Rais Magufuli: Suluhu ya Zanzibar ni Uchaguzi wa marudio

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Rais Magufuli ameyaeleza hayo katika hotuba yake kwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga leo ikulu jijini Dar es salaam.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli amewaeleza mabalozi hao kuwa licha ya Tanzania kuwa nchi moja, Zanzibar ina mfumo wake wa siasa, ina serikali yake, Katiba yake na pia tume yake ya uchaguzi inayojitegemea.

Amesema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Amesema mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yalifanyika bila mafanikio ambapo chama kikuu cha upinzani (CUF) kimeendelea kupinga uchaguzi wa marudio huku vyama vingine kikiwemo chama tawala vikionesha uhitaji wa uchaguzi huo wa marudio.

Amesema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

Amewaeleza mabalozi hao kuwa serikali pamoja na watanzania walio wengi wangependa kuona CUF inathibitisha madai yake ya kushinda uchaguzi huo kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa marudio.

“Tunakiasa chama cha CUF kama ambavyo watanzania wengi wangependa kuona, kuthibitisha madai ya ushindi wao katika sanduku la kura, hakuna jinsi nyingine ya kutatua suala hili zaidi ya kukubali kufanya uchaguzi wa marudio” imesema sehemu ya hotuba hiyo.

Magufuli amewahakikishia mabalozi hao kuwa nchi ni salama na hali ya amani na utulivu ni ya kuridhisha katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio.
 
Duu !!1kumbe jamaa si kuzungumza tu kumbe hata kusoma hio lugha hajui! hadi asemewe na Mahiga!
hapa kazi tu ya kukimbia tu
 
.Amesema tume hiyo ilifuta uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kisiwani Pemba, na kwamba tayari tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio imekwisha tangazwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Hapo ndipo ninapothibitisha ya kwamba Raisi wangu ni kilaza. hii statement kaandika yeye na wala haihitaji kuwa na elimu ya Rocket science kumjibu huu utumbo hapa.

Jibu lake: Zanzibar ni visiwa 2. Kama matatizo yalitokea ya uchaguzi yalitokea Pemba jee yale ya Unguja ambayo yamemalizika kulikuwa na haja gani kuufuta uchaguzi wote.

Amesema kwa hali ilivyo, busara inahitajika ili kunusuru suala hilo, na kwamba kususia uchaguzi siyo suluhu bali kutumia nafasi iliyopo sasa kujadili namna ya kuufanya uchaguzi wa marudio kuwa huru na wa haki.

Mheshimiwa Just curious jee mutakuwa tayari kuanzisha tume huru ya uchaguzi kwa uchaguzi wa marudio ama mutakuwa tayari UN wasimamie Uchaguzi huu!

Si watanzania wote ni vilaza!
 
Kuna kazi kubwa Mbele yetu,Wakati Mwingine Mwanasiasa bora ni yule Mwenye uwezo wa Kupima Maneno yake! Aongee nini,Wakati gani na kwa sababu zipi,Asiongee tu kwakuwa ana Mdomo.

Binafsi Ningeendelea kumchukulia Rais Magufuli kama alivyokuwa kuliko kuliongelea hili suala la Zanzibari Dizaini flani haelewi Mchezo uliofanyika.
Ana tofauti Gani na Yule aliyesema "Hata mimi Nilishangaa Uchaguzi wa Zanzibari kufutwa",Dizaini fulani hawaelewi Mchezo uliofanywa Na CCM yote.

Halafu na sisi wananchi tunapiga Makofi huku tukishangilia kwa Nderemo na Vifijo!! Hebu Watanzania tuungane tuwe wamoja,Hawa wanasiasa wasitumie Uanasiasa wao kutuona Hatuna uwezo wa kufikiri.
Tulaani,Tukemee kwa Pamoja Hila na Njama zote Mbaya tunavyofanyiwa na Hawa wanasiasa!! PERIOD.
 
Pinga mwenyewe,

Sisi wengine sio Wazanzibar
 
Hata sie tumestushwa sana na Uamuzi wa Ndg Jecha Salum Jecha kufuta uchaguzi znz baada ya kuona dalili zote CCM imeshinda,tunarudia uchaguzi kwa shingo upande-Jk,
Msimuone anachekacheka jamaa ( JK) mbaya kwelikweli!-Maalim Seif
 
Back
Top Bottom