MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Ziara hii itamfikisha katika nchi ya Ethiopia ambapo atakutana na viongozi wa serikali na Nchi za Afrika zaidi ya 50 katika kikao cha 26 cha Mkutano wa Umoja wa Afrika Mjini Addis Ababa, Ethiopia baadaye wiki hii.
Masuala ya amani na ulinzi yatakuwa katika ajenda ya juu hasa ikichukuliwa kile kinachoendelea katika nchi ya Burundi na pia mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika nchi za Burkina Faso na Somalia.
Viongozi wa serikali na nchi za Afrika wanatazamiwa kushiriki katika kongamano la 26 la Baraza Kuu la Umoja wa Afrika, litakalofanyika kati ya Januari 30 na 31 ambapo pia watamchagua Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Nchi za Afrika(AU).
Kwa mara nyingine tena viongozi wa Umoja wa Afrika(AU) wanatazamiwa kushinikiza kufanyika mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Licha ya pingamizi kutoka nchi 5 wanachama wa kudumu wa baraza hilo huko nyuma, viongozi wa AU wamesema kwa mara nyingine tena watashinikiza mageuzi katika chombo hicho, wakisisitiza kuwa muundo wa sasa wa baraza hilo hauakisi hali halisi ya siasa na uchumi wa dunia katika karne hii ya 21.
Kamati ya nchi 10 za Kiafrika juma lililopita ilifanya kikao na kuafikiana kuwa maslahi ya nchi Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndio miongoni mwa ajenda kuu za kikao cha Addis Ababa. Nchi hizo ni Algeria, Libya, Senegal, Sierra Leone, Namibia, Zambia, Uganda, Kenya, Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Viongozi hao wanatazamiwa kurejea mwito wao wa kutaka nchi mbili za Kiafrika ziwe wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa sasa nchi 5 wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN ni Marekani, China, Russia, Ufaransa na Uingereza.
Viongozi wa Kiafrika wanazituhumu nchi wanachama wa baraza hilo kuwa hazina demokrasia na kwamba zimekuwa zikitumia kura zao za veto kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Viongozi wa Umoja wa Afrika aidha wanapendekeza kuongezwa idadi ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoka 20 hadi 25.
Hii itakuwa ni nafasi kwa Rais Magufuli kufanya safari ya nje ya nchi kwa mara ya kwanza tokea achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.
Rais magufuli kwa sasa amekuwa gumzo katika majukwaa ya kimataifa kutokana na aina ya uongozi wake ambao wachambuzi wa kisiasa wanadai ni nadra kuupata kwa viongozi wan chi za Afrika ambapo rushwa, ufisadi, uvivu na ubadhirifu wa mali ya umma ni moja ya maisha ya viongozi wakuu wa nchi.