Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,858
Raisi Magufuli,japo mimi si mwana-CCM,lakini nakiri hadharani kumkubali sana mbunge wa chama chako, mh. Hussein Bashe kwani anaonyesha ni mbunge makini,mzalendo na mwenye uchungu na nchi hii na mwenye uelewa mzuri wa maswala ya fedha na uchumi.
Ukimsikiliza Hussein Bashe utagundua kabisa kuwa anaongea kwa uchungu tena kutoka moyoni na anajua ni nini cha kufanya kurekebisha mapungufu yaliyopo ila ni bahati mbaya tu hayuko katika nafasi inayomuwezesha kutekeleza mawazo yake zaidi ya kushauri tu.
Mh.nakuomba ujaribu kufikiria kumpa nafasi ya kumsaidia Waziri wa Fedha kwa kumteua kuwa Naibu Waziri kwani ninaamini atakuwa na mchango mkubwa sana katika kuleta mabadilko na tija katika wizara hiyo iwapo atapata hiyo nafasi na pia hataingiliwa au kukwamisha na mamlaka za juu katika utendaji wake.
Mh.Raisi,Hussein Bashe ni hazina ndani ya chama chako kama walivyo kina Tundu Lissu ndani ya upinzani hivyo itumie hiyo hazina kwa manufaa ya nchi hii.
Ni ushauri tu.