Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,890
- 141,554
Tukisema ni dicteta watu wanabisha kwanini utolee nchi za kidicteta mfano asipoongelea Libya ataongelea Rwanda
Hiyo mifano kwa nini asiitoe kwa south Africa ambayo ilikumbatia ubaguzi mpaka wakasababisha maafa kama anavyofanya yeye ubaguzi?Huwa anaongelea na Iraq pia...
Hiyo mifano kwa nini asiitoe kwa south Africa ambayo ilikumbatia ubaguzi mpaka wakasababisha maafa kama anavyofanya yeye ubaguzi?
Sasa kama mtu Role model wake ni Kagame unategemea na yeye atakuwaje?
Moja wapo ya alama ya udiketa ni matamshi ya vitisho kama haya "mtu akikuchezea niambie, haitachukua hata dakika 5"
Huyu ilashaonekana toka anagombea kwake msamiati Demokrasia haupo na haamini kama upo.
Nani aliomba upuuzi uo labda waulize Mimi cha kwanza kwangu ni Uhuru,Kwa sababu mlikuwa mnadai mtu asiye 'dhaifu'. Shifting goal post haisaidii,pokeeni majibu ya maombi yenu, baptism of fire! Go Magufuli go!
Somo muhimu ambalo rais wetu Magufuli anashindwa kulielewa ni: hata mtu awe anapata mahitaji yote lakini kama hana uhuru na haki basi hataridhika, na akipata mwanya au sababu hata mbaya namna gani ya kurudisha uhuru na haki yake iliyopotea yupo tayari kuitumia bila kujali atapoteza zile huduma anazopata.Huwa anaongelea na Iraq pia...
Ni mara kadhaa sasa nimemsikia mtukufu rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, akiwa anazungumzia suala la amani, akiitolea mfano nchi ya Libya kipindi cha Gadafi.
Kwamba mambo huko Libya yalikuwa safi tu. Vijana waliokuwa wanaoa walipewa hela, nyumba, na mengineyo.
Inawezekana kweli walikuwa wanapewa hivyo vitu lakini je, walikuwa wako huru kiasi gani?
Gadafi alikuwa dikteta. Tena dikteta mkubwa tu aliyeng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu sana hadi walipomfurumsha.
Mtukufu rais Magufuli naye watu wengi wameshaanza kumwona kuwa ni dikteta. Hataki watu wafanye siasa kwenye maeneo yasiyo yao.
Tumeshaona na kusikia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa makosa ya kumtukana/ kusema maneno mabaya dhidi yake.
Tumeona vyombo vya habari vikifungiwa kwa sababu zisizo na mashiko.
Sasa haya mambo ya yeye kuisifia Libya ya Gadafi mimi yananitatiza.
Nabaki najiuliza maswali tu. Ina maana yeye Magufuli alikuwa anamwona Gadafi kuwa ni kiongozi bora aliyeweza kutunza amani huko Libya hadi awe anaisifia sifia hivyo?
Kama Gadafi ndo mmoja wa viongozi ambao Magufuli anawaona kama mfano mzuri wa utunzaji wa amani, watu wakimwona na yeye dikteta watakuwa wanakosea kweli?
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?
Nani aliomba upuuzi uo labda waulize Mimi cha kwanza kwangu ni Uhuru,
Wa kusema
Kutembea
Kutotharirishwa
Mwambie uchara ajipange tunataka democracy
Mbona Kikwete alijenga barabara za kutosha kwani udicteta wake hata saa hii unanilishaUtakula huo Uhuru?
Uhuru ndio utajenga barabara na kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kupata elimu bora? Uhuru ndio utaleta madawa hospitalini?
Ingekuwa hivo nchi za kiafrika zisingekuwa hapa kimaendeleo miaka zaidi ya 50 tangia zilipoanza kupata Uhuru.
!
!
labda model wake ni waina hii....Akina Sadam wa Iraq , akina Gadaffi wa Libya, akina Asad wa Syria.