Habari za jioni wana jamvi.
Ndugu zangu nianze kwa kusema kuwa, Tanzania imekuwa ikiongonzwa na Viongozi (Rais) kutoka Chama Cha Mapinduzi tangu tumekuwa Jamhuri. Kwa vipindi vyote hivyo tumekuwa na awamu tano za Marais waliowahi kupewa dhamana ya kuliongoza Taifa hili. Tulikuwa naye Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere, awamu ya Pili Mh. Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, awamu ya Tatu Mh. Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa, awamu ya Nne Mh. Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na sasa awamu ya tano ambayo bado ipo madarakani Mh. Rais, Dr. John Joseph Pombe Magufuli ndiye anayo dhamana ya watanzania kuwapeleka wanakotaka.
Baada ya utangulizi huo, niseme kuwa, Marais wote hao walikuwa na dhamira na nia ya kuipeleka Tanzania mbele, kutoka kwenye wimbi la Umaskini, njaa, magonjwa, elimu na kulifanya jina la Nchi Tanzania kukuwa na kuwa kubwa Kimataifa. Tukiri kuwa pamoja na changamoto za kila awamu lakini hakuna hata awamu moja ambayo hautaona viashiria vya kujenga Taifa na Nchi bora kabisa.
Tukiwaacha marais wa Awamu Nne zilizopita, Mh. Rais Magufuli anayo ndoto kubwa kuhusu Tanzania. Tukubali kuwa binadamu tunazidiana kufikiri, kupambanua mambo, vipaumbele, uwezo wa kuchukuwa hatua, na ubora wa utendaji kazi. Mh. Rais Magufuli anao uwezo mkubwa sana wa yote hayo. Mfano mdogo kwa ngazi ya familia, ukiwa na baba asiye na maamuzi na asiye na ndoto ya namna gani familia iwe basi familia itakuwa vile itakavyokuwa, ila si maanishi lazima iwe ya hovyo isipokuwa hatma ya familia itategemea mazingira.
Tanzania ya leo ambayo bado tupo na Awamu ya Tano kwa miaka Mitatu hii, Mh. Rais ameonyesha kuwa, ni kiongozi mwenye maono hai na anataka sisi tuamue hatma ya Tanzania yetu.
Mimi najikita sana kuzungumzia fikra, kwa maana ya mawazo. Maana tukianza kujikita kwenye yapi ya maono amefanya Mh. Rais tutachukuwa muda mwingi kuyaongelea na ni mengi.
Moja ya viashiria vya kuwa na uwezo mkubwa wa maono,
i) Mh. Rais anajipanga kuijengea Nchi uwezo kwa kufanya maamuzo yake yenyewe ambayo yanatija kwa Taifa, uwezo wa kuwa na Umeme imara ili kusudi kuliwezesha Taifa kuwa na uwezo wa kuwekeza kwenye Viwanda kwani vinahitaji umeme mkubwa na madhuti.
ii) Mh. Rais amejikita kuiona Tanzania ya baadaye ambayo itakuwa na vijana wengi waliokuwa na uwezo, ufahamu na wanaoijuwa dunia kwa kuhakikisha elimu ya msingi kwa Tanzania ambayo inaishia kidato cha Nne ni bure, kwani hata kama tukiweza kuwa na viwanda ambavyo vitaendeshwa na wageni hapo bado haiwezi kuleta tija kwa Wananchi.
iii) Mh. Rais ameona umuhimu wa Miundo mbinu kama Reli katika kuimarisha uwekezaji wa Viwanda Nchini,
iv) Mh Rais amewajengea watumishi wa umma kote Nchi nzima dhana ya kutowanyanyasa wananchi wanaotaka haki na huduma katika ofisi hizo. Tumeshuhudia akiwaonya na kuwaelekeza mawaziri na viongozi wengine wa serikali kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri na kwa kuheshimiana.
v) Anapambana usiku na mchana kuhakikisha kuwa maeneo muhimu ya mapato yanaiingizia Serikali stahiki yake kwani kwa kufanya hivyo ndiyo tutaweza kupata Tanzania tunayoitaka.
Ikumbukwe mtangulizi wake Baba wa Taifa aliwahi kusema "Serikali ni lazima iwe na uwezo wa kujiendesha kwa kukusanya mapato yake yenyewe". Mh. Rais anaendelea kuwafanya Watanzania watambue kuwa wanao wajibu wa kuiendesha Nchi yao kwa kulipa Kodi. Tukubali kuwa katika awamu hizi za Urais Nchini, ufahamu mkubwa kuhusu ulipaji kodi na faida zake umekuwa zaida kwa awamu ya tano.
Watanzania tusiwe wajinga, tusimame pamoja na Rais, tumpe moyo kwani ni kati ya Watanzania ambao wanania njema na Taifa hili.9
Tukumbuke kila zama ina mapungufu yake na tutambue kuwa ukimpata ambaye anaonyesha muelekeo mzuri ni dhahiri mkishirikiana mtafanya vizuri zaidi. Tanzania yetu, rais wetu.
Najivunia kuwa mtanzania, najivunia kuwa na rais mwenye maono yenye tija kwa Taifa.
Itaendelea...........