesha vidonda vya wahitimu hawa kwa kauli zao zisizo na staha pasi kujali Mioyo ya vijana hawa iliyopondeka pondeka.

Nimalize kwa kusema Mhe Rais Magufuli umetupa Tumaini Jipya leo kwa vijana wote wa kitanzania kwenye suala hili la ajira na Kwa niaba ya vijana wote wa Taifa hili nakuombea Afya njema na Ulinzi wa MUNGU uwe pamoja nawe kwenye kufanikisha Maono yako kwa Taifa hili.

MUNGU ibariki Tanzania.

MUNGU Ibariki Africa.

Kwa maoni na ushauri usisite kumuandikia Muandishi kwenye barua pepe godjohn8@gmail.com

CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEE.....!
Umeandika mnoo ila umeshindwa kuainisha "uongo" dhahili, mwenzio kasema kuwa miaka hiyo mitano katengeneza ajira milioni sita!!! Na sasa anajifikilia kutengeneza milioni nane! Au hukumsikia au hukuelewa?
 
Back
Top Bottom