Rais Magufuli: Kuna mtu amelipwa zaidi ya bilioni 20 kununulia sare za Polisi, akamatwe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema inasemekana mwishoni mwa mwaka uliopita kuna mtu alilipwa zaidi ya bilioni 20 ndani ya wiki moja kwa ajili ya kununulia mavazi ya polisi lakini hakuna hata vazi moja lililonunuliwa.

‘’Kuna minong’ono nong’ono kwamba hata mwishoni mwa mwaka jana kuna mtu amelipwa mabilioni ya shilingi kwa ajiri ya uniform za polisi lakini hakuna hata uniform moja iliyokabidhiwa ndani ya jeshi la polisi, nina hakika Waziri unafahamu, nina hakika IGP umeshalisikia na nina uhakika Meja Jenerali, Rwegasira umeshilisikia na wewe ni mwanasheria na Meja Jenerali, nina uhakika makamishna mmeshasikia. Nategemea siku moja hawa wahusika waliohusika na hilo watapelekwa mbele ya sheria’’. Rais alisema.

Rais amemwagiza Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu kuhakikisha huyo mtu anafikishwa mbele ya sheria ili pesa aliyochukua airudishe ikafanye shughuri zingine ndani ya Jeshi la Polisi.

Rais hakulitaja jina la mtu huyo lakini alisema haiwezekani kuna magari ya polisi 77 bandarini yamekosa ushuru wa bilioni 4 lakini kuna mtu alipatiwa ndani ya wiki moja mabilioni kwa ajili ya sare za polisi ambazo mpaka leo hakuna hata sare moja aliyoleta.

Ameliasa Jeshi la Polisi kupitia viongozi wake wa juu lijirekebishe haraka katika utendaji kwa sababu ni chombo muhimu sana katika taifa.

VIDEO.
 
Tar 14 mwezi May mwaka 2014, aliyekua Waziri wa mambo ya ndani Ndg.Mathias Chikawe alisema sare za jeshi ikiwa ni pamoja na viatu na kofia hununuliwa kwa zabuni kutoka nchini India. Sasa hizi ambazo JPM anasema zilitakiwa kushonwa hapa nchini ni zipi? Au wizara ilikua inadanganya zinashonwa India halafu wanapeleka kwa mafundi wa Mchikichini? Waliokua viongozi waandamizi wa jeshi la Polisi. Wapandishwe kizimbani isije kuwa rais hana taarifa sahihi

Borrowed this segment from FB.
 
Rais hajasema kama nguo zilitakiwa kushonwa hapa nchini bali amesema pesa iliyotolewa kwa ajiri ya kununulia nguo za polisi.

Kama ulivyosema, hiyo ilikuwa ni tenda lakini inaonekana ilikuwa ni tenda yenye magumashi.
 
Back
Top Bottom