Meropenem
Member
- Dec 14, 2016
- 23
- 14
Nimekua nikifuatilia mwenendo wa mkuu wa nchi tangu kipindi anatushawishi tumchague.Alikua mtu wa uhakika na wengi waliamini utekelezaji wa anachokiahidi.Moja ya vitu muhimu alivyoahidi ilikua elimu bora kwa gharama nafuu.Mpaka sasa nashindwa kuelewa alitudanganya au hakumbuki alichoahidi.Mambo yafuatayo yamekua yakididimiza kuliko kupandisha elimu
1.Kuwanyima mikopo wanafunzi wa vyuo either wanaoanza au kuendelea na masomo.kazi yangu inanifanya nifike kwenye baadhi ya vyuo vikuu mara kwa mara.Mwanzoni mwa mwaka wa masomo nimekua nikikutana na wanafunzi wengi walioandika barua kusitisha au kuahirisha masomo.Hii inaletwa na kukosa mkopo
2.Uteuzi wa wahadhiri kwenye nafasi mbalimbali za kiuongozi serikalini.Hakuna elimu bila mwalimu.Leo hii Udsm na udom wameanza kulalamikia uhaba wa wahadhiri sababu ni wachache na serikali imewachukua
3.Ukosefu wa walimu shuleni.Kila mtu anajua namba ya walimu mashuleni ni ndogo.Binafsi baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari nilifanya kazi kama mwalimu wa kujitolea nikifundisha masomo ya sayansi ambayo hayakua na walimu katika shule moja ya mkoa wa Tangu hukua wakinipatia posho kidogo ambayo inatoka kwenye michango ya wazazi.Leo hii hili haliwezekani na pesa hakuna
4.Ubadilishwaji wa mitaala usioeleweka.Shule za msingi kuna baadhi ya shule zimepokea mtaala mpya na kupata semina kuhusu mtaala huo ambao unaonyesha elimu ya msingi mwisho la sita.Waziro wa elimu alikanusha lakini mtaala umeanza kutumika baada ya semina kuisha
5.Hali ya kifedha ya walimu na wafanyakazi kwa ujumla.Hili amezidi kuliharibu siimhitaji kulielezea kila mtu anajua
Naiomba serikali ijitafakari upya.Ibadili njia ya kusimamia elimu kabla mambo hayajaharibika