VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kila ugonjwa una tiba au kinga au vyote. Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa,Dr. J. P. J. Magufuli,tafadhali niwie radhi nikushauri kwa mara ya mwisho. Shaurika.
Mimi sikuwahi kuwa Rais. Mwenzangu ndiwe Rais. Lakini,mimi nimekuwa mwanasiasa mwandamizi na hata mtumishi mwandamizi wa idara nyetinyeti Serikalini kuliko wewe. Najua jambo moja kubwa:mgawanyo wa majukumu na kuwa ukomo wa jukumu fulani
Kiserikali,kuna mambo ya Rais;ya Makamu wa Rais;ya Waziri Mkuu;ya Waziri na kadhalika na kadhalika. Kila kiongozi Serikalini ana majukumu na mipaka yake. Ndiyo kusema,si kila jambo lamhusu Rais. Si kila jambo halimhusu Rais. Si mambo yote yanayomhusu Rais kuyashughulikia.
Mhe. Rais,wewe kuandikwaandikwa kwenye media kila uchao si jambo jema sana. Kuandikwa kwako kwa kila litokealo Serikalini ni mchoro wa kutia kihoro. Mchoro huoneshao kuwa unafanya au kusemea kila jambo-hata yale ya Mawaziri,Makatibu Wakuu wa Wizara na kuendelea. Hoja ya jeshi la mtu mmoja huanzia hapo. Haivutii
Mhe. Rais,nakushauri uwaruhusu wasaidizi na wateule wako wafanye kazi zao ulizowaamini wazifanye. Wakizifanya zao,kazi zako zitapungua na kuonekana vyema. Yapo mambo ya kutendwa au kuzungumziwa na wasaidizi au wateule wako. Hata Wasemaji wa Wizara wangetosha na kutisha!
Ushauri wangu unalenga kukupunguzia kazi. Tafadhali epuka kuona kila jambo Serikalini ni lako. Ikifika hapo,yote utayatenda wewe. Wengine watatumbua mishahara ya bure. Tena,utaandikwa na kusemwa sana. Utafurahi na kukereka sana. Utaona na kusikia sana. Utafanya kazi sana. Utachoka sana. Utasema sana. Utatutisha sana!
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam