makamanda , kwa kweli katika usanii ambao tunaendelea kuushuhudia ni chama kukosa katibu mkuu kwa ziadi ya miezi sita. tunakubali kabisa alivyokiri Mbowe kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuvaa viatu vya Dr Slaa , lakini chama hakiwezi kuendeshwa kisanii sanii hivi! katibu mkuu ndie mtendaji mkuu wa mambo yote. hivi sasa mambo ni holela tuu ! mwenyekiti anaamua kila kitu tena siku hizi kiongozi mkuu wa chama Lowasa ndio kila kitu. kiongozi mwenyewe hajawahi kuripoti ofisini kinondoni hata mara moja. yeye anaongoza kwa remote control kutoka ofisini kwake Mikocheni. siasa za ajabu kabisa. alafu ndio chama hiki kilitaka kupewa ridhaa na wananchi kishike dola. khaaa !!!!! kwa lipi hasa. kushika dola si mchezo makamanda. hatujawa tayari.
tufanye yafuatayo.
1) tumchague Sumaye awe katibu mkuu.
2) Lowasa apewe rasmi kuwa kiongozi mkuu wa chama kama alivyo Zito Kabwe.
3) Msindai awe naibu katibu mkuu
4) Mzee Kingunge awe mshauri mkuu
5) Mpeni Lembeli cheo walau ajisikie kuwa hakufanya maamuzi fyongo maana nilimuona kachoka na nadhani anajuta kwa nini alifanya maamuzi yake.
6) Makongoro Mahanga mpeni idara ya ulinzi na propaganda.
ni hayo tu.
cc. Kamanda Mbowe
Tundu lissu.