Vijana wa chadema ongezeni uwezo wa kuhoji

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
Na Thadei Ole Mushi.

Kuna nyimbo zinaimbwa sasa na watu wa karibu na Mbowe kuwa Operarion 255 zinatumia fedha za mwenyekiti Mbowe na kuwataka watu wengine kuchangia chama kama Mbowe anavyofanya.

Ok twende sawa hapa

Haya yanayotokea CHADEMA hata CCM yapo kama kulivyo na ujinga mwingi sana ndani ya vichwa vya watu wa Chadema kuhusu matumizi ya fadha za chama chao ndio hivyo hivyo ndani ya CCM kuna watu wajinga kuhusu uendeshaji wa CCM. As long as ni kiongozi wa Chama kasema inakuwa tu Tawire baba….. huwa najitofautisha na katika hili la Mbowe kutumia Fedha zake kuendesha chama naomba pia nijitofautishe na Rafiki yangu Martini M.M aliyeandika kuwa Mbowe anatumia fedha zake binafsi kukiendesha Chama.

Wengi wanadai Mbowe anajitolea pesa zake kutoka ktk biashara zake.Huu ni ujinga wa kiwango kikubwa sana.Hivi Mbowe anafanya biashara gani? Ziko wapi? Analipa kodi kiasi gani? Faida anayopata ni kiasi gani kuwezesha kuchota pesa ya kurusha chopper?

Labda watu hawajui. Mruko wa chopper ya kukodi kwa saa moja ni dollar 2000 sawa na sh. za Kitanzania 4,700,000/= kama haijabadilika kwa mujibu wa miruko ya Chopa kipindi cha Kampeni 2020 naamini kwa sasa imepanda nitaulizia. Kuna mfanya biashara yeyote anaeweza kufanya hilo? Yaani kurusha chopper siku nzima mwezi mzima kwa kujitolea? Kwa mikutano ya Chadema Chopa inaruka si pungufu ya masaa nane yaani hapo ni sawa na Dola 16,000 sasa chukua hesabu hiyo ni kila siku zidisha mara mwezi kweli tumegoma kutumia akili zetu? basi kama za darasani tumegoma hata zile za kuzaliwa mbona zinatosha kutafsiri hili?

Ndani ya Chadema hakuna mwenye uwezo wa kumhoji Mbowe kuhusu mapato na matumizi ya pesa zozote za chama; yaani ruzuku na mapato mengine.

Source za pesa ni nyingi sana. Mlisikia ziara ya Ujerumani na ahadi ya euro mil 50 kwa ajili ya haki za binadamu? Mashirika ya aina hiyo yanayotoa pesa na Wanachadema wangapi wanayajua? Hata katibu mkuu wa chama hana ubavu wa kuulizia hizi fedha.

Kuna source nyingine za wadau ambazo zinapitia moja kwa moja kwake. Je! huwa ana declare kwenye chama kama anavyopokea?

Nakumbuka kuna mfanyabiashara marehemu (Mchaga wa machame) alisaidia kampeni bil 2. Baadala ya kusema wazi ni fedha za chama toka kwa mfadhili alisema ni mali yake na ruzuku ilipoingia alikuwa akilipwa mil 50 kila mwezi kama marejesho ya deni hewa. Yaani unachukua Bilioni mbili za msaada unazibadili kuwa zako then unaanza kudai zilipwe hili nalo ni la kutafuta na Tochi?

Wabunge wa Chadema walikuwa wakikatwa sh. Mil 1.5 wabunge wa majimbo na mil 1.7 wabunge wa viti maalum kila mwezi kutunisha mfuko wa uchaguzi na zilikuwa zinawekwa ktk fixed deposit acct.

Mbowe alichukua fedha zote na kuanzisha mradi wa kilimo Ifakara. Waziri Lukuvi baadae alidai ardhi ya mradi ilikuwa mali ya serikali mradi ukafa na pesa zikapotea.Wote waliohoji walisukumiwa kashfa ya kuwa CCM B na kutengwa au kutoka kwenye chama.

Aliponunua Ford rangers za chama declaration ndani ya chama ilikuwa mil 130 kila moja lakini CMC DAR zilikuwa zikiuzwa mil. 90. Lakini zikaagizwa kwa milion 130 sawa na kila moja genji la milioni 40 hili nalo lipo wazi kabisa…. Halafu tunapata wapi ujasiri wa kuhoji vitabu vya hesabu za CAG?

Kuna kitu mnaweza kuniambia nikakubali kuhusu Mheshimiwa Mbowe cha kwanza ni kweli ana fedha na katokea familia yenye fedha toka akiwa utotoni ila hawezi kuzitumia kama mnavyotaka tuamini. Cha pili Mbowe ni kifaa kweli kweli cha Siasa za Upinzani kuwahi kutokea Tanzania. Huwa ana uwezo wa kuiendesha Serikali na CCM katika uelekeo anaoutaka hili halina ubishi. Lakini pia anakioenda Chama chake cha chadema sana….

Yote haya hayamfanyi kukosa asili yetu ya Uchaga ya utafutaji wa fedha na matumizi yake. Yote haya hayamfanyi awe malaika naye kama sehemu ya kukamilisha ubinadamu wake hakosi mapungufu.

Nadhani Chadema wasishangilie kuwa Mbowe ana uwezo wa kukiendesha chama chake kwa fedha zake, chadema ilipo imeshafikisha Umri wa Mtu Mzima inaweza kujiendesha yenyewe bila fadhila za mwanachama mmoja.

Ni hatari chama kuendeshwa na fadhila za mtu mmoja siku akiwa hayupo chama Kitakufa?
 
Umesikia wapi kuwa hela inayotumika anatoa Mbowe?
 
..hiyo ni homa iliyosababishwa na operation 255.

..naona sasa mashambulizi yanaelekezwa kwa Mbowe.

..mashambulizi dhidi ya Lissu yamegonga mwamba.

..kuna timu ya Mch.Msigwa inafanya mikutano kanda ya Nyasa.
 
kwani tatizo liko wapi?
kama ccm na serkalini kila mtu anakula kwa usawa wa kamba yake (shahidi CAG), kuna shida gani upinzani nao wakala kwa usawa wa kamba zao?, bahati mbaya kwa serikali wanakula kodi za wa tz masikini wakat mbowe anakula michango ya marafiki na wabunge matajiri.
kama inakuuma nawewe tafuta mahali ule.
 
Back
Top Bottom