Rais Magufuli kama kweli unatujali walalahoi tufungulie hili geti!

Barbarosa, ungewezaje wakati umri wako Dar es Salaam ni mfupi kuliko U RC wa Makonda
Inawezekana hata hajui kwamba mabasi ya Tanga/Iringa/Mbeya yalikuwa yanaanzia hapo na palikuwa wazi.
Palikuja fungwa baada ya ombaomba kujipatia makazi.
 
Inawezekana hata hajui kwamba mabasi ya Tanga/Iringa/Mbeya yalikuwa yanaanzia hapo na palikuwa wazi.
Palikuja fungwa baada ya ombaomba kujipatia makazi.

Hilo sijui, ila najua stendi ya Kisutu.
 
Inawezekana hata hajui kwamba mabasi ya Tanga/Iringa/Mbeya yalikuwa yanaanzia hapo na palikuwa wazi.
Palikuja fungwa baada ya ombaomba kujipatia makazi.
Uko sahihi mkuu hawa ni watoto wa enzi za kina Diamond Platnumz ukiwauliza ukumbi wa silent in au drive in hawawezi kujua, ila stand ya mabasi ya Tanga ilikuwa Kisutu.
 
Uko sahihi mkuu hawa ni watoto wa enzi za kina Diamond Platnumz ukiwauliza ukumbi wa silent in au drive in hawawezi kujua, ila stand ya mabasi ya Tanga ilikuwa Kisutu.

Drive inn najua, Mkapa aliwapa USA, nilishaangalia movies sana pale, ila hiyo silent sijui.
 
Sijawahi kuona hiyo bustani ikiwa wazi maisha yangu yote, kwanza hata viwanja vya gymkana vilikuwa kwa ajili yetu kupumzika, akapewa Muzungu achezee golf na kuweka uzio.

Sasa wewe wkt unakuja mjini si ulikuta stand ikiwa ubungo utajuaje haya mambo ya kitambo.
 
Sasa wewe wkt unakuja mjini si ulikuta stand ikiwa ubungo utajuaje haya mambo ya kitambo.

Nimezaliwa na kukulia hapa, hakuna kona siijui, kwanza naweza hata kuwa tour guide wa Watalii naijua mitaa yote hadi hata Historia ya sehemu nyingi tu za City.
 
Mageti yanawekwa makusudically hizo bustani zisitumike mithili ya Tahrir square!
 
Kunya hovyo ni tabia mbaya. Unatakiwa kujenga utamaduni wa kunya asubuhi na jioni nyumbani kwako.
 
Kunya hovyo ni tabia mbaya. Unatakiwa kujenga utamaduni wa kunya asubuhi na jioni nyumbani kwako.
Siyo kwamba nawatetea, watu wanaokunya pale sio kuwa wamependa bali kuna mazingira yanayoweza kukulazimisha, ukosefu wa huduma, tumbo kuchafuka ghafla, wasafiri, wagonjwa, watoto, ulevi nk.
 
We jamaa unaonekana ni Dar oyeee!!! Enz za mwalimu bustan ilikuwa wazi ile, tatizo lenu nyie madar oyeee mnajifanya kila kitu mnakijua wakati hamjui
 
Nimezaliwa na kukulia hapa, hakuna kona siijui, kwanza naweza hata kuwa tour guide wa Watalii naijua mitaa yote hadi hata Historia ya sehemu nyingi tu za City.
Kukulia sehemu siyo garantii ya kujua kila kitu, watu wamezaliwa Tanzania lkn mzungu mtalii anaijua mbuga ya Serengeti kuliko mtanzania.
 
Un
Unaweza usieleweke lakini umeongea kitu very logical.Tupo pamoja Mkuu
 
Pole fuatilia historia yake, wengine tumecheza sana pale, miaka ya 80/90 kwa pembeni kilikuwepo na kituo cha mabasi ya kwenda nyada za juu kusini, Mbeya, Iringa, Sumbawanga, Njombe nk

Ilanga moto, Kiswele, Ruvuma tours line, Twiga, Tawaqal, Comfort, Upendo, Embakas..n.k
 
Kukulia sehemu siyo garantii ya kujua kila kitu, watu wamezaliwa Tanzania lkn mzungu mtalii anaijua mbuga ya Serengeti kuliko mtanzania.

Mimi ni hobby yangu, kwanza hata majengo ya Kihistoria karibia yote nilikuwa nayajua na historia yake kabla hawajaanza kuyavunja na kujenga ujinga wa skyscraper, huwa najisikia raha mtu akiniuliza mtaa fulani ulipo au jengo au ofisi ya Serikali ilipo na kumuelekeza.
 
Na watufungulie Barack Obama avenue tupite mbele ya Ikulu, wafunge usiku.
 
Hii nchi ina matatizo makubwa sana, wakati JPM akisisitiza watu kuchapa kazi wengine wanaomba lango la mnazi moja liwe wazi ili wakalishe makalio yao 24/7.

Mtoa mada unachuki na Nyerere hadi unakera huku ukijifanya unampenda Magufuli na Mlumumba kindakindaki kumbe mnafiki mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…