Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Serikali imetangaza punguzo la kodi ya mapato (PAYE) la asilimia mbili i.e kutoka 11% ya sasa hadi 9% kwa income bracket ya TZS 170, 000 hadi TZS 360,000.
Kima cha chini cha mshahara wa serikali ni TZS 315,000 kwa mwezi. Chini ya kiwango hichi cha mshahara, punguzo la kodi ni TZS 2900 tu. Lakini kwenye uchambuzi wetu, tutatumia kipato cha tzs 265,000 ili kuendana na income bracket inayohusishwa na punguzo hili - yani Kipato kati ya TZS 1700,000 na TZS 360,000. Wastani wa bracket hii unatupa TZS 265,000.
Kabla ya punguzo hili, makato ya kodi yalikuwa ni (11%) ya mshahara wa mwezi ikimaanisha kwamba:
Mfanyakazi huyu wa kima cha chini alikuwa akikatwa kodi (TZS 265,000-170, 000)* 11% ambayo ilikuwa ni sawa na TZS 10,450 kwa Mwezi.
Baada ya punguzo hili, ambapo sasa makato ya kodi ni (9%), mfanyakazi huyu wa kima cha chini sasa atakatwa kodi (TZS 265,000 - 170,000)*9%, ambayo sasa itakuwa ni sawa na TZS 8,550.
Je, amepunguziwa mzigo wa kodi kwa kiasi gani (TZS)?
Jibu ni kwamba punguzo la TZS (10,450 - 8,550), ni sawa TZS 1,900.
Kwa maana nyingine, ahadi ya "mabadiliko" kupitia bajeti ya kwanza ya serikali ya awamu ya Tano kwa wafanyakazi wa kima cha chini linapokuja suala la punguzo la kodi ya mapato (PAYE), ni TZS 1,900.
Hapa tunaona kwamba punguzo husika la kodi halina 'impact' ya maana kwa watumishi waliolengwa na uamuzi huu. Maswali yanayofuata ni je:
1. Serikali imejipanga vipi Kumlinda mtumishi huyu dhidi ya mfumuko wa kodi (inflation)?
2. Je serikali imejipanga vipi Kumwongezea mtumishi huyu kipato chake katika bajeti hii ya "mabadililo" ili na yeye aweze kuboresha maisha yake na familia?
Tujaribu kuangalia haya Kwa undani.
Kwa mujibu wa idara ya takwimu ya taifa (NBS), mfumuko wa bei kwa kipindi cha Mwezi March 2015 hadi March 2016 ni wastani wa 5.4%. Kwa maana nyingine, gharama za maisha kwa mtanzania katika kipindi hiki ilipanda kwa wastani wa 5.4%.
Kwahiyo ili mwananchi huyu aweze kumudu maisha yale yale ya Machi 2015 (bila ya kujalisha ana maisha bora au duni kiasi gani), kipato/mshahara wake ulitakiwa uongezeke kwa 5.4% kufikia Machi 2016. Kwa maana nyingine, ili Mtumishi huyu aweze kumudu maisha yale yale duni aliyoishi mwaka 2015, ilitakiwa mshahara wake uongezeke kwa TZS 13,669 zaidi kwa kipindi husika 2016.
Muhimu:
Kwa ongezeko hili la TZS 13,669 katika mshahata wake haina maana kwamba uwezo wake kimaisha kwa 2016 utskuwa umeboreshwa. Badala yake ni kwamba uwezo wake kimaisha utakuwa angalau umerudishwa katika hali Ile Ile duni ya mwaka 2015, badala ya kuwa duni zaidi. Basi.
Je vipi suala la ongezeko la mshahara kukidhi maisha bora?
Ili kuelewa ni kwa kiasi gani Mtanzania huyu anaishi maisha duni, tunahitaji kuangalia mfumuko wa bei katika bidhaa moja moja badala ya wastani wa 5.4% kwa sababu takwimu hii ya wastani mara nyinyi inaficha uhalisia wa mambo hasa pale serikali inapokuwa na utamaduni wa kutoa kauli kwamba katika kipindi husika, mfumuko wa bei umedhibitiwa ndani ya tarakimu moja, kwahiyo uchumi upo imara, huku uhalisia wa mambo ukiwa kwamba mfumuko wa bei katika bidhaa moja moja muhimu kwa wananchi kama vile "chakula" ukibakia katika tarakimu mbili (double digits). Hii ni moja ya sababu kubwa kwanini wananchi wengi huwa hujiuliza - kulikoni serikali inasema imedhibiti mfumuko wa bei ndani ya tarakimu moja (single digit inflation), kwahiyo wananchi wasihofu, afya ya uchumi ni Mara lakini taarifa hizi hawazioni kila wanapoenda kununua bidhaa kama sukari, unga nk.
Kwa mujibu wa NBS, bidhaa za vyakula zinachukua 39% ya matumizi ya Mtanzania kila mwezi. Kwa maana hii, mfanyakazi wa kima cha chini (TZS 265,000) anatumia takribani TZS 103,350 kila Mwezi kwenye chakula tu. Katika kipindi cha March 2015 hadi March 2016, mfumuko wa bei za vyakula ulikuwa kama 9%. Hii ni Karibia Mara mbili ya wastani wa mfumuko wa bei kwa kipindi husika (5.4%), na ni Karibia na tarakimu mbili (double digits) ambayo hata kwa Serikali, sio "safe zone"linapokuja suala zima la gharama za maisha ya wananchi.
Kwahiyo ili Mwananchi huyu aweze kumudu bajeti ile Ile ya chakula ya mwaka uliotangulia (2015) kwa ajili yake na familia (tzs103,350) kwa Mwezi, kwa mfumuko huu wa bei ya vyakula (9%) kwa mwaka, inabidi katika kipindi husika cha mwaka 2016, kipato chake kukidhi mahitaji ya chakula inabidi kiongezeke kwa TZS 9,300 au zaidi.
Tukiendelea kujadili suala la kipato na maisha bora katika muktadha wa mfumuko wa bei:
Kwa mujibu wa idara ya takwimu ya taifa (NBS), huduma za Afya huchukua 2.9% ya matumizi ya Mtanzania. Kwa maana hii, kwa mfanyakazi wa kima cha chini, gharama zake za afya ni TZS 7,685 kwa Mwezi. Kwa mujibu wa NBS, katika kipindi husika (March 2015-2016), gharama za afya ziliongezeka kwa 6.2%, ikiwa ni zaidi ya wastani wa mfumuko wa bei ambao ulikiwa ni 5.4%. Hapa tunaona kwa urahisi kabisa kwamba kwa namna yoyote ile, kwa kipato hiki, mwananchi huyu hawawezi kupata huduma ya "afya bora."
Elimu:
Kwa mujibu wa NBS, wananchi hutumia 1.5% ya mapato Yao kwenye elimu. Kwa maana hii, gharama za elimu kwa mfanyakazi wa kima cha chini (tzs 265,000), ni TZS 3,975 kwa Mwezi, ambayo ni sawa na TZS 47,700 kwa mwaka. Je:
Ni elimu yenye "ubora gani" ambayo Mtanzania huyu anayepokea kima cha chini cha mshahara ataweza kuwapatia watoto wake? Kwa vyovyote vile, familia ya aina hii daima itaishi katika "vicious circle of poverty."
Katika kipindi husika, mfumuko wa bei katika huduma ya elimu ulikuwa ni 2.6%. Hiki ni kielelezo kwamba sehemu kubwa ya elimu inatolewa na serikali Kwa gharama ndogo sana kwa wananchi lakini pia elimu isiyotengewa bajeti ya kutosha, hivyo kuwa ni elimu isiyo "bora." Lakini kwa upande wa wazazi wanaojiweza zaidi kimaisha ambao wanasomesha watoto wao kwenye shule binafsi ambapo elimu ni bora zaidi, hii ni habari njema kwa sababu kwao, ongezeko la 2.6% kama gharama ya kusomesha watoto kati kipindi husika ni suala ambalo wengi wanamudu.
Je yepi zaidi tutayaona katika bajeti ya kwanza ya Mabadiliko?
Muda utatueleza.