Rais Magufuli: Mimi ni Rais kweli kweli, jiwe. Sitishwi wala sitishiki; azindua kiwanda cha Alizeti mkoani Singida

"Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni"

Hii kufuru itamfuata hadi kwenye kaburi lake
 
Hicho kiwanda kinafanya kazi hapo miaka mingi sana!! Zamani kilikuwa kikiitwa bunda mills kabla ya kununuliwa na Mount meru millers (Lalaa)nimefika kwenye hicho kiwanda mwaka 2011 na kilikuwa kinapiga kazi! Magu kaenda kukizindua Leo!!! Maajabu
Teh! Teh! Ndio Tanzania ya Viwanda hiyo
 
Mimi sikuwa nafahamu kumbe raisi wetu ni jiwe. Hivi ni jiwe la mtoni au la barabarani?
 
"Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni"

Hii kufuru itamfuata hadi kwenye kaburi lake
Hivi huyu anamfanya Muumba kuwa mtani wake? Asome historia juu ya mwisho wa watu waliomdhihaki Muumba wa mbingu na nchi.
 
Kwa wanaoangalia ZIARA ya MHESHIMIWA RAIS mkoani singida tumemsikia WAZIRI MWIGULI akifunguka ukweli juu kilicho jificha kwa sasa ndani ya nchii yetu juu hizi vugu vugu kwa sasa zinazochagizwa na WAPINZANI WASIOITAKIA MEMA NCHI YETU mfano UTEKAJI,MAUAJI.....maandamano yanayoandaliwa hapo 26/04/2018...kasema ni ukweli usiopingika haya mambo ya kutisha kabsa yanatokea kwa sasa baada ya WAPINZANI wa NCHI HII kukosa hoja za kisiasa juu ya serikali iliyopo madarakani na matokeao yake wanatafuta njia mbadala ya kuchafua picha ya SERIKALI YETU mfano kuitisha maandamano yasiyoruhusiwa KISHERIA na wao kutumia mwanya huo kufanya mauaji na mwisho wa siku kuihusisha serikali iliyo madarakani...
Unajua nyie watu mnajitekenya halafu mnacheka wenyewe,sasa kama wameishiwa hoja mbona mmewazuia kufanya mikutano ya kisiasa na kuwafunga kila siku!? Kama nyie wanaume si muwaache mshindane kwa hoja!!
Yani ni sawa na kupigana na Mtu aliyefungwa mikono kwa kamba then baadae ujisifu kwamba eti umempiga,huo kama si upumbafu ni kitu gani!?

Wekeni silaha chini mshindane kwa hoja wananchi waamue
 
kiwanda kipo tangu kabla ya 2015 anazindua nini? halafu ni cha Wahindi.

kweli hii serekali kwa kiki sidhani kama ipo ya mfano wake duniani!
Duh!! Ebu jaribu kuficha ujinga,eti cha wahindi, wewe ulitaka kiwe cha nani?

Wakati wewe baada ya kupambana na kuona fursa ila wewe unashinda kwenye mitandao ya kijamii kufanya siasa na kupinga kila kitu wanachokifanya serikali.

Kwa style hii waache wahindi wachukue fursa maana unayejihita mtanzania halisi umekalia siasa siasa kila jambo,majungu,fitina na chuki dhidi ya serikali.
 
ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.
Kwa Uongozi upi apewe hiyo nafasi? Anyway Mungu si Athumani. Sitaki kuandika wala kusema sana nisimkosee Mungu wangu bure.
 
Watanyooka tu, waponde mpaka wapondeke, ila tutafuata sheria bila shuruti, tutafanya kazi na kuziheshimu, tutawajibika hata kama tulizoea kubabaisha, tukiiba tutanyea debe..
 
Back
Top Bottom