Brown Ashika Tama
New Member
- May 23, 2020
- 1
- 0
Mh. RAIS WETU
Kwanza kabisa napenda kukupa pole kwa majukumu mazito ya kulijenga taifa uliyonayo tuliyokutwisha tangu mwaka 2015.
Vile vile napenda kukupa pongezi na hongera kwa mambo makubwa unayofanya na hatua nzuri unazochukua za kutujari watanzania ikiwemo kutuepusha na janga la homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).
Bila kusahau mikakati mizuri ya kukuza uchumi wa nchi yetu unayochukua na hatimaye jana tumetangazwa na benki ya dunia kuwa sasa rasmi sisi ni miongoni mwa nchi kumi bora barani afrika zenye uchumi mkubwa. Hakika tunajivunia kukupata kiongozi mwenye maono sahihi unayetekeleza ilani ya chama chetu cha mapinduzi kwa vitendo.
Mheshimiwa Rais na mwenyekiti wangu wa chama, sisi pia kama vijana hatuko nyuma, tunahakikisha tuko na wewe bega kwa bega katika kukutea na kulinda chama chetu kwa nguvu zote kwenye mitandao ya kijamii na jamii tunazoishi kwa kutangaza mambo mazuri uliyoyafanya ndani ya miaka yako mitano ya uongozi.
Tunatambua ni jukumu letu kuyatangaza kwa sababu tusipofanya hivyo wale wenzetu wale wa kupinga pinga kila kitu wanaweza kuyapaka matope na kufanya yaonekane mabaya.
Mheshimiwa, nilipokuwa kwenye harakati za kujenga chama nimekutana na makundi mbali mbali ya vijana na kweli mwitiko wa vijana wanaokuunga mkono ni mkubwa mno. Wapo wa chama chetu, wasio na vyama na wa vyama vya upinzani ambao wote kwa umoja wao wamenituma ujumbe nikuletee.
Mheshimiwa, wanasema kama Mungu akijaalia uwakumbuke kuhusu ajira wapo wengine wameniambia nikukumbushe ahadi yako ya ajira za ualimu ukiwa unafungua mkutano wa uchaguzi wa chama cha walimu CWT jijini dodoma na wengine wa fani zingine.
Kuhusu uchaguzi, Vijana Wamesema huna mpinzani kwa sababu mambo makubwa uliyofanya watanzania wanayaona na kuyaishi, lakini ujumbe mkubwa zaidi ni huo wa kuwakumbuka kupitia ajira ili wapate nguvu zaidi ya kukipigania kwa hali na mali na kukiwezeshea chama chetu ushindi wa kishindo cha asilimia mia moja.
Kwakuwa sikuwa na njia nyingine nimeamua kutumia njia hii kukufikisha ujumbe huo hivyo kama nitakuwa nimekiuka taratibu za chama kwa namna moja au nyingine naomba radhi sana kwa chama changu.
Mwisho nakutakia majukumu mema na Mungu azidi kukubariki na kukuongezea maono zaidi ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo watanzania.
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI