Rais Magufuli, Je huoni na wewe Utumbuliwe?

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Magufuli ameshateua Watendaji kadhaa na Kuwatumbua ndani ya Mwezi, Na hii ilitokana na kufanya kosa fulani, Mambo ambayo hukuyatarajia au kwa Kile anachokiita Kutokwenda direction anayoitaka. Na kwa Criteria hiyo mimi sikulaumu. Ila standard yako ni nzuri sana kama Wananchi wakiitumia pia hasa kwako.

Labda na mimi Nikuulize?

1) Mh. Magufuli, wananchi hawakutarajia wewe kukwapua pesa 2.7 bill hazina na Kuwapa wabunge wa CCM wagawane, Je wakutumbulie mbali? Yes or No!

2) Mh. Magufuli Wananchi hawakutarajia Kuwafukuzia watoto wao 7000 mitaani bila nauli wala chakula kwa makosa yasio yao, na kisha kuwatukana Villaza Je wakutumbulie Mbali? Yes or No?

3) Mh. Magufuli wananchi hawakutarajia wewe kuchukua fedha za humanitarian relief zilizotolewa kwa ajili ya wananchi wahanga wa Bukoba na kuzitumia fedha hizo kwa ukarabati wa majengo na barabara kisha kuwapa wao majani ya chai, na biskuti moja! Je wakutumbulie mbali Yes or No?

4) Mh. Magufuli wananchi hawakutarajia serikali yako kumlinda mtu kwa Polisi akiwa anafanya jinai kama Ulivyofanya kumlinda lipumba akivunja ofisi za CUF na Kuingia kwa jinai, Je wakutumbulie mbali,Yes or No?

5) Mh. Magufuli wananchi walitajia viwanda na ajira Lakini hata kama basic ajira kama za waalimu wanaambiwa ati waalimu wa Sanaa wametosha Je Wakutumbulie Mbali Yes or No?

6) Mh. Magufuli Uliahidi kujenga Viwanda ili vitoe ajira badala yake Serikali yako inaweka takwimu inayojumuisha Kinu cha Mchi na Mbuzi za Kukunia Nazi Kama Viwanda ili kuwahadaa, Je wakutumbulie mbali? Yes or No?

7) Mh. Magufuli wananchi hawakutarajia katika miaka ya baada ya 2000 wangekaa foleni kununua sukari kama ilipokuwa wakati wa Vita ya Kagera Duka, aka la Kaya, Wewe kwa sababu unazojua mwenyewe ukawafikisha huko, Je wakutumbulie Mbali? Yes or No?

8) Umenyamazia Ufisadi Kama wa IPTL, UDA na Lugumi ukaizima kiaina kwa kumtumia stooge wako Naibu speaker Tulia, Je kwanini wananchi wasikutumbulie mbali?

9) Wanafunzi walitarajia kupata mikopo wanapata ya Manati, Waalimu wahitimu wanaambiwa ati waalimu wa sanaa, wametosha, hakuna ajira, Je Wananchi wakutumbue au wasikutumbue? Yes or No?

10) Wamama wajawazito walitarajia kupata dawa lakini sasa hata gloves inabidi wanunue wenyewe huku wewe ukikwapua fedha keshi na kununua ndege kiserikali na kuwapa ATC, Je wananchi Wakutumbulie mbali, Yes or No?

11) Wewe Uliyekuwa ukipigia makofi wahuni, wapambe wako wakisema Lowassa kajinyea, Lowassa mfu mtarajiwa, Hakuna budget ya mazishi ikulu etc Wanachi hawakutarajia waone Unafiki wako wa kumweka mtu ndani kwa shinikizo la ajabu ati kwa kuota utakufa, Je wananchi wakutumbue wasikutumbue? Yes or No?

12) Wewe unayezunguka nchi nzima mpaka majmbo yaliyokukataa kama Dar na Arusha na Pemba ukisambaza siasa ya hadaa uwongo na Maji taka (mifano ni mingi eg wapinzani walifunga midomo kupinga mahakama ya mafisadi isianzishwe b) Jecha apewe tuzo c)Malipo ya Matibabu ya Seif yasisainiwe!)

Wewe unayetumia Ikulu kufanyia vikao vya CCM kwa kile unachoita kuimarisha chama, Ikulu!, Na kudanganya Ikulu chama chochote kinaweza kufanya mkutano. Unapata wapi guts za kuzuia wengine kuimarisha vyama hata chini ya mwembe au mtembo. Je Kwa unafiki na uzandiki wako huu Wananchi wakutumbulie mbali? Yes or No?

Kuna Mengi Mh Magufuli ya Kukutumbua, Nahisi Utakalolisema, Utasema upewe Muda wewe ulishampa Nani Muda, Utasema una maelezo ya kudorora kwa uchumi wewe ulisha entertain excuses za wangapi? Utasema uhurumiwe mzigo wa kazi ni Mkubwa wewe ulishawahurumia wazembe wangapi, Utasema jamani mniamini, wewe ulishaamini nani?
 
Mganga?

Kwenye masuala yasiyo serious Mganga asijigange tu

Ila kwa masuala yenye maslahi kwa taifa, Tubadilisheni kanuni hizi ni misemo ya kale


KATIBA MPYA?

"Hapana, Hilo ni wazo la Upinzani!"
 
Kaka una hasira.Omba Mungu wale jamaa zake wasikukute.Hujaongezea tu na zile Barabara za chini ya standard, bado ile Bilioni nane iliyonunua kivuko hewa, bado zile nyumba za Serikali. Duh list ni ndefu.

Najua utatukanwa sana lakini upinde umenipata
 
Ni angalabu keyboard inaweza kumtumbua mtu....na kwa sheria hizi za uhalifu wa kimtandao labda itumike keyboard ya mwendokasi!
 
Kazi mnayo endeleeni kuwasafisha mpaka wasafishike maana mliwachafua wenyewe
 
Kumbe kibao cha kukunia Nazi,mwichi na kinu vilihesabiwa katika idadi ya viwanda vilivyojengwa awamu ya tano?

Mleta mada umeniamsha akili!!
 
Sasa hivi natengeneza tochi za kupima kiongozi aliyechaguliwa/atakayechaguliwa kimakosa bila sifa sitahiki. Tochi hizi zitakuwa mithili ya zile za polisi za kupima mwendokasi. Hizi ntakazotengeneza ntaziita KIONGOZI MAKOSANOMETER
 
Yesses to all questions:ila ubavu huo mnao?
Uko sahihi,kwa katiba hii hesabuni maumivu!
Huo ndio ukweli,japo mchungu!
Msemo wangu ni huu ipo siku Madictator wa Afrika itabidi Vipolisi wao viwameze kuwalinda maana Upumbavu wa kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya Mtu mmoja hauna ushindi na wanajua, Upumbavu wa kushindana na Serikali kwa ajili ya Mtu mmoja siku zote tutaumia. Lakini Tunge apply falsafa ga Yesu kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe. Hata mtu mmoja tu Makini anaweza Kumbebesha Dictator yoyote Mzigo wake na Africa isingechukua mwaka wangeisha wote na wanaowafuata wafuate Washike adabu na Kutii Utawala wa Sheria na Katiba au wafuate mkumbo! Nao wabebe mzigo wao, Africa Ingenyooka tu!
 
Back
Top Bottom