Rais Magufuli tafadhali ibinafsishe TANESCO

Tanesco ikibinafsishwa umeme hautashikika kwa bei yake na vibatari, chemli na mishumaa vitahusu sana tu.

Sasa tufanyeje au ndio tukubali kuanza kutumia vibatari?
 
Wakichukua wazungu, TANESCO ikianza kufanya vizuri, mgao wa umeme ukaisha, mtaanza kuwaambia, 'wametuibia sana', mtaunda tume zenu uchwara halafu mje kusema wanadaiwa matrilioni ya shilingi, 'kama hawataki kulipa nitawafukuza'.

Hakuna wa kuja kuwekeza Tanzania sahizi. Tumechagua dhiki, lazima tukubali kufa na tai shingoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama yeye mwenyew Ana 30% yake mnadhani atagusa mzizi wake ataishia kugusa matawi tu ili mpige makofi
 
Aaaaaaah kubinafsisha Tanesco inawezekana ila Ndo shirika litakufa mazima.
 
Ni kilo cha kila siku kwa mamilioni ya wa Tanzania juu ya utendaji usiyo kidhi kutupatia huduma ya umeme lkn bado serikali imelifumbia macho kama vile hakuna kinacho endelea.Sasa tunakuomba binafsisha hao wapiga dili wa Tanesco mgao wa umeme hauishi kila siku hadi watu tunaibiwa mali zetu kisa giza mitaani!

Nafikiri kabla ya kuibinafshisha, serekali iwe ina NIA ya dhati ya kuondoa matatizo ya umeme nchini na UELEWA wa chanzo/vyanzo vya huduma MBAYA za umeme kutoka TANESCO.
Baada ya kuwa na uelewa huo, ndio wajiridhishe kama jawabu la kuviondoa/kuvidhibiti vyanzo hivi ni kueweka TANESCO chini ya umiliki binafsi au la.

Je matatizo ya TANESCO yapo kwenye uzalishaji, usambazaji (transmission), ugawaji, rasilimali watu au vyote?

Nadhani moja ya changamoto la TANESCO katika ugawaji wa umeme ni MIPANGO MIJI mibovu. Hii huondoa mantiki na hitaji la TANESCO kuweka miundombinu ya kudumu katika ugawaji wa umeme, kwa mfano kupitisha umeme chini ya ardhi, kuweka nguzo za zege/chuma, kuweka transformer kwenye vyumba maalumu, n.k. Uwekaji wa miundombinu ya ya kudumu ya ugawaji wa umeme utaipunguzia sana TANESCO gharama za matengenezo na hasara itokanayo na ukosefu wa huduma, wakati huohuo ikiwapa wananchi huduma bora.

Siwezi kuelezea vya kutosha UMUHIMU wa kuwa na miji/vitongoji vilivyopangwa vyema.
Ndio, huduma ya umeme wa TANESCO ni MBAYA sana! Lakini je chanzo chake ni kipi? Na tunakitatua vipi?
 
Umejitahidi sana kufafanua vizuri ila umesahau na serikali kuanzisha miradi kisiasa kama vile hii ya REA ambayo inaongeza mzigo kutoka kwenye vyanzo vya umeme bila kuzingatia uwezo halisi wa hiyo mitambo
 
Back
Top Bottom