Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
BAADA YA SIKU 100 ZA UTAWALA WA Mh. MAGUFULI NIMEJIFUNZA YAFUATAYO
1. Hatutotoka hapa Tulipo Kwenda Huko tupatakako kwa kulalamika Pasipo Kuwa Wawajibikaji and taking actions immediately if anything goes wrong. Serikali ipo kusimamia na wananchi ndio wawajibikaji. Usisubiri Serikali ikufanyie jambo bali ifanyie serikali jambo.
2. Tusimvizie ama kumtegea Mh. Magufuli ashindwe ili tumzomee ama kumsonta vidole. (Tumsapoti atende vyema maana mafanikio yake ni yetu sote tuache siasa kwenye maendeleo ya taifa letu). Ni sumu sana kuchanganya siasa na maendeleo. Ni muda wa kutoa sapoti kwa serikali yetu na kuwa wazalendo kwa taifa letu.
3. CCM ni ile ile na kwa mwendo huu kubadilika si leo wala kesho hivyo tusiwe na imani nayo sana. (Muhimu hapa ni kumsapoti huyu Rais na kumueleza mambo mema kadha wa kadha mfano ni muhimu ajue nchi hii ina wazee wengi wenye busara tofauti tofauti sio lazima awe akizungumza na wale wa Dar-Es-Salaam pekee ilihali huku mikoani kumejaa wazee wenye maono tofauti na hao waswahili wawaza kahawa wa hapo Dar ambao asilimia kubwa ni Wazaramo, Wangindo, Wamakonde na Wakwere). Azunguke Tanzania nzima kupata maoni sio ya wazee tu hata ya vijana pia ni muhimu. Kwani vijana ndio nguzo ya taifa.
4. Tanzania itasonga mbele endepo tutanena na kutenda. (Hili ni la muhimu sana katika ustawi wa Taifa letu, ni lazima maneno yalingane na vitendo. Endapo tutakuwa watu wa kuongea tu basi tutabaki kuwa wale wale miaka nenda miaka rudi.). Tuache poroja na majungu. Na pia tupende ukweli na kufanyia kazi mapungufu ili taifa lisonge sio kubwabwaja.
5. Tuwe Wazalendo Wa Nchi Yetu. (Sikatai Lazima tuwe na Wivu wa Maendeleo na tukubali kuiga kwa wenzetu lakini huku tukitambua Tanzania ni yetu, Tupie unamba one na Tuipende Daima). Tushabikie vilivyo vyetu na kuvienzi daima.
Katika hili La Uzalendo Nadhani ni lazima kama taifa tujibadilishe na ikiwezekana tuwe na slogan nyingi za Kizalendo
Ninachokiamini mimi Mla Rushwa sio Mzalendo let's fight corruption, Rushwa ni Adui Wa Haki, Tuipige vita kwa nguvu zetu zote
SEMA;
Mimi Ni Tanzania Na Tanzania Ni Mimi,
Ni ya Wanangu na Wajukuu Zangu,
Ni yangu na ya kwetu sote,
Wale ni watanzania, Mimi ni Mtanzania hivyo Sote ni Ndugu: Pamoja tusonge mbele.