Rais Magufuli, Mama Ndalichako, mnadhani mko sahihi kuichukulia Div.3 ya Sayansi sawa na ya Arts?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,316
Watanzania wenzangu,viongozi na wadau mbalimbali wa elimu,nadhani wakati umefika tutofautishe masomo ya sayansi na masomo kama ya Arts na Biashara kwani hivi ni vitu viwili tofauti kabisa na kimoja kikiwa ni mbingu na kingine ni ardhi.

Nayasema haya kufuatia taarifa zisizo rasimi kwamba hivi sasa kuna mabadiliko yanakuja ambayo ili mtu aweze kujiunga chuo kikuu kuchukua shadada ya kwanza ni lazima awe na Division 1 au 2 ya kidato cha 6 na wala sio 3 na kama ataingia kwa Equivalent qualifications, basi awe na Diploma ya kuanzia GPA 3.3 na kuendelea(sijui ukweli wa taarifa hizi).

Nia na dhamira inaweza kua ni njema kabisa,lakini kwa upande wa sayansi, mtatuletea janga la elimu katika sayansi na zaidi kuturudisha nyuma kama kweli huu ndio mpango uliopo.

Masomo ya sayansi mbali na kuwa ni magumu,pia bado yana changamoto nyingine nyingi kuliko masomo ya michepuo mingine:ukosefu/upungufu wa majengo ya maabara, ukosefu /upungufu wa vifaa vya maabara, ukosefu wa walimu, wanafunzi wachache wanaojiunga na masomo ya sayansi,shule chache za michepuo ya sayansi, n.k.Hizi zote ni changamoto ambazo kwa namna moja au nyingine zinapelekea kuwa na wahitimu wachache wa masomo ya sayansi na zaidi ufaulu mdogo wa masomo ya sayansi katika shule zetu hasa shule za serikali ambako ndiko kimbilio la watanzania wengi wasiomudu gharama za shule za binafsi(private schools).

Mbali na changamoto hizo,mtu anayesoma sayansi anatakiwa kufanya paper 3 kwa kila somo moja katika mtihani wake wa mwisho tofauti na yule wa arts au biashara anaefanya paper mbili tu kwa somo moja.

Kwa mfano,mwanafunzi anaechukua combination ya PCB,atatakiwa kufanya jumla ya paper 11 kama ifuatavyo.

1.Paper 1 ya physics
2.Paper 2 ya physics
3.Paper 3 ya physics(practicle)

Hali ni hiyo hiyo kwa Chemistry na Biology bila kusahsu somo la General Studies na Basi Applied Mathematics jumla ya masomo yanakuwa 11.

Kwa upande wa mchepuo wa arts na biashara hali ni tofauti kabisa.Mtu anaesoma HGE kwa mfano anakuwa na jumla ya paper 7 tu ambazo ni:
1.History 1
2.History 2
3.General Studies

Hali ni hiyo hiyo kwa masomo yaliyobaki ya Geography na English. Ukijumlisha na somo la General study anakuwa na jumla ya paper 7ikiwa ni tofauti ya paper 3/4 na mtu wa sayansi.

Hivyo basi nawashauri viongozi na watunga sera za elimu wa nchi hii,wabadili mtazamo na kuruhusu wanaopata division 3 katika masoma ya sayansi kwenye mtihani wa kidato cha sita waruhusiwe kujiunga na vyuo vikuu kuchukua shahada ya kwanza.Tofauti na hapo,tutarajie yafuatayo siku za usoni:

1.Wanafunzi wachache wa sayansi kudahiliwa katika vyuo vikuu

2.Vitivo vya sayansi katika vyuo vikuu kukuosa wanafunzi.

3.Vyuo vingi vya private vinavyotoa shahada za masomo ya sayansi kukosa kabisa wanafunzi na pengine hata vitivo hivyo kufutwa

4.Wahadhiri wa masomo ya sayansi katika vyuo vikuu vingi hasa ya binafsi kupoteza ajira

5.Kuongezeka kwa tatizo la walimu wa sayansi kwani mtu aliepata division 1 au 2 ni vigumu kukimbilia kwenye ualimu fani ambayo inaonekana kusahauliwa huku walimu wengi wakiwa ni watu wa kulalamikia maslahi duni(wenye 3 wangeanda tofauti na waliopata 1 na 2).

Tutambue hivi sasa tuko kwenye zama za Proliferation of Regional Integration kama vile East African Community(EAC),COMESA n.k.Hapa maana yake ni kwamba tunaruhusu muingiliano baina ya mataifa ya nchi washirika huku watu wetu wengi wakiwa hawana elimu ya vyuo vikuu. Hii ni hatari sana.Watanzania wengi watakosa fursa za ajira na kutoa mwanya kwa wasomi kutoka nchi washirika kuchukua ajira za wazawa.

Viongozi wa awamu ya 5,badala ya kuvuruga karibu kila kitu cha awamu iliyopita,ni bora mkaelekeza nguvu katika kuviboresha na kuviendeleza tofauti na hapo ya sukari yatajirudia katika elimu na si kwa sayansi tu,bali hata katika nyanja zingine kama arts na biashara.

Hivi sasa ni bora mkaelekeza nguvu katika elimu ya msingi na sekondari kwa lengo la kuboresha elimu na kuongeza ufaulu ili kupata wanafunzi wengi zaidi wa kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini badala ya kuanza kuvuruga huko juu(vyuoni).

Imarisheni msingi kwanza huko juu itakuwa ni kama tu kumsukuma mlevi.

Ukweli ni kuwa,watu husoma masomo ya aina fulani kwasababu wanayapenda na ni ukweli pia watu wote wanaosoma sayansi wanaisoma kwasababu wanaipenda lakini si kweli pia watu wote wanaosoma masomo yasiyo ya sayansi wanayapenda masomo hayo bali wapo baadhi waliipenda zaidi sayansi ila waliikimbia wakijua kuwa sayansi ni ngumu.
 
Kuna graduate wengi tu watakuwa walimu hao division 3 ni vilaza hawana sifa za kuwa walimu
 
Kweli hii nchi ilishalaaniwa, hiv hizo one na two ziko ngapi hapa nchin? fuatilieni takwimu kwanza ndo mlete majibu hapa. Halafu hatuwezi ku control udahili kwa kuangalia uwezo wa bodi ya mikopo nyie wasengerema, yan uache div 3 ambazo zinaweza kupata nafasi chuo sababu unaogopa kuonekana umeshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wote, hii akili au tope? kama wanafunz wamefikisha GPA inayotakiwa kwa udahili waingie vyuoni, tunakokwenda tunahitaji wasomi wengi, japokuwa wanaweza wasiwe na weledi sana, lakin mambo ya weledi market yenyewe itabalance. Hii dunia inakoenda regional integration itawaacha watu wetu vibarua tu sababu CCM hamna akili za kuangalia mbele.
 
Kweli hii nchi ilishalaaniwa, hiv hizo one na two ziko ngapi hapa nchin? fuatilieni takwimu kwanza ndo mlete majibu hapa. Halafu hatuwezi ku control udahili kwa kuangalia uwezo wa bodi ya mikopo nyie wasengerema, yan uache div 3 ambazo zinaweza kupata nafasi chuo sababu unaogopa kuonekana umeshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wote, hii akili au tope.
tope
 
Back
Top Bottom