Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,846
Nimeshtushwa sana tena sana na taarifa kwamba, Rais Magufuli amewaonya wabunge wake wa CCM wanaogawa Muda wao kwa Wabunge wa Upinzani.
Pia, Rais amemwagiza baba ya mbunge mmoja wa kike amuonye mwanaye kwa kitendo chake cha kuvujisha siri za Chama kwa huyo mbunge wa Upinzani, kwanza, mwanzoni taarifa zilianza kusambaa kwamba, Halima Bulembo ndiye anayetuhumiwa kuvujisha siri za CCM kwa mbunge huyo wa Upinzani, kwamba, Halima ana mahusiano na Mbunge huyo na kwamba wamepanga kuoana na kwamba ana mimba yake, taarifa zikasema, baba yake amekorofishana na mwanaye juu ya hatua hiyo na kwamba Rais naye amechukizwa sana na kitendo cha mbunge huyo kuwa mahusiano na mbunge wa Upinzani, sasa Taarifa rasmi zimemnukuu Rais Jana akiwa na kikao na Wabunge wake wa CCM akimuonya Mbunge huyo vikali na kumwamuru Baba ya mbunge huyo amuonye mwanae...
Pia, Rais amenukuliwa akichukizwa na kitendo cha wabunge wa CCM waliotaka kwenda kumuona Lema Gerezani, nimeshangaa sana.
Rais unajenga nchi ya namna gani? yaani hujui kuwa Siasa si uadui? hulka ya watanzania ni upendo, sasa sijui unataka watanzania tusipendane?
Naamini sasa, kwa kuwa umeanza hivyo, muda si mrefu utapiga marufuku wana CCM kuhudhuria misiba ya wanachama wa upinzani.
Muda si mrefu, utachukizwa na kupiga marufuku wana CCM kutembea barabara moja au kuchota maji au kusali pamoja na wale wa upinzani, kumbuka Mh. Rais, Mwalimu Nyerere alisema, "Ukila nyama ya mtu huwezi kuacha" kwa kuwa umeanza hivo, sasa ndivyo utakavyoenenda hivo hivo, nchi ikija kushtuka, tayari tutakuwa tumishagawanyika vipande vipande.
Nawaomba sana Viongozi wa Dini mkemee hii tabia ya Mh. Rais kuanza kuonyesha dalili ya kuwagawa watanzania, watanzania wana maadili yao ambayo ni ya pekee, sasa anapotokea mtu kuanza kuyamomonyoa ni lazima akemewe sana, mbona wakati wa JK. mlikuwa mnakemea? awamu hii mmekuwaje enyi viongozi wa dini? nini kimewapata?
Ni lazima Rais aambiwe ukweli na bayana kuwa awe mvumilivu, yaan awe na kifua kipana cha kupokea au kusikia jambo na mengine ayanyamazie, si kila kitu ni cha kusema sema hadharani, pia, Rais aambiwe, kabla ya kusema jambo lazima apime athari zake kwa jamii au nchi.
Mwisho: Nawaomba Ndugu zangu watanzania, Tuendelee kuwa wamoja, tupendane na tuendelee na utamaduni wetu ambao umekuwepo tangu Enzi na Enzi, huyu ni Rais tu, kesho hayupo madarakani, kwa hiyo ni lazima tujitambue, mimi sioni tofauti kati ya CCM na Chadema au CUF kwa muktadha wa WANACHAMA, maana wote tu watanzania, tofauti ni mitizamo tu na Imani.
Nawapenda sana Watanzania.