Rais Magufuli na waziri Lukuvi - Natoa ushauri mzuri kwa ujenzi mbovu Dar

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
Ninaona hapa ujumbe unaweza fika na ukasaidia. Kwa mawazo yangu mepesi, Serikali nilazima ianzishe njia mbadala kulibadili jiji La Dar.

Mtu anayetaka eneo la Kuwekeza biashara yenye Maslahi kwa Taifa, Wananchi waliojenga kiholela eneo ambalo Lingefaa kwa uwekezaji, Kuamua kuwaita wananchi husika na kuwapa taarifa ya kubadili mfumo wa makazi yao kwa KUJENGA MAGOROFA MAKUBWA NA MAREFU LABDA KAMA YA MICHENZANI ZNZ.

Na wananchi wa eneo husika bila kuwaathiri kwa kuwahamisha, Gorofa zenyewe baadhi ya wananchi wakubali kutoka maeneo yao kwa muda mapema kuruhusu ubomoaji na ujenzi wa Gorofa ambalo linaweza kuwa accomodate Labda zaidi ya nyumba 50 zipande gorofani na kuachia maeneo yao kuwa wazi na kuendeleza mfumo kwa kuwapandisha watu magorofani ambapo utaweza tengeneza maeneo makubwa sana ya wazi na huduma za kijamii kupatikana kirahisi na labda Ujenzi wa majumba haya wawekezaji wengine wenye maslahi kwa taifa wakaamua kusimamisha magorofa hayo ambapo ni mjadala wenye kuhitaji fikra zaidi ya mimi nisiyejitambua.

I do think, We can change our City by trying to invest in this ideas,
 
Last edited by a moderator:
Ninakubaliana na wewe kabisa na ukizingatia hizo sehemu ambazo zinavunjwa Nyumba kama kutatokea Tajiri was kujenga ayo magorofa naamini hayatokua ba athari yoyote ya mafuriko ambayo yatatokea kwakua miundo mbinu itaboreshwa vizuri sana.

Haitokua na maana kwa mfano pale jangwani uvunje halafu pabakie mito ambayo itaweka maji kwa muda mrefu na kubakia mammbu wengi sana na wengine kufanya ni sehemu zao za kujificha kwa uhalifu.

Tunavunja lakn je ni nini kitafuata kijulikane, kuna baadhi ya sehemu nimeona Kariakoo zimepigwa x je baada ya kuvunjwa ilo eneo litaachwa kwa ajili ya wamachinga kuendeleza biashara zao zilizozagaa kila sehemu maeneo ya Kariakoo?
 
Ushauri huu miji mikubwa duniani wanaokuja mjini wanakuta magorofa wanapangisha kwa kilipa mapato. Tanzania ina sehemu unaingia Chumba cha kulala pembeni yake ni choo cha jirani na Nyuma yake Jiko la mwingine. Serikali lazima iangalie mbali. Wapandishwe watu magorofani maeneo mengi ya wazi yazalishwe
 
Back
Top Bottom