VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
- Uteuzi wa Kangi Lugola kuwa Naibu Waziri na sasa Waziri wa Mambo ya Ndani. Huyu alishtakiwa kwa kesi ya kupokea rushwa mahakamani na TAKUKURU. Jamhuri ikawasilisha hati mahakamani ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka. Jamhuri iliyomshtaki ni Serikali ya awamu ya nne. Alishtakiwa kimakosa na Serikali ya mtangulizi wako hadi sasa awe safi na kuwa Waziri?
- Uteuzi wa Alexander Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa .Ni kama ulimpandisha cheo baada ya kuanikwa kwa video zinazomuonesha akipanga mipango ya kuwanunua Madiwani wa CHADEMA. Ushahidi ulikabidhiwa kwa TAKUKURU na hadi leo hakuna lolote lililofanyika. Kumpa ukuu wa mkoa ni kuonesha kuwa ni mtu safi?
- Uteuzi wa Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru. Huyu alikamatwa na pingu na alishtakiwa na Jamhuri/Serikali ya mtangulizi wako mahakamani kwa makossa mbalimbali ya rushwa na kukutwa na pingu. Uteuzi wake ni kuonesha kuwa ni mtu safi na alionewa na Jamhuri?
- Uteuzi wa Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Huyu alikamatwa na polisi na kushtakiwa na Jamhuri kwa kujifanya Usalama wa Taifa. Alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha. Polisi walidai alighushi kitambulisho cha Usalama wa Taifa na kesi yake ikaisha ilivyoisha. Ana usafi gani hadi awe Mkuu wa Wilaya? Alionewa na Jamhuri/Serikali iliyokutangulia?
- Uteuzi wa Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Huyu aliripotiwa 'kumshugulikia' Mbowe wa CHADEMA kwa kuharibu shamba lake la mbogamboga. Wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Kuna kesi ya madai dhidi yake kuhusu uharibifu huo. Alikufurajisha kipi hasa hadi ukampandisha cheo kuwa mkuu wa mkoa?
- Uteuzi wa Daudi Albert Bashite alias Paul Makonda wa Dar. Huyu anasemwa kuwa ana vyeti vya elimu vya kughushi. Yaani, hana vyeti halali vya elimu yake. Inasemwa pia kuwa ana utajiri wenye ukakasi. Akawa Mkuu wa Mkoa wa Dar baada ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Kwa lipi hasa?
Ukonga na Monduli 'tutashinda' ila chamoto tunakiona!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam