Rais Magufuli, Mafuru apelekwe mahakamani sio kupangiwa kazi nyingine

Halafu hivi hio FNBE bank, ina operate wapi hio bank Tanzania?
Dawa ya kumpuuza mtu uwa ni kutochangia chochote kwenye anachokiandika ..

Unapoandika kwa kejeri maana yake umeguswa ...

Nakushauri acha kejeri kwa wengine ambao uwajui wametumwa nini humu au wanafanya nini maana ndio tabia yako .......

Ukiona kitu ukipendi au kina utata uwa unasoma unapita kimya kimya.......
 
Hii thread imenifahamisha vitu vingi kuhusu Mafuru. Kumbe ni board member crdb. Hapo lazima kuwe na conflict of interest
 
Hakuna typo hapo,hujui unachokiandika.Mi ni fisadi mlalahoi a.k.a Choka mbovu kama kuna wa kunishughulikia anakaribishwa.Next time tuliza Uno chini andika vitu vinavyoeleweka.
Habari yako hio hata mtu aki connect dots+ reading between the lines haina maana yoyote.
Eti typo , typo ndio nini kama na wewe ni mtu uliye makini?

Very foolish.....
 
Acha kuongea ujinga. Jamaa yupo vzr sn UPSTAIRS. Ni bahati mbaya sn kajuchanganya ccm inatakiwa mtu km yule aishi na mawazo huru sio kumtumikia mkurupukaji. Ni hazina kubwa kwa taifa akikaa nje ya mfumo mchafu wa ccm
Hata hiyo upstairs nzuri akitumia vibaya aachwe tu?
 
Salaam.....

Kwanza Mh. Rais Nikupongeze tu kwa kazi kubwa unayoifanya kuendesha nchi kwa kutumia nguvu, akili na uwezo wako binafisi kuongoza watu m 50 sio kazi ndogo.

Pia nikukumbushe kuwa kuna jambo nilikuwa sijakwambia

Ulimuondoa Dr Dau NSSF ukampangia kazi nyingine nikanyamaza.

Ukamuondoa Katibu Mkuu kiongozi ukampangia kazi nyingine nikanyamaza.

Sasa umemuondoa Mafuru na kuahidi kumpangia kazi nyingine hapa sitanyamaza hata kidogo.

Mafuru anatakiwa apitie mahakamani kwanza kabla ya kazi nyingine.

Huyu si ndio alipiga pesa pale NBC kwa kuwakopesha watu wa magari ya mizigo ndio zao la GSM na matokeo kushindwa kurejesha pesa na mmoja wa wanufaika si ni mtoto wa mfalme aliyepita mashahidi wapo wa kukusaidi pale Bacrays Bank.

Kesi ikazimwa akapelekwa kwenye BRN (Big Result Now) matokeo makubwa sasa kilichotokea huko watanzania wanajua na dunia inajua pesa iliyokuwa ikipigwa hata ukiangalia kwenye Vitabu vya auditing vya CAG wakati huo ni madudu na huyo ndiye alikuwa mratibu wa ushenzi wote huo wafanyakazi wa BRN wakajitajirisha kwa ufisadi.

Akatoka hapo akaenda FBME bank huko utakatishaji wa pesa ndiko ulifanyika kwa kiwango cha kutisha.

Akaja HAZINA hapo sasa ndipo amefanya madudu ya kila aina ikiwemo kusajiri hisa 51% zilizouzwa kinyemela za UDA kutoka jiji kwenda tena kwa mmoja wa mwana wa mfalme aliyepita .

Alifanikiwa kusajiri pia hisa za kampuni ya Rugemalira ambayo ni kampuni iliyofanikisha ukwapuaji wa pesa bilioni 76 ($39 Milioni) Escrow account kwenye zile bilioni 320 zilizochotwa kwa magunia pale Mkombozi na Stanibic bank.

Huyu sasa hivi ni Member wa Bodi ya CRDB na ndio walikuwa wanafanya Lobbying kufungua fixed deposit account ili kuendelaea kufanya ujanja ujanja wa kuzichezea bank zingine faulo ndio maana ulimuona akitoka hatharani kukukana kuwa si dhambi kufungua FD huku akijua bank itakayopata wateja wengi Serikali ni CRDB ambayo yeye ni member wa bodi hiyo.

Mtu kama huyu unampangia kazi nyingine?

Mtu anayeonekana kushirikiana na majizi kukwapua na majambazi wa nchi hii kuiba mali za umma bado anapangiwa Kazi nyingine baada ya kumuburuza mahakamani?

Hawa watu ni wa kuweka kuzuizini na kuchunguza mali zao sio kuwapangia kazi nyingine.

Kazi yangu ni kukwambia ukweli weka watu hawa chini ya TAKUKURU wachunguzwe mafisadi waondoe kwenye mfumo lasivyo watakukwamisha utaona 2020 hiyo uku ukiendelea na panga pangua.
Braza uko vizuri
 
Eti typo , typo ndio nini kama na wewe ni mtu uliye makini?

Very foolish.....
Hahah kumbe we punga una tatizo hata typo hujui ni nini?Aisee
Typo-an error (as of spelling) in typed or typeset material
upo hapo we kichaa.Rudi darasani kasome tena.
 
Hahah kumbe we punga una tatizo hata typo hujui ni nini?Aisee
Typo-an error (as of spelling) in typed or typeset material
upo hapo we kichaa.Rudi darasani kasome tena.
Very stupidity,rubbish
 
hivi mtumishi wa umma kuwa mwenyekiti wa taasi binafsi kisheria na kiutaratibu inaruhusiwa?

Hakuna popote mtoa mada kasema Mafuru ni mwenyekiti wa bodi ya CRDB bali alisema ni mjumbe (member) wa bodi ya CRDB. Kuwa mwenyekti wa bodi ni tofauti na kuwa mjumbe bodi. Go and read his post between lines, siyo kupostpost tu madudu kimazoea.
 
Salaam.....

Kwanza Mh. Rais Nikupongeze tu kwa kazi kubwa unayoifanya kuendesha nchi kwa kutumia nguvu, akili na uwezo wako binafisi kuongoza watu m 50 sio kazi ndogo.

Pia nikukumbushe kuwa kuna jambo nilikuwa sijakwambia

Ulimuondoa Dr Dau NSSF ukampangia kazi nyingine nikanyamaza.

Ukamuondoa Katibu Mkuu kiongozi ukampangia kazi nyingine nikanyamaza.

Sasa umemuondoa Mafuru na kuahidi kumpangia kazi nyingine hapa sitanyamaza hata kidogo.

Mafuru anatakiwa apitie mahakamani kwanza kabla ya kazi nyingine.

Huyu si ndio alipiga pesa pale NBC kwa kuwakopesha watu wa magari ya mizigo ndio zao la GSM na matokeo kushindwa kurejesha pesa na mmoja wa wanufaika si ni mtoto wa mfalme aliyepita mashahidi wapo wa kukusaidi pale Bacrays Bank.

Kesi ikazimwa akapelekwa kwenye BRN (Big Result Now) matokeo makubwa sasa kilichotokea huko watanzania wanajua na dunia inajua pesa iliyokuwa ikipigwa hata ukiangalia kwenye Vitabu vya auditing vya CAG wakati huo ni madudu na huyo ndiye alikuwa mratibu wa ushenzi wote huo wafanyakazi wa BRN wakajitajirisha kwa ufisadi.

Akatoka hapo akaenda FBME bank huko utakatishaji wa pesa ndiko ulifanyika kwa kiwango cha kutisha.

Akaja HAZINA hapo sasa ndipo amefanya madudu ya kila aina ikiwemo kusajiri hisa 51% zilizouzwa kinyemela za UDA kutoka jiji kwenda tena kwa mmoja wa mwana wa mfalme aliyepita .

Alifanikiwa kusajiri pia hisa za kampuni ya Rugemalira ambayo ni kampuni iliyofanikisha ukwapuaji wa pesa bilioni 76 ($39 Milioni) Escrow account kwenye zile bilioni 320 zilizochotwa kwa magunia pale Mkombozi na Stanibic bank.

Huyu sasa hivi ni Member wa Bodi ya CRDB na ndio walikuwa wanafanya Lobbying kufungua fixed deposit account ili kuendelaea kufanya ujanja ujanja wa kuzichezea bank zingine faulo ndio maana ulimuona akitoka hatharani kukukana kuwa si dhambi kufungua FD huku akijua bank itakayopata wateja wengi Serikali ni CRDB ambayo yeye ni member wa bodi hiyo.

Mtu kama huyu unampangia kazi nyingine?

Mtu anayeonekana kushirikiana na majizi kukwapua na majambazi wa nchi hii kuiba mali za umma bado anapangiwa Kazi nyingine baada ya kumuburuza mahakamani?

Hawa watu ni wa kuweka kuzuizini na kuchunguza mali zao sio kuwapangia kazi nyingine.

Kazi yangu ni kukwambia ukweli weka watu hawa chini ya TAKUKURU wachunguzwe mafisadi waondoe kwenye mfumo lasivyo watakukwamisha utaona 2020 hiyo uku ukiendelea na panga pangua.

Umeongea mengi sana. Kama alivyo Mafuru, mfumo ulijaa watu wa namna hiyo na bado hawajaisha. umetaja watu ambao wameenguliwa na kupangiwa kazi nyingine. Kwa tasfiri yako ni kwamba nao ni mafisadi ila sio kwa kiwango cha Mafuru. Usiwe mtu wa kuangalia sheria kwa upande mmoja, unaona haki kwa Mafuru kupandishwa mahakaman ila hao wengine huoni kuwa ni haki!!! Maana kama ingekuwa haki usingekaa kimya, bali ungepasa sauti kama ulivyofanya hapa.

Well and good, nafikiri sheria haitakiwi imkomalie mmoja na impendelee mwingine. Watanzania tuache harakati za kukomoana. Hii thread ni nzuri ila ina-reflect upendeleo wa wazi kwa watu fulani. Sion haja ya kusema Mafuru apande mahakamani huku unawaacha wengine wenye tuhuma kama za kwake wabaki salama na ulikaa kimya!! Kwa mwendo huu wa sheria kuchagua watu wa kukomaa nao na kuwaacha wengine, hakutapunguza ufisadi ndani ya taifa letu, bali utatengeneza ufisadi mwingine utakaofanywa na wengine watakaolindwa na sheria na sio wale waliozea. Waliozoewa watapandishwa kizimbani kama kafara, na kwa kuwa ni "untouchable" watashinda kesi na sisi tutashabikia kwamba walipandishwa kizimbani. Usinielewe vibaya kuwa nashabikia ufisadi, ila sheria haitakiwi kuwa double standard kama unavyotaka kuniamisha mkuu!
 
Endeleeni kumchochea, mwisho wa siku hakuna atakayeweza kufanya naye kazi, labda J wa chuo cha kata!

Hayo ya ufisadi kama yapo sawa apelekwe mahakama lakini sio unaongea uongo kugain popularity ukisahihishwa unafura kwa hasira as if kifaru ameshikwa masaburi!
professionalism iheshimiwe!

Kifaru kishikwa nini eti.....................!!!!! Hataree sana
 
Jamaa alijidai kuto kuwapatia kazi watuhumiwa lakini sasa anawapatia anaendeleza siasa za maji taka
 
Umeshajua maana ya TYPO?
Sifa za kijinga unaonekana utakuwa mhaya au wa kigoma maana ndio wapenda sifa .....

Hata nimepekua threads zako nimekuona ni wa hovyo sana ....

Nenda ubishane na watu type yako hili ni jukwaa huru Fanya yako achana na Mimi unijui wala sikujui ukiona kitu ukipendi pita kimya kimya acha tabia za kike kike fala wewe
 
Akatoka hapo akaenda FBME bank huko utakatishaji wa pesa ndiko ulifanyika kwa kiwango cha kutisha.

Akaja HAZINA hapo sasa ndipo amefanya madudu ya kila aina ikiwemo kusajili hisa 51% zilizouzwa kinyemela za UDA kutoka jiji kwenda tena kwa mmoja wa mwana wa mfalme aliyepita
Maelezo yako mengine ni majanga tupu; ni vile tu watu humu ni zoa zoa wa chochote wanachokisikia, basi ni rahisi kuwadanganya!! Jana hapa nilisema wazi kwamba naona taabu kubishana na watu lakini mtu akiamua kuchambua hayo madai yako; si ajabu akakuta mengi ni ya kupika... kwa makusudi au kwa kutolewa!

Habari za mwanzoni kabisa kuhusu kashifa ya utakasaji fedha FMBE zilitolewa April 21, 2012 na Gazeti la The East African. Sehemu ya taarifa hiyo inasema:
Italy’s Guardia di Finanza (the financial unit of the tax police in Rome) is presently investigating a questionable 4.5 million euro ($5.9 million) transfer to Tanzania, while 1.2 million euros ($1.5 million) were sent to Cyprus and 1 million euros ($1.3 million) were invested in Norway Crowns.

Investigation by The EastAfrican in Dar es Salaam showed that the money in question was sent to Tanzania through Federal Bank of the Middle East (FBME) in Cyprus and then to FBME Bank in Tanzania. Mr Belsito was apparently the one who deposited the money in the Tanzania bank.

Tanzania’s Financial Intelligence Unit (FIU) is investigating the case on suspicion of embezzlement, aggravated fraud committed against the state and money laundering.
Wakati kwa mara kwanza kashifa inaripoitiwa ilikuwa ni April 2012; Mtandao wa Allafrica.com unatoa taarifa za Mafuru kusimamishwa kazi NBC... habari imetolewa July 12, 2012. Sehemu ya habari hiyo inasomeka:
THE Managing Director of National Bank of Commerce (NBC), Lawrence Mafuru has been asked to take time off work to allow investigations that allegedly perpetrated at the bank.

It was announced by the Board of Directors of NBC Limited that Mr Mafuru has been requested and accepted to go on leave .The Chairman of NBC Board of Directors, Dr Mussa J Assad said, "The Board of Directors of NBC has received allegations of irregularities against NBC Executive Management. NBC is a reputable and trusted bank for best practice and good governance.
Kumbe basi tutaona wakati FMBE inakumbwa na kashifa ya money laundering, Mafuru bado alikuwa NBC huku wewe ukitaka kuaminisha watu kwamba, alitoka BRN akaenda FMBE ambako likatokea suala la utakasaji fedha! By the way, Mafuru alienda FMBE lini na kwa malengo gani? Africa Leadership Initiative East Africa Foundation wanaripoti uteuzi wa Mafuru kuwa STATUTORY MANAGER wa FMBE na sehemu ya taarifa inasema:
Considering the potential effect of the decision taken by CBC to take over FBME’s Bank branch in Cyprus which may likely bring into the banking system in Tanzania, and consistent with the provisions of of section 56(1)(g)(iii) of the Banking and Financial Institutions Act 2006, the Bank of Tanzania has taken over the management of FBME Tanzania Limited effective 24th July 2014. The Bank of Tanzania has accordingly appointed Mr. Lawrence Mafuru as Statutory Manager with immediate effect to handle all matters pertaining to the bank.
Kumbe, wakati kashifa ya FMBE imetokea mwaka 2012 kurudi nyuma, Mafuru alipelekwa FMBE mwaka 2014; miaka miwili baada ya taarifa za scandal za FMBE kuwa hadharani lakini unataka kuaminisha watu kwamba, baada ya Mafuru kwenda FMBE, ndo yakaja hayo ya money laundering!! Na alipelekwa huko na BoT kwa sababu FMBE ilikuwa chini ya uangalizi wa BoT!

Aidha unadai alipotoka FMBE, ndipo
Akaja HAZINA hapo sasa ndipo amefanya madudu ya kila aina ikiwemo kusajili hisa 51% zilizouzwa kinyemela za UDA kutoka jiji kwenda tena kwa mmoja wa mwana wa mfalme aliyepita .

Alifanikiwa kusajili pia hisa za kampuni ya Rugemalira ambayo ni kampuni iliyofanikisha ukwapuaji wa pesa bilioni 76 ($39 Milioni) Escrow account kwenye zile bilioni 320 zilizochotwa kwa magunia pale Mkombozi na Stanibic bank.
Tuanze na hilo la Mafuru kwenda Hazina... alienda Hazina kama Msajili lini? The Citizen wanaripoti taarifa za JK kumteua Lawrence kuwa Msajili wa Hazina. Habari hii ya The Citizen ni ya December 12, 2014 na sehemu ya habari hiyo inasema:
President Jakaya Kikwete has appointed Mr. Lawrencee Mafuru as Treasury Registrar. The President has also made seven other appointments, Chief Secretary Ombeni Sefue said in a statement.

He said, Mr. Mafuru's appointment came into effect on November 5.
Kumbe Mafuru aliteuliwa kuwa Treasury Registrar on November 05, 2014. Na kwa maelezo yako, hapo ndipo akafanikisha upigaji wa Escrow!

Hebu tuone Escrow Saga ni wakati gani ilienda public? Gazeti la Mwananchi la May 09, 2014 sehemu ya habari yake inasema:
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh. 200 bilioni zilichotwa katika kampuni ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya TANESCO na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Hapo habari ya Escrow ndipo ilifahamika na wengi lakini kwa mara ya kwanza iliripotiwa lini? The Citizen la March 10, 2014, sehemu ya habari yake ya kiuchunguzi inasema:
The $122 million (Sh.201 billion), which was at the escrow account held at the Bank of Tanzania(BoT), was transferred to Pan Africa Power Solutions (Tanzania) Ltd (PAP) account between November 28 and December 8, last year, The Citizen can reveal today.
Kwa maelezo hayo inaonesha hadi March 2014 tayari habari zikaanza kwenda public huku tukijuzwa pesa ilipigwa mwaka mmoja nyuma; yaani kati ya November 28, 2013 hadi December 08, 2013.

Hapo watu ndo wanapiga rasmi, upigaji ulikuwa approved lini? The Citizen tena hawa hapa:
According to details gathered by The Citizen, which are also corroborated by official correspondence from the BoT to the Treasury, the agreement to release the escrow billions was signed on October 27, 2013
Kumbe hadi kufikia October 27, 2013, kila kitu kilikuwa kimeshakamilika! Lakini wewe unadai Mafuru alipelekwa Hazina na akafanikisha deal la Escrow wakati yeye aliteuliwa Msajili wa Hazina November 05, 2014 wakati mchezo ulimalizwa tangu October 27, 2013... almost a year earlier!!!

Hebu tuangalie hilo la hisa za UDA unazodai ni Mafuru ndie alifanikisha usajili wake wakati yupo Hazina! Hapo juu tumeshaona Mafuru alienda Hazina November 05, 2014. Ina maana 51% ya Hisa za UDA zilisajiliwa after November 05, 2014?

Awali ya yote jambo ambalo lipo wazi tunaelezwa zile hisa tunazoambiwa ni za Simon Group yeye ni kivuli tu cha Mwana Mfalme. Kwa maana nyingine, kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba, huyu Mafuru ndie anahusika na usajili wa hisa za Simon Group ambazo zinasemekana ni za Mwana Mfalme! Mwanahalisi hawa hapa:
Nyaraka zinaonyesha mkataba wa mauziano ya hisa kati ya jiji na SGL (Simon Group Ltd) ulifanyika 11 Februari 2011.

Katika kile kinachoweza kuitwa kuweka mazingira vizuri, tarehe 6 Juni 2011, Robert Kisena, aliandikia barua msajili wa hazina na mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam akiwataka kuitishwa mkutano wa wanahisa ili kuliokoa shirika hilo.
Aidha Mwanahalisi wanaedelea:
MwanaHALISI limefahamishwa uuzaji wa UDA umegubikwa na utata. Kwa mfano, mchakato wa uuzaji wa UDA ulianza mwishoni mwa mwaka 2010, lakini ulipamba moto wakati Dk. Masaburi aliposhika kiti cha umeya Februali 2011.
Hata hapa JF napo, miaka kadhaa iliyopita suala la hisa za UDA kwenda kwa Simon Group lilijadiliwa. Hii ni quote kutoka kwenye habari ndefu ambayo imezungumzia hilo suala:
Shareholders: Dar es Salaam City Council, Simon Group Ltd and the government through the Treasury Registrar agreed in principle last December that the second evaluation should be done for the purpose of clearing the air over the much hyped malpractices and non-adherence to set procedures during the sale of UDA shares to Simon Group Ltd in February 2011.
Hiyo ni post ya March 23, 2012. Kumbe by the time, watu walikuwa washapiga hisa za UDA lakini wewe unadai Mafulu ambae aliingia Hazina November 2014; takribani miaka 3 baadae ndie alifanikisha upigaji wa hisa za UDA!!!

Unajisikiaje kupotosha kwa tuhuma mzito kama hizo? Hapo moja kwa moja inaonesha madai yako mengi kama sio yote is COMPLETELY BIG LIE....

c.c Pascal Mayalla, Mbase1970
 
Back
Top Bottom