G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,772
- 36,650
Utendaji kazi wa rais Magufuli kwa kweli unazua sintofahamu kubwa kwa wale waona mbali.
Rais Magufuli alianza na mahakama kwa kuwapa bilioni kadhaa huku akitoa angalizo linaloonyesha dhahiri ni kuingilia utendaji kazi wa mahakama. Nadhani tulishaandika humu hivyo haina haja kurudia.
Sasa ameligeukia bunge. Bunge linaonekana sii chochote wala lolote mbele ya serikali kiasi cha kuliacha lifanye mambo gizani huku matukio likuki ya rais Magufuli yakirushwa "live" zaidi yeye ndiye anayepanga nini kinatakiwa kupangwa na bunge.
Haya mambo yana hatari kubwa kama yataachwa hivihivi. Serikali haina miungu bali ina watu! Watu hao nao wanahitaji kusimamiwa na kushauriwa! Hiyo ndiyo kazi ya bunge! Watu hao wanahitaji kuonywa pale wanapokosea, hiyo ndiyo kazi ya mahakama. Watu hao wanahitaji kuwajibishwa, hiyo ndiyo kazi ya bunge!
Kuwaingilia mihimili mingine na kufanya uamuzi juu yao ni hatari kuwa hata siku serikali ikihitajika kuwajibishwa itazima hoja kibabe na mambo yakapita.
Tujifunze kwa Jakaya Kikwete! Mbali na kuwa alikuwa na mapungufu mengi aliweka wazi ili awajibishwe. Huo ndiyo uongozi bora! Hivi kama Kikwete angeamua kufanya hivi kama serikali hii leo mngemsema kwenye majukwaa? Si anasemwa baada ya kuacha mambo yawe wazi na yajulikane?
Tusijifanye kuwa sisi ni miungu! Sisi ni binadamu wenye nyama na damu!