Rais Magufuli: Suluhu ya Zanzibar ni Uchaguzi wa marudio

Na endapo dhifa ilitakiwa kufanywa na waziri, njia bora ilikuwa kuandaa Hotelini (naogopa watakurupuka gharama)

Leo wanaitwa 'nyumbani' mwenye nyumba kasepa! hata katika logic za mitaani haiingi akilini
Unamwalika rafiki yako 'host' anakuwa mdogo wako! teh teh

Mabalozi ni wawakilishi wa wakuu wa mataifa mengine. Inawezakaje kuwakimbia?

Nadhani hofu ni lile tangazo la kuwazuia wasifanye kazi zao au hili la ZNZ au kuna jingine. Haiwezekani lipo jambo!

Hivi the Boss unakumbu kumbu zozote ikiwa ilishawahi kutokea huko nyuma mabalozi kuitwa Ikulu na Rais akakacha?
 
The Boss hii jambo ni zito, watetezi wa #Hapakazi wakiwemo ''46 wanaofikiriwa'', nawaona wanyoonge! Sura zimeswajika, wamekumbwa na mfadhaiko, simanzi tele huku wakiwa wametunduwaa

Wanajiuliza waanzie wapi kutetea hili.
 

Una hakika nani rais ndiye aliwaalika mabalozi na sio Foreign Minister? Na ni wapi imeandikwa kuwa event ya mabalozi lazima rais awepo?

Kwenye matumizi, Yes, serikali inabana matumizi, lakini haizui vikundi vya hiari kufanya sherehe zake.
 
Magufuli &co pelekeni vifaru na majeshi huko zanzibar ili mufanye uchaguzi ila nakuhakikishia wazanzibar hawatorudi nyuma kurejesha mamlaka yao,na hata kama mtawauwa wote basi haki yao haipotei itarudi tu kwa wazanzibar.
 
Una hakika nani rais ndiye aliwaalika mabalozi na sio Foreign Minister? Na ni wapi imeandikwa kuwa event ya mabalozi lazima rais awepo?

Kwenye matumizi, Yes, serikali inabana matumizi, lakini haizui vikundi vya hiari kufanya sherehe zake.
Wapi imeandikwa event ya mabalozi ifanyike Ikulu hata kama ni waziri ameandaa!

Serikali inabana matumizi wakati serikali nzima imesafiri kwa gharama za umma kwenda shughuli za vikundi binafsi! ebo!

Ulinzi, magari, madereva, wasaidizi n.k. unadhani vinatolewa na CCM
 
Baada ya Singida, kubana matumizi ilihamia Dodoma.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu Maalum ya CCM, leo, Ikulu Ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.

 
Tume huru ipi unayoisema hapa Kirikou? Tume ya Jecha? Weka wazi, Tume huru ipi hiyo?
Kama CCM imeshinda Tanganyika(Tanzania bara) kwa nini pia uchaguzi huku haurudiwi ili watanzania wajiridhishe kama kweli CCM walishinda? Kama CCM walishinda,watashinda tena, wapiga kura waliopigia CCM ni wale wale, wanaogopa nini kuitisha uchaguzi wa marudio?
Tume ya Lubuva ni huru? Kwa nini ilitupilia mbali maombi ya Chadema ilipolalamikia kasoro za uchaguzi?
 
Yaani CUF wakithibitisha uchaguz hautarudiwa?
Anadai wathibitishe kwa kukubali kushiriki uchaguzi na kushinda.
Hata hivyo najua kuna kitu wanakiogopa. Kama ameshasema kuwa vyama vingine pamoja na CCM wanautaka uchaguzi wa marudio, kuna haja gani ya kuitajataja CUF kila mara? By the way, hivyo vyama vingine vilivyoshiriki mazungumzo ndio vipi?
 
Una hakika nani rais ndiye aliwaalika mabalozi na sio Foreign Minister? Na ni wapi imeandikwa kuwa event ya mabalozi lazima rais awepo?

Kwenye matumizi, Yes, serikali inabana matumizi, lakini haizui vikundi vya hiari kufanya sherehe zake.
Moja Waziri awaalike Mabalozi lakini asome hutuba ya Rais? Inawezekana wanahabari wameandika kimakosa kuwa Mahiga alimwakilisha Rais?

Pili, Wizara ya Mahiga haina ukumbi wake wa mikutano? Kwa nini Mkusanyiko huo haukufanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Mahiga au Ukumbi wa hoteli ya bei poa?

Tatu kwa nini Mahiga amewasimamisha Mabalozi kama watoto wa shule wanaotakiwa kuimba kwaya?
 
Hapa Kikwete anajiwakilisha.
 

Mkuu kabla hatujakwenda mbali kujadili Tume ya Jaji Lubuva, mkuu napenda kujua uchaguzi bara unataka urudiwe kumfurahisha nani?
 
Wateuane tu kwani hamna haja ya kupiga kura tena inchi hii iwe tanganyika au zanzibar naona kiini macho tu
 
yaan hili la Zanzibar limewakalia vibaya sana ccm kweli wizi unamwisho ujanja ujanja wa ccm naona kama umegota.sasa leo rais magufuli kaamua kufunguka waziwazi kuwa Zanzibar ni nchi inakila kitu chake! wakati pinda alivyoulizwaga bungeni alisema ni moja ya kipande cha tanzania yaa mkoa.leo rais amethibitisha! kaenda mbali eti cuf warudie kuthibitisha ushindi wao!hiv kumbe ukishinda huwa unatakiwa kurudia uchaguz tena bila kampen! na hizo pesa za marudio nan atatoa?na aliye haribu uchaguzi yuko magereza au? tume wako wamoja au wamegawanyika? eee mungu simama upande wa haki yetu sisi wazanzibar
 

Kama mapungufu yalionekana Pemba, kwa nini kufuta uchaguzi wote? Nani aliyelalamika kuhusu mapungufu hayo ya Pemba?
 
Sio Bure wanahitaji maombi!
this
magu's speech is purely propaganda
 
This is a joke kwa mabalozi ambao walituma waangalizi sehemu zote na kuridhika.
Kwanza kawakimbia mabalozi .
Sijawahi kusikia mtu kualika wageni halafu ukajifungia chumbani
Yaani hapo ndo simuelewi JPJM! Kwa nini anapenda kuwakilishwa kila mahali; hata humu humu nchini? Mimi nafikiri ikulu inabidi wafike mahali watuambie tu ukweli wa tatizo au mkakati wa huyu mheshimiwa sana!
 
The Boss hii jambo ni zito, watetezi wa #Hapakazi wakiwemo ''46 wanaofikiriwa'', nawaona wanyoonge! Sura zimeswajika, wamekumbwa na mfadhaiko, simanzi tele huku wakiwa wametunduwaa

Wanajiuliza waanzie wapi kutetea hili.
Huu uharamia wanaoufanya hao mahafidhina wa CCM wachache sana ambao idadi yao inawezekana haizidi hata watu 100, naamini kabisa mamilioni ya wanaccm wenzao watakuwa hawapendezwi nayo hata chembe.

Hiyo ndiyo siri kubwa inayofanya hata wale ambao tunawaita die hard JF Lumumba team, wamelazimika waingie mitini kukwepa kabisa kujadili hoja hii, kwa kuwa hata wao nafsi zao zinasonononeka sana namna wanavyoona haki ya wazanzibari inavyotaka kuporwa kwa nguvu kwa kutumia vifaru vya kijeshi.
 
Hivyo 'Vyama Vngine' kwa mujibu wa babu duni aliponukuliwa na Mwananchi hata kura 80 havikufikisha,na kwa mujibu wa KATIBA YAO ILI KUUNDA SUK ni kwamba chama kinachofuata kuna asilimia fulani kinapaswa kufikisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…