Rais Magufuli na Elimu Bure

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Kumekuwa na majadiliano marefu, mazito na makali kuhusu bia ya Rais Magufuli kutoa elimu bure. Elimu ni falsafa ya siku nyingi iliyoanzishwa na Baba wa Taifa.

Katika mijadala mingi suala limekuwa ni ubora wa elimu na siyo elimu bure. Kwa mfano watoto wa shule za msingi kusoma wakikaa chini.

Hili Rais Nagufuli ameliona na kulichukulia hatua. Jana kwenye sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa CCM, mkoani Singinda amewaagiza viongozi wote wa Mikoa (Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi) kupunguza safari na tafrija (ulaji) ili fedha hizo zitumike kununulia madawati ili watoto wasikae chini.

Amenukuliwa na Mwananchi, Jumapili, Februari 7, 2016: "Hiki (kupunguza safari na ulaji) kitakuwa kipimo cha wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi, ikiwa sivyo itabainisha kwamba nafasi uliyonayo haikufai, kwa hiyo kila mmoja ajipange katika kuhakikisha anatoa kero kwa watu anaowaongoza".

Ubunifu, uwajibikaji na uzalendo ni baadhi ya sifa za viongozi wa Serikali ya sasa ambazo Rais Magufuli anasisitiza. Mungu amjalie maisha marefu kwa hekima na busara anazoonyesha.

Mimi na Wewe:
CHAMBUA CHUNGUZA AMUA CHUKUA HATUA
 
Elim Bure isubiri bajet ya 2016/17.
Mafungu ya 2015/16 yarumike kuboresha miundombinu,watoto wanakaa chini kweli,zana za kufundishia ni duni wallah
 
Back
Top Bottom