Rais Magufuli pitia upya Sera na mishahara sekta ya madini itanufaisha taifa

Nsubhi

Senior Member
Jan 27, 2015
159
51
Wakati kikao cha raisi na wadau wa madini kikiendelea. Napenda kumpongeza raii kwa juhudi anazozifanya ili kuona Tanzania ya viwanda, lakini kuna watendaji wake wanamwangusa aidha kwa makusudi au kwa kutojua wanachokifanya.

Nimewahi kusikia viongozi wakisema, eti wafanyakazi wa sector binafsi ya madini wakilipwa mshahara mkubwa watakua walevi, wengine wakasema itasababisha wafanyakazi wa serikali kuacha kazi na kukimbilia migodini nk.

Kuna maswali ya kujiuliza, hivi migodini nafasi za kazi hazihesabiki? Au wanaruhusu walevi kuingia kazini wamelewa? Majibu ni hapana. Viongozi wenye mawazo kama hayo niliyo yataja hapo juu ni wabinafsi na wala rushwa wazuri tu. Ndiyo maana hawataki taifalao lineeneke na wawekezaji.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba serikali ingeweza kukusanya mapato makubwa sana zaidi ya sasa kutokana tu PAY. Kama serikali ingefanya yafuatayo:-
1.Kupandisha kima cha chini kwenye sector ya madini angarau kikawa 2,500,000Tshs. Serikali ingekusanya kodi kubwa sana kwa kila mtanzania anaefanya kazi mgodini. Na ndiyo maana wafanyakazi wanapoona uzalishaji ni mkubwa, wakiomba kuongezewa mshahara, utasikia mgodi mnasema oooh kwanza tulisha vuka kima cha chini. Na wanaenda mbali zaidi kwamba eti sera ndivyo inavyowaelekeza.
2. Kila mfanyakazi anaefanya kazi mgodini angepata TIN ingejulikana kila mtanzania anaefanya kazi mgodini anachangia kiasi gani, tofauti na sasa inaonekana migodi ndiyo inayochangia hata kile anachokatwa mfanyakazi PAY, kwa sababu tu PAYya mfanyakazi inapitia kwenye TIN ya mgodi. Hivyo ongefanyika hivi hata mwekezaji angejulikana analipa kiasi gani nasiyo kujificha kwa wafanyakazi. Utasikia ACACIA katipa kodi 36Billion kumbe 30Billion ni PAY ya wafanyakazi yeye kalipa kiduchu.

Ukifata haya mheshimiwa raisi nakuhakikishia tutafika mbali. Ushawahi kujiuliza kwenye nchi wanazotoka hawa wawekezaji wakubwa wa madini kwanini hawalipi mishahara kama hii ya kwetu? Kwamba watanzania hawajui kutumia hela?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu mishahara haichotwi tu kwenye makampuni,kuna vigezo vinatumika kupanga mshahara,
Uwezi kumpangia mwajiri alipe kiwango gani!
Kama mapato ni makubwa,unaweza kulipwa hata 12M kwa mwezi,ni kitu cha kawaida,lakini kuimbia serikali iweke fixed amount kwa sekta Fulani,sio haki kwa wenye makampuni.
Sekta ya madini inalipa vzr sana,lakini hata sekta ya mawasiliano,kuna watu wanavuta 12M kwa mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii migodi karibia yote inamilikiwa na wageni. Sasa kama watu wa nyumbani mwako(civil servant) kima chao cha chini ni 300,000 Tshs. itawezekana vipi ukawa na uchungu na watu wa nyumba ya jirani?
Serikali hii ina roho mbaya ya kibinafsi.
Mtu analipwa Millions 15 na hupewa stahiki zingine kama Malazi, Chakula, Usafiri n.k bure, huku anamlipa mwenzake 500,000 Tshs au 300,000 Tshs huku anamwambia jitegemee kuanzia usafiri, chakula, malazi, ulinzi, kama una watoto shauri yako .
Kama lengo kodi tu na si maslahi ya wananchi waongeze ila kiukweli ubinafsi umeishika ngozi nyeusi ,hakuna anayejali maslahi ya mwenzake.
Nimewahi kufanya kazi mgodi wa Bulyanhulu nikaacha within 5 months.
 
Back
Top Bottom