KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Toka alipokuwa waziri katika wizara tofauti, Rais Magufuli alikuwa mtu wa kasi, viwango na ubora. Aliweza kumudu majukumu yake katika hali ya kiwango cha hali ya juu na utendaji kazi wake ulikuwa ni wa kasi na ubora. Hasa alipokuwa waziri wa ujenzi, Rais Magufuli atakumbukwa kusimamia ujenzi hasa wa barabara na madaraja katika kasi, viwango na ubora unaotakiwa. Hakika matokeo tuliyaona, nchi ilitapakaa barabara na madaraja ya kutosha.
Usimamizi huo mzuri wa shughuli za ujenzi katika ubora na kasi inayotakiwa, kwa kiwango kikubwa imeleta kasi kubwa katika maendeleo. Kusema kwamba Rais Magufuli ni mzuri katika kuleta maendeleo kwa kasi ina maana kwamba matokeo ambayo pengine tungeyapata kwa miaka 10-15 ijayo tumefanikiwa kuyaona na kuyapata ndani ya miaka 4 ya uongozi wake. Hii ni kasi kubwa sana katika ujenzi wa taifa letu. Kwa kasi hii, ndoto ya kuwa na uchumi wa kati inawezekana.
Katika kupambana na umasikini, Rais Magufuli kaiva vizuri sana. Moja ya njia za kumkwamua mwananchi dhidi ya umasikini ni Kazi na Rais Magufuli akaja na kauli ya ‘ Hapa kazi tu’ ikiwa na lengo la kutuhamasisha na kutuelekeza umuhimu wa kazi. Katika Uongozi wa Magufuli watu wameshirikishwa na kushiriki vya kutosha katika shughuli za kimaendeleo kama njia ya kuwafikia watu na kuwapatia ujuzi wa kuleta maendeleo na kujikwamua na umasikini. Mabadiliko chanya makubwa yameonekana baada ya watu kuhamasika katika ujasiriamali kama njia ya kuondoa umasikini. Hii ni mifano ya kuonesha ushiriki wa Rais Magufuli katika kupigana na Umasikini ulivyo mkubwa sana.
swali langu ni: je, ni nani kutoka upinzani ana rekodi nzuri kama hii? Kama hamna mtu mwenye rekodi kama hii, Je watanzania watakuwa wana uhakika gani kuwa wakichagua upinzani wataweza kupata maendeleo ya kasi na kupungua kwa umasikini? Mwandishi mmoja aliwahi kusema kuwa’ kosa ambalo utakuja kujuta ni kufanya majaribio ya uongozi’. Kwa maneno hayo ya huyo mwandishi ni ujumbe unaotuasa umakini wa kuchagua na tusimchague mtu kujaribu kama ataweza ama laa.