Rais Magufuli nisamehe,nakushauri kwa mara ya mwisho. Tafadhali shaurika!

Kuongea ongea sana sio ujanja kabisa.. Anapaswa kuelezwa na kuelewa madhara yake ki inteligensia
 
Kila ugonjwa una tiba au kinga au vyote. Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa,Dr. J. P. J. Magufuli,tafadhali niwie radhi nikushauri kwa mara ya mwisho. Shaurika.

Mimi sikuwahi kuwa Rais. Mwenzangu ndiwe Rais. Lakini,mimi nimekuwa mwanasiasa mwandamizi na hata mtumishi mwandamizi wa idara nyetinyeti Serikalini kuliko wewe. Najua jambo moja kubwa:mgawanyo wa majukumu na kuwa ukomo wa jukumu fulani

Kiserikali,kuna mambo ya Rais;ya Makamu wa Rais;ya Waziri Mkuu;ya Waziri na kadhalika na kadhalika. Kila kiongozi Serikalini ana majukumu na mipaka yake. Ndiyo kusema,si kila jambo lamhusu Rais. Si kila jambo halimhusu Rais. Si mambo yote yanayomhusu Rais kuyashughulikia.

Mhe. Rais,wewe kuandikwaandikwa kwenye media kila uchao si jambo jema sana. Kuandikwa kwako kwa kila litokealo Serikalini ni mchoro wa kutia kihoro. Mchoro huoneshao kuwa unafanya au kusemea kila jambo-hata yale ya Mawaziri,Makatibu Wakuu wa Wizara na kuendelea. Hoja ya jeshi la mtu mmoja huanzia hapo. Haivutii

Mhe. Rais,nakushauri uwaruhusu wasaidizi na wateule wako wafanye kazi zao ulizowaamini wazifanye. Wakizifanya zao,kazi zako zitapungua na kuonekana vyema. Yapo mambo ya kutendwa au kuzungumziwa na wasaidizi au wateule wako. Hata Wasemaji wa Wizara wangetosha na kutisha!

Ushauri wangu unalenga kukupunguzia kazi. Tafadhali epuka kuona kila jambo Serikalini ni lako. Ikifika hapo,yote utayatenda wewe. Wengine watatumbua mishahara ya bure. Tena,utaandikwa na kusemwa sana. Utafurahi na kukereka sana. Utaona na kusikia sana. Utafanya kazi sana. Utachoka sana. Utasema sana. Utatutisha sana!

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Tunajua mmechukia Rais kuamuru Nay wa mitego kuachiwa maana mlitaka kulifanya la kimanufaa kwenu......
hahahah Rais kawapiga chenga sana
 
Kamsahihishe Mbowe kwanza!

Nikikumbuka mwaka jana miezi kama hii wakati awamu hii bado single ya majipu inaheat ulikuwa unashambulia kwa kumwaga sifa kibao. Lakini siku hizi naona mzee umechuja huna jipya zaidi ya kuzuia mashambulizi tena kwa jazba. Umegeuka huna hoja mpya zaidi ya cdcm, Mbowe na Lowassa. Ulitaraji mwaka huu ungekuwa umeota mbawa, lakini badala yake mmegeuka kupangia nini vyombo vya habari vitangaze tena kwa vitisho. Sidhani kama mnatoboa safari hii.
 
Sasa we Tupatupa unadhani wataweza vipi hao wateule wake kufanya kazi iwapo mtu akitimiza tu wajibu wake anatimuliwa kazi? Watakaofanya kazi ni wale watakaopokea maelekezo kama Mwakyembe leo.hata ningekuwa ni mimi nisingejihangaisha kwa lolote.
 
Moja ya sababu kwanini watu siku hizi wanakuwa wanamtukana Rais hovyo hovyo.

Maana wameshamzoea vya kutosha coz president mwenyewe amekuwa pia msemaji wa issues ambazo zingetakiwa kusemwa na makatibu wa wizara. Too bad..

Rais angepaswa kuwa na ule uraibu wetu wa kiafrika kwa baba mwenye nyumba. Anajenga ukuta wa mazoea ya kipuuzi kati yake na family lakini anakuwa kwa mlango wa nyuma anayajua na kuyapanga yote yanayohusu family kwa weledi mkubwa.

Magu alipoteza hiyo sifa tangu mwanzo na ndo kinachomgharimu kwa sasa. Hata akinguruma sahiv hawajali tena, wameshamzoea..
Hujakosea mkuu
 
Wewe ni nani Nchi hii hadi utake ushahuri wako Raisi wa Nchi auchukuwe? Kamshauri Mbowe jinsi ya kuishi na Wema na Mamake, kama ukipenda!
hii post ni kwa ajili ya wenye akili zao tuu.sio kwa ajili ya watu waliotupa akili zap lumumba
 
Kuna watu wana hulka ya kupenda kusifiwa kwa ubaya. They will reap what they sow. 2020 not so far.
Kila nikiona comment ya kujifariji ya design hii roho inaniuma sana, kama uchaguzi ungekuwa wa huru na haki tusingefikia hapa, namba zitasomeka kwa mda mrefu sana. Unadhani guts za kufanya haya madudu wanapata wapi? binafsi sitafanya ujinga tena wa kupanga msitari eti napiga kura. nonsense.
 
Wewe ni nani Nchi hii hadi utake ushahuri wako Raisi wa Nchi auchukuwe? Kamshauri Mbowe jinsi ya kuishi na Wema na Mamake, kama ukipenda!

BASHITE bana huwezi kujibu hoja kwa hoja????? Mtanzania yeyote yule ana haki ya kumshauri kiongozi wakati wowote ule hiyo ni mojawapo ya haki yake.....matusi na bastola ya nini???
 
Kila ugonjwa una tiba au kinga au vyote. Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa,Dr. J. P. J. Magufuli,tafadhali niwie radhi nikushauri kwa mara ya mwisho. Shaurika.

Mimi sikuwahi kuwa Rais. Mwenzangu ndiwe Rais. Lakini,mimi nimekuwa mwanasiasa mwandamizi na hata mtumishi mwandamizi wa idara nyetinyeti Serikalini kuliko wewe. Najua jambo moja kubwa:mgawanyo wa majukumu na kuwa ukomo wa jukumu fulani

Kiserikali,kuna mambo ya Rais;ya Makamu wa Rais;ya Waziri Mkuu;ya Waziri na kadhalika na kadhalika. Kila kiongozi Serikalini ana majukumu na mipaka yake. Ndiyo kusema,si kila jambo lamhusu Rais. Si kila jambo halimhusu Rais. Si mambo yote yanayomhusu Rais kuyashughulikia.

Mhe. Rais,wewe kuandikwaandikwa kwenye media kila uchao si jambo jema sana. Kuandikwa kwako kwa kila litokealo Serikalini ni mchoro wa kutia kihoro. Mchoro huoneshao kuwa unafanya au kusemea kila jambo-hata yale ya Mawaziri,Makatibu Wakuu wa Wizara na kuendelea. Hoja ya jeshi la mtu mmoja huanzia hapo. Haivutii

Mhe. Rais,nakushauri uwaruhusu wasaidizi na wateule wako wafanye kazi zao ulizowaamini wazifanye. Wakizifanya zao,kazi zako zitapungua na kuonekana vyema. Yapo mambo ya kutendwa au kuzungumziwa na wasaidizi au wateule wako. Hata Wasemaji wa Wizara wangetosha na kutisha!

Ushauri wangu unalenga kukupunguzia kazi. Tafadhali epuka kuona kila jambo Serikalini ni lako. Ikifika hapo,yote utayatenda wewe. Wengine watatumbua mishahara ya bure. Tena,utaandikwa na kusemwa sana. Utafurahi na kukereka sana. Utaona na kusikia sana. Utafanya kazi sana. Utachoka sana. Utasema sana. Utatutisha sana!

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Wewe mbeba ngada za mboe tangu lini ukawa lini ukawa mshauri wa rais wetu?
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom