Rais Magufuli kama Rais Kagame?

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,267
21,443
Ni jambo la kutafakari juu ya urafiki kati ya Magufuli na Kagame. Binafsi nimependezwa sana na maendeleo ambayo Kagame ameiletea Rwanda, lakini niko macho sana na gharama ambayo Rwanda wamelipa ili kupata maendeleo hayo, hasa ukiangalia tuhuma nyingi na nyingine nzito dhidi ya uongozi wa Kagame nchini Rwanda.

Mambo wanayokabili wana harakati na wanasiasa wa upinzani nchini Rwanda, kutia ndani na wale wenye mtazamo tofauti na Kagame, yako wazi kwa kila mtu. Ni kama Kagame amekuwa akiongoza Rwanda kwa philosophy kwamba "the end justifies the means".

Labda kweli, maana kuna wakati Waziri Mkuu mmoja wa Uingereza aliwahi kusema kitu kama democracy is government of the people, by the people, for the people, but national development is most efficient when the people shut up and let their democratically elected (and appointed) leaders do their job.

Hivyo suala la kujiuliza ni kama Tanzania tunaelekea njia waliyoipitia Rwanda ili kupata maendeleo ya kujivunia waliyo nayo sasa. Ni maendeleo makubwa wameyapata, lakini gharama yake katika nyanja za demokrasia na haki za binadamu zimekuwa kubwa pia, kama tunavyotaarifiwa katika vyombo vya habari.

Sasa swali la kujiuliza ni kwamba, Magufuli naye anataka kujifunza kwa Kagame kwamba "the end justifies the means", kwamba the end we want ni Tanzania iliyoendelea sana, na ole wako utakaeonekana hauko nasi katika nia hiyo?

Wengine hata wanatoa mfano wa Libya; maendeleo yao chini ya Ghadafi mwenye kudhibiti democracy, na matokeo ya kumwondoa Ghadafi ili kuwa na demokrasia. Hivyo utaulizwa uchague; unataka demokrasi na umasikini na ufisadi au demokrasi iliyodhibitiwa na maendeleo bila ufisadi? Tunaambiwa Afrika tuna machaguo hayo mawili tu; kwamba Afrika Kusini ni mfano mzuri wa demokrasi na ufisadi unaokua kwa kasi. Sijui kama Botswana wamefanikiwa kuwa na demokrasi huru na maendeleo.

Labda kwa hali ya uozo Tanzania tuliyokuwa tumefikia, hicho ndicho tunahitaji, angalau kwa miaka kumi ijayo, unorthodox democracy justified by the end.
 
Ukizungumzia maendeleo ya Rwanda na Tanzania nakushangaa sana,Rwanda ina ukubwa wa kolometa za mraba sawa na mkoa wa Arusha! Hata angepewa mkulima wa tangawizi angeweza kuleta maendeleo Rwanda with good policy
Ni kweli kwa ukubwa wa Rwanda nategemea wangekua na maendeleo zaidi ya hapo walipo.
 
Ukizungumzia maendeleo ya Rwanda na Tanzania nakushangaa sana,Rwanda ina ukubwa wa kolometa za mraba sawa na mkoa wa Arusha! Hata angepewa mkulima wa tangawizi angeweza kuleta maendeleo Rwanda with good policy

Sidhani kama suala la msingi ni ukubwa wa nchi. Mbona Lesotho na Swaziland hatuoni kuwa zimeendelea sana kwa kuwa zina size ndogo? Na Egypt je, moja wapo ya nchi kubwa sana, iweje leo ni ya pili (kama sio ya kwanza) kwa ukubwa wa uchumi Afrika, pamoja na kuwa ni jangwa? Na unadhani DRC haijaendelea kwa sababu ya ukubwa wake?

Na China je - umeona kasi ya maendeleo yao pamoja na ukubwa wake? Ukweli ni kwamba kwa miundo mbinu hakuna taifa duniani linaifikia China.

Kumbuka kwamba ukubwa mara nyingi unakuwa ni kichocheo cha maendeleo pia - kwamba unakuwa na tax base kubwa. Ndio maana kuna argument kwamba kuungana kwa Afrika kutatupa nguvu kubwa ya soko.

In fact Kagame anasema kama yeye angekuwa Raisi wa Tanzania huenda tungekuwa nchi ya kwanza kwa maendeleo Afrika, zaidi sana ya Rwanda yake ndogo!

Katika suala la size bwana ukubwa wa pua hauhusiani na wingi wa kamasi
 
Ukizungumzia maendeleo ya Rwanda na Tanzania nakushangaa sana,Rwanda ina ukubwa wa kolometa za mraba sawa na mkoa wa Arusha! Hata angepewa mkulima wa tangawizi angeweza kuleta maendeleo Rwanda with good policy
hapo ndo ujinga wetu unaanzia,hivi ujerumani na urusi ipi nchi kubwa alafu nani anamzidi mwenzie kiuchumi na siasa bora?hizi ndio akili ndogo ambazo ni mtaji mkubwa wa ccm,wewe unasema kanchi kadogo je kwa rasilimali kiasi gani kuwa tosheleza wananchi wapale,wewe kwa bandari tu ya Dar unaendesha nchi hii lakini bado kunawatu wanaishi kwa mlo mmoja, Mungu katupeni madini,gas na kila thamani ya hapa duniani !!je tumefika wapi??
 
hapo ndo ujinga wetu unaanzia,hivi ujerumani na urusi ipi nchi kubwa alafu nani anamzidi mwenzie kiuchumi na siasa bora?hizi ndio akili ndogo ambazo ni mtaji mkubwa wa ccm,wewe unasema kanchi kadogo je kwa rasilimali kiasi gani kuwa tosheleza wananchi wapale,wewe kwa bandari tu ya Dar unaendesha nchi hii lakini bado Mungu katupeni madini,gas na kila thamani ya hapa duniani je tumefika wapi??

Mkuu, mara nyingine tukubali tu kwamba wachangiaji humu JF tuna namna na uwezo tofauti ya kuelewa mambo. Tuvumiliane. Hili ni jukwaa la wote.
 
usisahau kwa wakati huo Rwanda ni kati ya nchi chache duniani zenye sera nzuri zianazo vutia wawekezaji..sidhani kama Rwanda wananchi wake wana suffer na hizi double taxations
 
Ukizungumzia maendeleo ya Rwanda na Tanzania nakushangaa sana,Rwanda ina ukubwa wa kolometa za mraba sawa na mkoa wa Arusha! Hata angepewa mkulima wa tangawizi angeweza kuleta maendeleo Rwanda with good policy
umeongea pumba,hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maendeleo na ukubwa au udogo wa nchi
 
msamehe anayetetea mada ya maendeleo kwa hoja ya ukubwa wa nchi ya Rwanda badala ya uongozi bora. Ukubwa wa nchi ni faida kwa sababu ya rasilimali (ikiwemo rasilimali watu) soko la ndani, nguvu kazi n.k
 
Aliyesema Rwanda ni size ndogo sioni kama kakosea, tusijaribu kulinganisha Russia na Germany alafu ukasema mkubwa hampiti mdogo, huko ndiko kufikiria ndani ya box, kila nchi ina situation yake na matatizo yake, in this case Rwanda kwa popolation yao na ukizingatia eneo lao lilivyo dogo ni rahisi wao kuliendeleza kwa speed kubwa, wameconcetrate kila kitu kwenye eneo dogo, population ya Rwanda ni 11Million, ukilinganisha na size ya nchi yao hiyo ni manpower kubwa mno.

Rwanda wanajitahidi hata kusomesha watoto wao, nimekutana na warwanda kibao kwenye vyuo vikubwa duniani wengine wanalipiwa na serikali na wanategemea wamalize kusoma warudi nyumbani kuendeleza nchi yao, wengine wanalipiwa na vyuo vyenyewe. Ila in the end wanarudi home. Wakiendelea kukaza wanaweza grow very very fast tukawa tunawaonea juu kwa juu tu.

Na tutiseme Rwanda wana uchumi mzuri, nope, hawa jamaa wana GPD ndogo sana, sema tu wamejipanga kutumia vizuri kile walichonacho, ila kwenye uchumi tunawapiga fimbo mbali sana.
 
Ni jambo la kutafakari juu ya urafiki kati ya Magufuli na Kagame. Binafsi nimependezwa sana na maendeleo ambayo Kagame ameiletea Rwanda, lakini niko macho sana na gharama ambayo Rwanda wamelipa ili kupata maendeleo hayo, hasa ukiangalia tuhuma nyingi na nyingine nzito dhidi ya uongozi wa Kagame nchini Rwanda. Mambo wanayokabili wana harakati na wanasiasa wa upinzani nchini Rwanda , kutia ndani na wale wenye mtazamo tofauti na Kagame, yako wazi kwa kila mtu. Ni kama Kagame amekuwa akiongoza Rwanda kwa philosophy kwamba "the end justifies the means". Labda kweli, maana kuna wakati Waziri Mkuu mmoja wa Uingereza aliwahi kusema kitu kama democracy is government of the people, by the people, for the people, but national development is most efficient when the people shut up and let their democratically elected (and appointed) leaders do their job.

Hivyo suala la kujiuliza ni kama Tanzania tunaelekea njia waliyoipitia Rwanda ili kupata maendeleo ya kujivunia waliyo nayo sasa. Ni maendeleo makubwa wameyapata, lakini gharama yake katika nyanja za demokrasia na haki za binadamu zimekuwa kubwa pia, kama tunavyotaarifiwa katika vyombo vya habari.

Sasa swali la kujiuliza ni kwamba, Magufuli naye anataka kujifunza kwa Kagame kwamba "the end justifies the means", kwamba the end we want ni Tanzania iliyoendelea sana, na ole wako utakaeonekana hauko nasi katika nia hiyo?

Wengine hata wanatoa mfano wa Libya; maendeleo yao chini ya Ghadafi mwenye kudhibiti democracy, na matokeo ya kumwondoa Ghadafi ili kuwa na demokrasi. Hivyo utaulizwa uchague; unataka demokrasi na umasikini na ufisadi au demokrasi iliyodhibitiwa na maendeleo bila ufisadi? Tunaambiwa Afrika tuna machaguo hayo mawili tu; kwamba Afrika Kusini ni mfano mzuri wa demokrasi na ufisadi unaokua kwa kasi. Sijui kama Botswana wamefanikiwa kuwa na demokrasi huru na maendeleo.

Labda kwa hali ya uozo Tanzania tuliyokuwa tumefikia, hicho ndicho tunahitaji, angalau kwa miaka kumi ijayo, unorthodox democracy justified by the end.

Kwa nchi ilipofikia tunamuhitaji jpm now than ever,now way we can move from here without a leader like him..in 10 yrs to come,insee a new tz,belive me
 
kikubwa mkuu kuachana na nilichochangia hapo juu,Tanzania kwanza napinga kama ilishakuwa na full democracy kama ambavyo tunahubiriwa,kutembea popote kuishi popote ndani ya hii aridhi lakini ukaminywa hakizako za msingi kwahiyo kwa kipindi chote Tanzania imepitia katika mfumo wa udikteta ila ukiwa unapisha kulingana na mtawala mwenyewe..!!
kunamaswali machache naweza kukuuliza kuhusu Gadaf na Libya,hivi pale kati ya Gadafi nani alikuwa na maisha mazuri??je kama ungekuwa mwananchi wa Gadafi ungekubali miaka nenda rudi ushi maisha average wewe na kizazi chako waki mfalme nafamilia yake wanatanua kwenye kasri lililo jaa dhahabu??
Serikali yoyote iliokatika mfumo wa kidemokrasia kama SouthAfrica nirahisi sana kwa mambo yaliyo na ukakasi kuchukuliwa hatua na pengine kuhojiwa na kutolewa ufafanuzi na mamlaka husika..!!
 
  1. Pia Rwanda wameiba sana Congo na kuzitumia pesa za wizi kufanya maendeleo.
  2. Binafsi sijawahi kuona hata kiberiti au toothpick kutoka rwanda
 
Kiongozi anaweza kutimiza wajibu wake kwa kazi aliyoomba bila kuminya demokrasia na akatumia tuu sheria na katiba kudhibiti mambo na kila kitu kikaenda sawa.
Madhara ya udikteta pamoja na hata ulete maendeleo ni kuligawa taifa na wewe mwenyewe kuishia pabaya kama Gadaffi.
Mbona Jerry Rwalling wa Ghana aliendesha nchi kwa mkono wa chuma lakini akiheshimu katiba na utawala wa sheria na kufanikiwa sana na sasa anaishi kwa uhuru na raha hata super market au sokoni anaweza kwenda bila hofu?
Tunahitaji kiongozi mkali katika uwajibikaji,mbunifu, anayeshaurika lakini anayeheshimu katiba na utawala wa sheria ili hata akitoka tuendelee kumheshimu na kumpenda na kuwa mfano kwa anayenfuatia
 
Mkuu, Libya ya Ghadaffi kwa mwananchi wa kawaida ilikuwa hakuna mfano wake. Ghadafi alichokataa kabisa ni wananchi wake kujiingiza mambo ya siasa na kumwingilia, lakini upande wa huduma za jamii zilikuwa hakuna tena, labda nchi iliyoikaribia Libya ilikuwa ni Norway tu. Wananchi walipata huduma karibu zote bure; elimu, afya nk. Ghadafi alifikia hatua kwamba unapooa unapewa allowance na serkali ya kuanzia maisha!

Ila alitaka siasa au kuhoji sijui anaendeshaje nchi usiguse kabisa huko, wewe faidi huduma za bure za serikali na ukae kimya. Ilikuwa ukijifanya wewe mwanaharakati wakati wa Ghadafi utaishia pabaya na kuminywa sana. Wamarekani wakasema mwongo huyooo, anawanyima demokrasia - mambo yale ya Adamu na Hawa na Ibilisi dhidi ya Mwenyezi Mungu!
 
Mkuu, Libya ya Ghadaffi kwa mwananchi wa kawaida ilikuwa hakuna mfano wake. Ghadafi alichokataa kabisa ni wananchi wake kujiingiza mambo ya siasa na kumwingilia, lakini upande wa huduma za jamii zilikuwa hakuna tena, labda nchi iliyoikaribia Libya ilikuwa ni Norway tu. Wananchi walipata huduma karibu zote bure; elimu, afya nk. Ghadafi alifikia hatua kwamba unapooa unapewa allowance na serkali ya kuanzia maisha!

Ila alitaka siasa au kuhoji sijui anaendeshaje nchi usiguse kabisa huko, wewe faidi huduma za bure za serikali na ukae kimya. Ilikuwa ukijifanya wewe mwanaharakati wakati wa Ghadafi utaishia pabaya na kuminywa sana. Wamarekani wakasema mwongo huyooo, anawanyima demokrasia - mambo yale ya Adamu na Hawa n Ibilisi dhidi ya Mwenyezi Mungu!
ndohapo sasa mimi napo pishana na watawala wa namna hii,kwahiyo kwa wasomi wote pale libya hakuna aliekuwa anawzakustabilize haliya kiuchumi ya Libya zaidi ya Gaddafi na wanae??binafsi sitamani nchi ya namna hiyo
 
Kiongozi anaweza kutimiza wajibu wake kwa kazi aliyoomba bila kuminya demokrasia na akatumia tuu sheria na katiba kudhibiti mambo na kila kitu kikaenda sawa.
Madhara ya udikteta pamoja na hata ulete maendeleo ni kuligawa taifa na wewe mwenyewe kuishia pabaya kama Gadaffi.
Mbona Jerry Rwalling wa Ghana aliendesha nchi kwa mkono wa chuma lakini akiheshimu katiba na utawala wa sheria na kufanikiwa sana na sasa anaishi kwa uhuru na raha hata super market au sokoni anaweza kwenda bila hofu?
Tunahitaji kiongozi mkali katika uwajibikaji,mbunifu, anayeshaurika lakini anayeheshimu katiba na utawala wa sheria ili hata akitoka tuendelee kumheshimu na kumpenda na kuwa mfano kwa anayenfuatia

Nakuelewa, lakini huwezi kusema kwamba Rawlings aliiletea Ghana maendeleo ya ajabu sana, au kukomesha ufisadi.

Angalia nchi kama Ethiopia. Huyu waziri Mkuu wao aliyekufa (katika mazingira tatanishi), Meles Zenawi, alikuwa dikteta sana tu. Yaani akiamua kitu hakina mjadala, hata ndani ya chama chake. Lakini akaifanya Ethiopia ibadilike sana, na kuwa na uchumi unaokua kwa kasi kubwa sana duniani. Ila huku chini chini watu walikuwa wanalia kwa ubabe wa Zenawi. Wabunge alikuwa anawakata kauli Bungeni, anawaambia hamjui uchumi nyie, hivi ndivyo tutafanya, hata kama inflation inapanda, ili mradi tujaze wazalendo mapesa. Na alikuwa mkali mno kwa ufisadi. Aliwahi kumfunga Best Man wa harusi yake ambaye alikuwa pia kaimu wake wakiwa msituni miaka mitano jela kwa ufisadi!

Ethiopia ikawa inapiga hatua, miundo mbinu kubadilika kwa kasi, wananchi kuwezeshwa kwa kiasi kikubwa kiuchumi - lakini kile kinachoitwa demokrasia kikazorota sana Ethiopia. So, Zenawi alikuwa sahihi katika filosofia yake ya uongozi kwa sababu iliibadilisha na Ethiopia na kuleta maendeleo?

Yaani Raisi Magufuli huwa namuona kama photocopy ya Zenawi kwa msimamo yake ya ndani na nje ya nchi. Kama Magufuli, Zenawi hakubabaishwa na mataifa ya magharibi, na akawa rafiki mkubwa wa China kwa sababu aliwaamini sana - sawa kabisa na Magufuli. Mataifa ya magaharibi yalianza kumchukia Zenawi - ndio maana nakuwa na wasiwasi mara nyingine na nini kilimuua Zenawi!
 
ndohapo sasa mimi napo pishana na watawala wa namna hii,kwahiyo kwa wasomi wote pale libya hakuna aliekuwa anawzakustabilize haliya kiuchumi ya Libya zaidi ya Gaddafi na wanae??binafsi sitamani nchi ya namna hiyo

Hewaaa. Ndio maana nikasema, Afrika tunaambiwa tuna machaguo mawili; demokrasi ya kweli na umasikini na ufisadi; au demokrasi ya kuminywa na maendeleo bila ufisadi. Sasa unataka Raisi Magufuli akae upande upi katika kuongoza hii nchi?
 
  1. Pia Rwanda wameiba sana Congo na kuzitumia pesa za wizi kufanya maendeleo.
  2. Binafsi sijawahi kuona hata kiberiti au toothpick kutoka rwanda

Mmmh usiasahau Rwanda wanalima sana kahawa na chai, na pia pareto, mazao ya biashara ambayo Tanzania tumeyatupa. Wanauza nchi za Germany, USA na China. Unafikiri kwa nini Kagame anataka reli kupitia Tanzania? Sio kwa ajili ya Warwanda kusafiria kuja Dar, ni kwa ajili ya bidhaa. Pia usisahau wana sekta ya utalii ya hawa sokwe ambayo inawapa pesa nzuri tu na mara nyingine ikiongoza kwa pato la fedha za kigeni (Nyungwe National Park). Na sasa wanataka wawe hub ya mambo ya IT hapa Afrika.
 
Back
Top Bottom