Michezo itenganishwe na mambo mengine isichanganywe na habari , yaani kulipaswa kuwepo na wizara ya michezo tu Kama ulivyo wizara ya Fedha au maji , yaani awepo waziri aliyecheza michezo mpenda michezo, Katibu Mkuu awe mwanamichezo bajeti ya wizara ya michezo iwe ya kitosha inayokidhi gharama za kusafirisha Timu kwenda mashindano ya kimataifa nk, Kwa sasa michezo imedorola Kwa sababu mawaziri si wanamichezo pia wapo busy na kufungia Radio, magazeti na mambo mengine huku waziri akiwa Hana mzuka na michezo kabsa, Ni vyema wizara ya michezo iwe peke yake hizo habari zipelekwe kwingine huko wizara ya sayansi na tekinologia.