Rais Magufuli na Museveni: EPA ni ukoloni mwingine

Rais Magufuli na Museveni: EPA ni ukoloni mwingine

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Rais Magufuli na Rais Museveni kwa nyakati tofauti wamesema EPA ni ukoloni unaoletwa katika nchi zetu na nchi za Ulaya kwa njia nyingine.

Hayo yamezungumzwa na Marais baada ya kusaini mikataba na makubaliano mbali mbali ya kiuchumi katika Ikulu Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa Rais Museveni yuko nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Rais Magufuli alisema, ‘’Sisi Tanzania tunaona EPA haina faida nani ukoloni mwingine ambao unaletwa’’.

Aliendelea kusema, ‘’huwezi ukazungumzia juu ya viwanda na wakati huo huo unashindana na watu wenye viwanda vikubwa vikubwa’’.

Rais Museveni alisema, ‘’Tatizo letu ni kutokuwa wamoja hata kwenye suala dogo kama hili la EPA. nimekuja Tanzania ili kuhakikisha tunakuwa pamoja kifikra na kimsimamo katika hili suala la EPA. Hili jambo sio juu ya EPA bali ni juu yetu sisi, lazima tuwe na msimamo mmoja’'.

Aliendelea kusema, ‘’Tatizo letu kama Waafrika tunachukua bima za majengo na magari lakini hatujaweza kuchukua bima zinazotuwezesha kutotawaliwa tena na kudharauliwa''.

VIDEO
​
 
Napenda tu kumtaarifu mh rais kuwa hvyo vitu vidogo vidogo anavosema mkandarasi anaweza akawa anachukua sio vidogo vidogo kama anavyodhani.
 
Ni kweli EPA haina manufaa kwa nhi za east africa.
Lakini wakenya wanajitoa ufahamu kutokana na ufisadi walionao,uchaguzi unakuja karibuni.Hawana jinsi ili waweze kusaidiwa na wazungu.
Rwanda-Kagame tunajua ni puppet leader wa westen world.Kwake yeye has nothing to loose maana bado uhumi wake ni mchanga sana.
Kwahio unakuta kila mtu anafanya maamuzi ya ustawi wa jamii za nchi zetu kwa maslahi yake na sio watu wake.
 
Kila nchi iamuwe kivyake kwanini waungane? Hatuna rais wa EAC kwanini tusumbuke kama Kenya inaona watakuwa na manufaa basi waongee na EU nikataba yao. Ni maoni yangu!
 
Vp jana uwanja wa taifa[emoji23]wale mliopanga warudishe kadi za ccm kumsapoti wema,mambo yalienda kama kawa?[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kila nchi iamuwe kivyake kwanini waungane? Hatuna rais wa EAC kwanini tusumbuke kama Kenya inaona watakuwa na manufaa basi waongee na EU nikataba yao. Ni maoni yangu!
Tupo katika umoja wa ushuru wa forodha wa pamoja ndio maana hii EPA inabidi iamuliwe kwa pamoja, vinginevyo kama baadhi ya nchi zitaruhusiwa basi tutakaribisha mgogoro mkubwa zaidi katika ushuru wa forodha.
 
Kenya wapo mbele Kiwanda hivyo wanaweza kufanya biashara na EPA pamoja na EAC kwa faida. Nchi zingine hazina cha kuuza Ulaya zaidi ya kuwa Soko la bidhaa za Viwanda wa Ulaya.
Hiyo itadidimiza ukuwaji wa Viwanda vya EAC labda kuacha Kenya. Hivyo Kama kweli nchi za EAC wanataka kukua Ki Viwanda basi mipango ya EPA isimame kwanza.
 
Big up sana museveni hapo Mimi ndipo ninapokukubali sana kwani unajenga hoja nzito na hupendi neo colonialism
 
Back
Top Bottom