Rais Magufuli, kuwapunguzia mshahara walio juu ili uwaongezee wa chini ni sawa, lakini...

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
Nimemsikia Leo Rais wetu alipokuwa mwanza kuwa atawapunguzia mshahara watumishi wa umma walio na mshahara mikubwa.

Rais ametoa mfano kuwa kuna watumishi wanalipwa mil 40 kwa mwezi, jambo lililo onekana kumkera. Hata Mimi limenikera kwani ni unyonyaji.

Hofu YANGU NI kuwa kwakuwa umewatangazia, watajipanga kwa kukopa hadi mwisho wa kukopesheka, ili ukiwapunguzia wanaleta muongozo wa Hazina wa 1/3 ibaki kama sehemu ya mshahara. Japo sina hakika kama hii ni KWA watumishi wote au ni KWA walimu tu.

Tambua Rais wangu hawa watu wamesoma, ndio wanao tuibia KWA kutumia vema ELIMU zao NA kalamu.

Huo ni mtazamo wangu unge kaa kimya ili suala hili ulifanye kama ambushing yaani shitukizo, hapo wasingekuwa NA muda wa kujipanga.
 
Hili ni wazo zuri tu. Ila ingependeza sana kama Magufuli angeanza kuwa mfano kwa yeye mwenyewe kwanza. Kama alivyofanya wakati wa kuhakiki silaha. Mshahara wa Raisi wa Tanzania, kwa vile hana gharama zozote, basi milioni 2 unamtosha na chenji ikabakia! Magufuli onesha uzalendo wako hapo kwa kutetea wanyonge. Anza kupunguza mshahara wako kwanza!
 
akijipunguzia itakua poa kweli! maana hata malipo kwa marais, waziri mkuu na top wengine walio staafu itapungua

hapo 2020 kura yangu atapata
 
Ila bahati mbaya sheria ya kazi hairuhusu kupunguza mshahara wa mtumishi. Anachoweza fanya Pombe ni ku freeze mshahara mkubwa usipande kwa muda ataona unafaa. Hili iliwahi fanywa na serikali kwenye taasisi yake inaitwa CMSA. Hapo ilifikia secretari analipwa 4m. Serikali ikasema hamna kupanda tena mpaka itavyoamua vinginevyo.
 
Mshahara wa mtu ni swala la kikatiba na kisheria na bahati nzuri lina kinga nzuri sana kisheria. Sitegemei Rais avunje sheria.
Swala la mishahara mikubwa lina chimbuko lake ila limewekwa kama watu wanajilipa. Sivyo. Hakuna mtu anayejipangia maslahi yake. Mtu hupewa na mamlaka ya juu yake.
Pia wapo watu wametafutwa kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kujaza mapengo ya kiutaalam na uzoefu uliokuwa unahitajika. Huko walikotolewa walikuwa na mishahara yao mikubwa. Ili wakubali kuja ilibidi makubaliano maalum yafanyike. Watu hawa walioshawishiwa wakaacha kazi zao huko kuwaachisha bila muafaka ni kukaribisha kesi kwenye mahakama ndani na nje ya nchi.
Ukishampa mtu mkataba ni haki na huwezi kuivunja kwa jazba. Mtalipa watu bila kazi. Uangalifu unahitajika.
 
Aweke wazi mshahara wake na aanze kupunguza yeye na mawaziri wake. Kama ni mzalendo na mcha Mungu wa kweli. Hata Yesu alikuwa transparent na hakuficha kitu. Kununua soda na kukaa na makada wa CCM waliokwenda kumsalimia Mwanza bado ni kipande cha mchezo wa kuigiza.
 
Amesema atapunguza kodi kutoka 11 ya sasa hadi 10 mpaka 9,sasa najiuliza anatofauti gani na serikali zilizopita,maana yeye aliahidi maboresho makubwa ya maslahi ya watumishi wa umma,kweli inaonesha bado watumishi wa nchi hii hawajapata mkombozi anaejua shida na kero zao .
 
Hili ni wazo zuri tu. Ila ingependeza sana kama Magufuli angeanza kuwa mfano kwa yeye mwenyewe kwanza. Kama alivyofanya wakati wa kuhakiki silaha. Mshahara wa Raisi wa Tanzania, kwa vile hana gharama zozote, basi milioni 2 unamtosha na chenji ikabakia! Magufuli onesha uzalendo wako hapo kwa kutetea wanyonge. Anza kupunguza mshahara wako kwanza!
Kwani unaujua mshahara wa Rais ni shs. ngapi? Rais kuamua kupunguza mishahara mikubwa tayari keshaonyesha uzalendo na kutetea wanyonge. Ni aibu, dhuluma na wizi mtupu kwenye nchi yenye walalahoi wanaoshindia mlo mmoja kwa cku kama viboko, mfanyakazi wa serikali anapokea mshahara wa 40m kwa mwezi. Yaani anapata milioni na zaidi kwa siku! Waliopanga hiyo mishahara hawana uzalendo kabisa, ni majipu ya aina yake!
 
wakuongezea waongezewe ila asimpunguzie mtu ataleta mvutano. anasema hatakuwepo mtu wa kulipwa zaidi ya mil 15, labda aanze na mawaziri na makatibu wake then afuate wabunge ila asiguse misharaha ya wetu wenye taaluma zao
 
Hiyo haiwezekan taratibu za utumishi wa umma hazisemi hivo hta muundo wa utumishi haupo hivo,haiwezekan mim nipo TGTS I(2800000/=) kwa mwezi unipunguzie mpka TGTS D(730000/=) kwa mwezi.
mkuu hzo tgts duh... kunamtu akiona hzo no anataman alipwe hata 1/3ila haiwezekani.. kunamtu kazi yake ni kusain tu docoment analipwa milions of tsh...
 
Hiyo haiwezekan taratibu za utumishi wa umma hazisemi hivo hta muundo wa utumishi haupo hivo,haiwezekan mim nipo TGTS I(2800000/=) kwa mwezi unipunguzie mpka TGTS D(730000/=) kwa mwezi.
Mkuu wanabadilisha skeli za mshahara. Kutokana na mabadiliko hayo ndiyo mishahara itapangwa upya? Kuna madai kuwa idadi ya mifumo aka skeli ikapungua (sina uhakika) hivyo kada nyingi kutumia skeli zinazofanana
 
Nimemsikia Leo Rais wetu alipokuwa mwanza kuwa atawapunguzia mshahara watumishi wa umma walio na mshahara mikubwa.

Rais ametoa mfano kuwa kuna watumishi wanalipwa mil 40 kwa mwezi, jambo lililo onekana kumkera. Hata Mimi limenikera kwani ni unyonyaji.

Hofu YANGU NI kuwa kwakuwa umewatangazia, watajipanga kwa kukopa hadi mwisho wa kukopesheka, ili ukiwapunguzia wanaleta muongozo wa Hazina wa 1/3 ibaki kama sehemu ya mshahara. Japo sina hakika kama hii ni KWA watumishi wote au ni KWA walimu tu.

Tambua Rais wangu hawa watu wamesoma, ndio wanao tuibia KWA kutumia vema ELIMU zao NA kalamu.

Huo ni mtazamo wangu unge kaa kimya ili suala hili ulifanye kama ambushing yaani shitukizo, hapo wasingekuwa NA muda wa kujipanga.
Mshahara wa rais upo kwenye katiba wanasema ni marufuku kupunguzwa kipindi chote cha kua rais ,ata kwenye hazina kubaki kias cha mshahara wake basi inasema apewe yeye tu.Ili kupunguza mpaka wabunge wapitishe mswada wa mabadiliko ya katiba
 
wakuongezea waongezewe ila asimpunguzie mtu ataleta mvutano. anasema hatakuwepo mtu wa kulipwa zaidi ya mil 15, labda aanze na mawaziri na makatibu wake then afuate wabunge ila asiguse misharaha ya wetu wenye taaluma zao
Nikweli katika hili inabidi ajipange? Lasivyo watampunguza y#y@
 
Back
Top Bottom