Rais Magufuli: Kama balozi atakaa miezi sita bila kuleta ripoti ya alichokifanya ntamtumbua

Hizi lugha zina ukakasi kwelikweli, bora angekuwa anatengua anamwambia mwenyewe inatosha. Naiona kama haiku sawa hii.
hiyo ndio baabkubwa kusudi iwe fundisho kwa viongozi wengne legelege...mambo ya kubebana yamepitwa na wakati!.
Kiongozi anatakiwa ajue kabisa akiwa mzembe siku anatumbuliwa inakuwa aibu hadi ukweni kudadeki.
 
Awatumbue tu maana hawana jipya na angeanza na Dr wa mihogo
 
Inawezekana na madc kawapa hayo masharti ndiyo maana wanalazimishaga kuwaweka watu ndani masaa 48 ili wapate cha kusema kwa mteule wao
 
TZ ndio nchi pekee ambayo watu wake wanatamani madaraka kwa ajili ya kula bata au kuweka title ya wadhifa na sii kulitumikia taifa na wananchi au kutimiza majukumu ya nyadhifa zao. KONGOLE za dhati kwa harakati za Raisi wetu ktk hili Dr. JPM
 
Inaonekana mambo ya nje kuna networks nyingi za wajanja wapigaji. Mindset ni kama bado haijabadilika.
Na hii hutoakana na fikra kuwa TZ bado ni taifa changa hivyo maeneo km hayo huwa hata viongoz wengi hawayafuatilii utendaji wake na pia ilizoeleka kuwa ni mopja ya sekta ambayo nafasi zilikuwa zikitolewa km shukran kwa wahusika waliozipata nafasi hizo. Wakati ni moja ya maeneo mazuri sana ya kuwezesha utangazwaji mzuri wa TZ ktk kila nyanja + fursa zilizopo
 
Hapo ndipo wakenya wanapotuzidi, kuelewa ni sekta ipi ipewe kipaumbele na kwa wakati gani.

Walifikia hatua ya kuiambia dunia kwamba mlima kilimanjaro upo kwao, na wakati huo sisi tulikuwa tumelala tu.
 
Hapo ndipo wakenya wanapotuzidi, kuelewa ni sekta ipi ipewe kipaumbele na kwa wakati gani.

Walifikia hatua ya kuiambia dunia kwamba mlima kilimanjaro upo kwao, na wakati huo sisi tulikuwa tumelala tu.
Mwaka 2011 ktk maadhimisho ya siku ya kuzaliwa malkia wa Uingereza, wakenya walisemekana kuwa ndio wenye Lugha ya kiswahili na walitakiwa kutoa speech ktk lugha ya kiswahili. Ukweli ni kwamba wao hawapo vizuri hivyo walimkodi mtanzania MRISHO MPOTO ili akatoe speech ile mbele ya malkia naye akafanya hivyo, sasa km serikali ya awamu ile haikulipigia kelele hilo ingewezaje kupigia kelele suala la mlima Kilimanjaro kuwa ni wa Kenya?

Ila kwa kipindi hiki tarajia kuona watu wakiwajibika ipasavyo, na masuala km hayo ya mlima Kilimanjaro pamoja na Kiswahili hayawez tokea tena.
 
MRISHO MPOTO ili akatoe speech ile mbele ya malkia naye akafanya hivyo,
MPOTO aliihujumu Jamhuri ya Muungano Tanzania kitamaduni, kidesturi,kisiasa na kidiplomasia kama kweli tukio hili lilitokea na yeye alijua kabisa kuwa amekodiwa kwa malengo hayo ya wakenya na UK. Kwa kitendo hicho, Mpoto anatakiwa kuomba radhi Jamhuri ya Muungano Tanzania kabla rungu halijamshukia. Ule ulikuwa utovu wa uzalendo wa hali ya juu kabisa.
 
Baada ya tukio lile alihojiwa na yeye mwenyewe alitupa lawama kwa viongoz wa taifa,
 
Baada ya tukio lile alihojiwa na yeye mwenyewe alitupa lawama kwa viongoz wa taifa,
Asante sana mkuu kwa taarifa. Hata hivyo naomba link ya mahojiano hayo ya MPOTO akielekeza lawama kwa taifa. Natanguliza shukrani.
 
Asante sana mkuu kwa taarifa. Hata hivyo naomba link ya mahojiano hayo ya MPOTO akielekeza lawama kwa taifa. Natanguliza shukrani.
Aisee, utanisamehe kwa suala la link, ila ilikuwa TBC1 ktk kipindi chao cha asubuhi ambacho huruka mida ya saa 12 hivi. Ilikuwa mwaka 2011 nami nilicheki kipindi live
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…