HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,212
- 1,552
Habari wanaJF,
Kama mjuavyo, kasi ya 'utumbuaji majibu' imeshamiri. Imepamba moto kiasi kwamba wapo waliobeba kaulimbiu hii 'kikasuku' bila ya kuangalia mipaka ya mamlaka zao.
Niharakishe kutamka hapa kwamba naunga mkono harakati za Rais JPM za kudhibiti wizi 'uliohalalishwa' Serikalini na Taasisi za Umma,kujenga nidhamu kwenye utumishi wa Umma,kudhibiti ukwepaji kodi n.k. Nchi ilikua kwenye 'auto pilot'. Imegeuzwa shamba la bibi,imekua maficho ya wadudu kama mchwa na kupe. Lakini pia kuna 'cannibals'.
Pamoja na juhudi hizi,ni hatari kutegemea mtu au kikundi cha watu kunyoosha mambo.Hili ni suala la nyakati.Hatuwezi kupata Magufuli na Nyerere kila siku.Jambo bora na lenye afya kwa mustakabali wa nchi ni KUSUKA MFUMO MADHUBUTI wa kuongoza nchi yetu.
Hapo ndipo penye ULAZIMA wa Katiba mpya.Katiba ya wananchi (wenye nchi),sio Katiba ya wanasiasa au genge la watu fulani.Tunataka Katiba yetu.Na pa kuanzia kupo.Tuanzie pale kwenye Rasimu ya pili ya Tume ya Katiba.Katiba inayopendekezwa ni ya wanasiasa na washirika wao.
Sisi wananchi HATUITAKI.
Rais Magufuli,tunakuomba sana,kama kweli unawatetea wanyonge,tupatie Katiba yetu.Najua mahafidhina kwenye chama chako hawataki kuiona rasimu ya Warioba,lakini jua kwamba wanyonge wana matumaini makubwa kwako.Tupatie Katiba,hakutokua na tabu tena ya kutumbua majipu kwa mikono kwani Rasimu ile imebeba 'zana' za kutumbulia.
Rais Magufuli,tunataka Katiba mpya.Naanza mimi 'kupiga mayowe'.Chonde chonde Rais wetu,usiondoke bila ya kutuachia alama yako.