Rais Magufuli: Kama balozi atakaa miezi sita bila kuleta ripoti ya alichokifanya ntamtumbua

RPC ni mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, mwenyekiti wake ni RC na sio DC.

DC ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya, mjumbe wake ni OCD na wengine level ya wilaya.

Usichanganye madesa
Kama RPC ni wa mkoa wa kipolisi basi boss wake anakuwa DC wa wilaya. Mfano RPC kinondoni anakuwa chini ya DC kinondoni
 
Tukiondoa 'fine details (print)' hili ni eneo moja kati ya machache ninayoweza kumuunga mkono Rais Magufuli.

Utendaji kazi wa lelemama ni tatizo kubwa, na ndilo linalochangia kwa kiasi kikubwa nchi hii isiende mbele.

Kuna wizara nyingi tu zinazohitaji kutikiswa na kukorogwa ziache kufanya kazi kwa mazoea.

Natamani mtikiso huo auhamishie wizara ya elimu na wizara ya kilimo. Hawa wanahitaji hata kuwa wanatandikwa viboko kabisa kama wanashindwa kutimiza malengo waliyowekewa.
 
hawa wasaidizi wa Rais wamezidi uzembe. Ni aibu kubwa kutumbuliwa kwa kosa la kushindwa kujibu barua. Hizo PhD za huko Nyingi zitakuwa za mashaka.
Elimu Siyo Cheti Ni Ujuzi
Maana Hao PhD Oops Kama Ngumbaro
 
Naona kamtaja balozi kairuki jinsi alivyoshindwa kujibu barua 20 za balozi wa china.
Nahisi huyu balozi hana maisha huko china
Punguza kuropoka uwe unasoma kwa umakini...........

"Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwahi kuandika barua 24 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, lakini zilijibiwa 2 tu. Kuna mambo mengi ya hovyo yanayofanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje."-
 
Waziri Mahiga nae angemchomoa tu.. Sbb huyo sio mtendaji bali ni mtu wa lugha nzuri tu za kidiplomasia.. But ktk wizara hawezi kwenda na speed ya Mh. JPM, Mahiga ni mtu wa maneno mazuri mazuri but utendaji mzuri sahau..!! Better waziri mwingine wa Foreign ministry achaguliwe ASAP..


Reporting from Dubai.. On transit
 
Waziri Mahiga nae angemchomoa tu.. Sbb huyo sio mtendaji bali ni mtu wa lugha nzuri tu za kidiplomasia.. But ktk wizara hawezi kwenda na speed ya Mh. JPM, Mahiga ni mtu wa maneno mazuri mazuri but utendaji mzuri sahau..!! Better waziri mwingine wa Foreign ministry achaguliwe ASAP..


Reporting from Dubai.. On transit
Mahiga kapooza kweli yani hii Wizara ni muhimu ila imepoa yani kah inahtaji mabadiliko maana ni Wizara muhimu sana kwa nchi yetu
 
“Nataka ukafanye kazi, nimesema mara nyingi na hapa nataka kurudia, wizara hii ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hainifurahishi, nataka ukaisimamie vizuri, ukiona kuna mkurugenzi hafai mtoe”

Nadhani Waziri kazi yake ya kwanza ni kuandaa sera rasmi ya mambo ya nje. Kwa tanzania sera yetu ilenge (1) kujenga mahusiano ya kiuchumi (WIN-WIN) INVESTMENTS (2) kuhamishia kwetu teknolojia na knowledge ili tuweze kuibua viwanda na (3) kujenga mahusiano ya kimkakati ya kimatifa na kikanda. - BALOZI ZA KISIASA TUFUTILIE MBALI

Kule ambako tutaona hakuna tija tusiishie kulalamika kuwa hawafanyi kazi, tusipeleke kabisa mabalozi, au tuwarudishe nyumbani waliopo huko. Lazima tujitambue kuwa sisi ni taifa lililorudishwa nyuma na serikali za CCM hivyo lazima twende na akili mpya.
 
Mahiga kapooza kweli yani hii Wizara ni muhimu ila imepoa yani kah inahtaji mabadiliko maana ni Wizara muhimu sana kwa nchi yetu
mkuu unataka mahiga awe mchangamfu kama ametiwa ndimu ya mchina?
yani arukeruke kama bisi motoni au awe mapepe kama joti?
 
Naona kamtaja balozi kairuki jinsi alivyoshindwa kujibu barua 20 za balozi wa china.
Nahisi huyu balozi hana maisha huko china
Baloz aliandika barua zaidi ya 20 wizaran bila kupewa majibu!!
"Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwahi kuandika barua 24 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, lakini zilijibiwa 2 tu. Kuna mambo mengi ya hovyo yanayofanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje."-
 
Anaanza kujutia matendo yake angali bado yuko ofisini na akistaafu ndio atajuta zaidi.

Binafsi hili neno huwa silipendi hata kuliandika humu JF na kama niliwahi, basi ni mara chache sana maana sipendi hata kulitamka.

Yeye leo hii ndio anaona ubaya wa hili neno? Hapa ni wazi huenda amegundua kuna wengi kawaonea na ndio maana hata hilo neno sasa anaanza kulikataa.

Apandacho mtu, ndicho avunacho.
Hata mimi nasikiaga kinyaa kbs, mara ya kwanza alivyohotubia bunge alivyolisema tu nikazima tivii
 
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli atamuapisha Dkt. Damas Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ikulu Jijini DSM leo tarehe 29 Sept, 2018 kuanzia saa 4:15 asubuhi hii.

Tazama TBC1 na tovuti rasmi ya Ikulu

UPDATES;

Rais Dk John Pombe Magufuli, amemuapisha Dk Damas Ndumbaro, kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
View attachment 881377
Dk Ndumbaro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Susan Kolimba ambaye uteuzi wake ulitengukiwa.

Baada ya kuapisha, rais Magufuli katoa neno.

"Nilitaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Prof Adolf Mkenda na yeye nimuondoe kabisa, lakini anabahati kukawa na nafasi iliyowazi Wizara ya Maliasili na Utalii nikampeleka huko. Naamini atakuwa amejifunza na atafanya kazi nzuri."

"Mabalozi sasa watakuwa wanaleta ripoti, kwamba kwa kipindi nilichoteuliwa nimeifanyia Tanzania A, B, C. Kama mtu miezi sita atakuwa hajafanya chochote, ameenda tu kunywa wine, ajiandae kurudi.

"Siku hizi sipendi kutumbua, na hata sipendi kulisikia hilo neno, lakini utafanyaje? Unamteua mtu unaona hafanyi kitu, wengine wanahangaika yeye yupo tu. Ndio maana niliamua kumtoa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje."

"Lengo letu ni kuipeleka Nchi mbele, Wapo watendaji wengine wazuri pale Foreign lakini barua hazijibiwi, Balozi wa China aliwahi kuandika barua 24 zilijibiwa 2 Tu"

"Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwahi kuandika barua 24 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, lakini zilijibiwa 2 tu. Kuna mambo mengi ya hovyo yanayofanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje."-

=====
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 29 Septemba, 2018 amemuapisha Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Ndumbaro imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai na viongozi mbalimbali.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Dkt. Ndumbaro amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumteua kushika wadhifa huo na ameahidi kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa hasa kwa kuzingatia mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza kulinda heshima ya Tanzania kwa mataifa mbalimbali duniani, na kuitekeleza vizuri zaidi diplomasia ya uchumi.

Pamoja na kumpongeza, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Ndumbaro kuhakikisha dosari za utendaji usioridhisha katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zinarekebishwa ikiwemo kuwaondoa watendaji ambao wameonekana kuwa kikwazo cha ufanisi wa wizara hiyo.

“Nataka ukafanye kazi, nimesema mara nyingi na hapa nataka kurudia, wizara hii ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hainifurahishi, nataka ukaisimamie vizuri, ukiona kuna mkurugenzi hafai mtoe” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Ndumbaro kuhakikisha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali wanafanya kazi kwa manufaa ya Tanzania na wanatoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao ili kujua kila Balozi kafanya nini, na kama anastahili kuendelea kuiwakilisha Tanzania katika nchi husika.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema amefanya mabadiliko ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutokana na kutoridhishwa kwake na mwenendo wa wizara hiyo na hivyo amemtaka aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda ambaye amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha wizara hiyo inaongeza mapato yatokanayo na maliasili zilizopo na vivutio vingi vya utalii vilivyopo hapa nchini.

“Prof. Mkenda uzuri ni kwamba wewe ni mchumi mzuri, natarajia kule Maliasili na Utalii utafanya mabadiliko yatakayoisaidia nchi kupata mapato zaidi, asilimia 32.5 ya nchi yetu ni maeneo ya hifadhi, na nchi yetu ni ya pili kwa vivutio vingi vya utalii duniani, mwaka huu tutaongeza hifadhi nyingine 5, kwa hiyo kahakikishe tunapata mapato zaidi” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf ambaye amemaliza kipindi chake cha miaka 3.

Akizungumza baada ya kuagana Mhe. Elshawaf amesema uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Misri ni imara, na ameshukuru kwa ushirikiano mzuri alioupata kutoka Serikalini katika kipindi chote alichoiwakilisha nchi hiyo.

Mhe. Elshawaf amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi mzuri na ameahidi kufisha salamu za Mhe. Rais Magufuli kwa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah el-Sisi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

29 Septemba, 2018

Mabalozi wanapewa pesa za kufanya kazi huko ktk balozi? Wanao watendaji weledi? Nadhani hotuba nyingine ni furahisha baraza tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom