Rais Magufuli ni Dereva Mahiri lakini Gari ni Bovu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
WATANZANIA tulitaka mabadiliko. Hatujayapata. Lakini kuna watu, kwa kutazama staili ya kazi ya Rais John Magufuli, wanadhani tumeyapata.

Maana yake ni kwamba wapo Watanzania wengi ambao walitamani mabadiliko, lakini hawakujua aina ya mabadiliko,

Rais Magufuli naye alikuwa mjanja tangu wakati wa kampeni. Akisaidiwa na wanamkakati, akina Januari Makamba, walipogundua kuwa Watanzania wanataka mabadiliko, na kwamba wameamua kuyasaka kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), walimfunda na kumfunza siasa za kuiga, naye akaanza kuimba mabadiliko.

Ilifika mahali, Magufuli akaghushi hata kirefu cha M4C, Movement for Change, ambayo CHADEMA waliiita vuguvugu la mabadiliko. Akina Januari walimfundisha aliite Magufuli for Change!

Katika hotuba zake, Magufuli alitoa kauli zenye takwimu, maelezo, hisia, sababu na mwelekeo wa UKAWA. Magufuli akaacha lugha ya CCM, Chama Cha Mapinduzi. Akazungumzia lugha ya UKAWA.

Kwa watu wanaokwenda kwa upepo na wepesi wa kupigwa propaganda, ilikuwa rahisi kuwachota na kuwateka.

ALifanikiwa kuteka wengi. Si kwa kauli tu, bali pia kwa sababu nyingine ambazo zinaendelea kumsaidia kushangiliwa hata anapokosea.

Magufuli hakuwa anaamini katika UKAWA. Lakini alizungumza lugha ya UKAWA. Kwa sababu hiyo, akafanikiwa kupata wafuasi na watetezi kirahisi.

Jaji Joseph Warioba, kwa mfano, alimfanyia kampeni kwa sababu alimtazama kwa jicho la uadilifu. Alidhani Magufuli ni mwadilifu, na kwamba kwa uadilifu huo angeweza kuleta mabadiliko yaliyotakiwa.

Humphrey Polepole alimtazama Magufuli kwa jicho lile lile, lakini hasa kwa kuwa alikuwa mgombea wa chama chake. Pamoja na hamu yake ya katiba mpya, na licha ya kutambua kuwa Magufuli akiwam gombea wa CCM asingeweza kutetea katiba mpya waliyotaka akina Warioba na Polepole, walimpatia ushirikiano wa kutosha awe rais kwa vile tu ni mwana CCM mwenzao.

Bahati mbaya, kwa “wazalendo, wapiganaji na mashujaa” hawa wa katiba mpya, lilipofika suala la urais, CCM ikawa bora kuliko Tanzania.

Kuna jambo jingine lilichangia kuwapofusha – wao na wengine wengi waliomshabikia Magufuli na kutafuta njia zote za kuharibia UKAWA.

Walijielekeza kwa mgombea binafsi. Walitazama mgombea wao, wakamtazama na mweingine wasiyemtaka binafsi.

Kwao, chama kama taasisi hakikuwa na nafasi. Katiba ya nchi haikuwa ajenda tena. Mfumo haukuwa muhimu, bali mtu. Ghafla, mabadiliko waliyokuwa wakipigania yakabadilika maana, wakaanza kupigana kutafuta kura za mtu wao badala ya nchi yao.

Hawakuelewa tena kwanini UKAWA walisema huko nyuma, na wakasisitiza mara kwa mara, kwamba kwa jinsi tunavyotaka mabadiliko, na kwa jinsi tulivyochoka kuwa chini ya CCM, hata likiwekwa jiwe, tutalipigia kura liwe rais.

Lakini wana UKAWA walio wengi na wafuasi wao, walikuwa wameelewa fika ujumbe huu. Ndiyo maana gia zilipobadilishwa angani, wagombea wakapishana mlangoni, UKAWA haukutetereka, bali uliimarika zaidi.

Licha ya serikali kuingilia kati kutumia mashushushu wake, na kupokonya vigogo wawili wakuu katika UKAWA – Dk. Willibrord Slaa na Profesa Ibrahim Lipumba – UKAWA ulibaki imara.

Ndiyo maana hata zilipopigwa propaganda za CCM kwamba UKAWA “wameweka fisadi agombee urais,” huku wakijaribu kukumbusha kuwa UKAWA ndio walimtuhumu kuwa fisadi tangu 2007 kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam, wana UKAWA walibaki wamoja, na baadhi walihoji:

“Kama Mwembeyanga tulituhumu vigogo 11 ndani CCM, na miongoni mwao ameondoka mmoja akajiunga nasi, ni nani amewasafisha wengine kiasi cha kumuona huyu mmoja aliyeondoka ndiye fisadi kuliko 10 waliobaki?”

Kwa sababu za ushabiki wa mtu badala ya mfumo, hata baadhi ya watu wenye heshima waliowahi kunieleza kuwa wanatamani tuondokane na mfumo wa udikteta wa chama kimoja, walisahau haja ya kuunda mfumo mpya, wakawa wanatafuta rais mpya.

Nakumbuka mmoja wao aliwahi kunieleza kuwa CHADEMA inapaswa ibadilishe mkakati, iachane na hoja ya ufisadi majukwaani, kwani imezoeleka na haigusi tena wananchi na haipandishi tena chati ya CHADEMA.

Kumbe alikuwa rafiki binafsi wa Dk. Slaa. Mwenzake alipoondoa kwa hasira, naye akajiunga na Magufuli kwa hasira. Nasikia sasa ni mmoja wa washauri wake anayemfunza jinsi ya kucheza na sehemu ya sera za UKAWA kunasa mashabiki.

Tafsiri rahisi ni kwamba hata huyu alighubikwa na hisia, akaondoka kwenye mstari wa kupigania ujenzi wa mfumo mpya, akasahau katiba mpya, akaganda kwa rais mpya.

Nayaona haya katika utendaji wa Rais Magufuli. Nasikia wanaommwagia sifa hata katika makosa.

Nasikia baadhi ya wananchi wakisema hii ndiyo Tanzania waliyoitaka, kwa vile tu ameonesha ukali dhidi ya wabadhirifu wazembe na wezi.

Kiukweli, ukali wa rais ni jambo zuri. Lakini ukali wake bila mfumo imara wa kuhimiza, kulinda na kudhibiti ukali huo, hauwezi kuleta mabadiliko tunayotaka.

Baadhi yetu tunaamini kwamba rais anafanya kazi nzuri kudhibiti wezi, lakini hatumii mfumo kuwadhibiti. Kwa maana hiyo, anapigana vita itakayomchosha muda mfupi ujao.

Tunaelewa, na tulishasisitiza huko nyuma, kwamba kwa mfumo huu wa CCM, na bila katiba mpya, hata akishushwa malaika Gabriel akakabidhiwa serikali, atafanya kazi kwa mtindo wa mbio za sakafuni.

Kwa wale ambao wanaona, kwa nia njema kabisa, kwamba Magufuli atafanikiwa kubadili nchi hii akiwa ndani ya CCM, na katikamfumo huu, watapata tabu sana kuelewana miaka miwili au mitatu baadaye, utakapoanza kudhihirika ukweli huu tunaosema na kubezwa wakati huu.

Lakini acha Magufuli awe kielelezo. Acha awaonesha kuwa rais mkali katika mfumo uliochoka ni sawa na dereva mahiri anayeendesha gari bovu.
 
Unamkubali Magu na serikali yake.... Tatizo uchama ulio nao ndio umekutia upofu
 
Binafsi naona hili Gari ni jipya isipkuwa lilikosa dereva anaejua njia na anaejua kuendesha
na dereva huyu wa sasa hajui njia ila anaendesha kwa kasi na kwa mbwembwe....

tunaomsisitiza uliza njia kwanza tunaonekana tunataka kuchelewesha safari
sasa safari ya kwenda Mwanza lakini gari inaelekea Mtwara....
yetu macho
 
Muda si mrefu itabidi,mbowe atatowa tamko la chama kumuunga mkono Raisi...hamna jinsi,ukweli haupendi kupuuzwa!
 
''ALifanikiwa kuteka wengi. Si kwa kauli tu, bali pia kwa sababu nyingine ambazo zinaendelea kumsaidia kushangiliwa hata anapokosea.''

aliwateka wengi maana yake ni kwmba watu wamempima vya kutosha na kuamini anaweza leta mabadiliko kwa hyo wewe endelea kuzungusha mikono mkuu lakini sie tunapiga kazi tu
 
Na Nyie Mkatuletea Mgombea asietaka kutamka maneno haya " Ufisadi" hata kwa bahati mbaya na Zuhra Yunus alipojaribu kutumia Mbinu za kiuandishi atamke Maneno hayo aliishia kusema anaonewa!
Siasa ni kama Mpira ukitumia nguvu nyingi ku defend wenzio unawapa fursa kushambulia!. Mbowe alichagua Beki (Lowassa) akamtosa Forward (Slaa), Ccm ikatumia Striker wake vizuri kushambulia!
 
lakini gari lake litafika kwa kuwa atalifanyia overall lote na kuweka spea mpya hata kupiga rangi na itakuwa poa
 
Back
Top Bottom