Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Katika hali ambayo inaashilia kwamba utawala huu kama uliopita, bado unadhani kuendelea kuipamba Dar ndo njia ya kuinua taswira ya nchi. Magufuli naye kaingia ktk mtego huu. Utawala uliopita umekopa pesa nyingi kwa ajili ya Dar, miradi mikubwa ya barabara, ujenzi wa hospitali na vyuo kwa ajili ya Dar.
Kwa ujumla siyo vizuri na hata salama kutumia sehemu kubwa ya kipato cha nchi kinachozalishwa mikoani kwa ajili ya kuipamba Dar. haya ndo yaliyotokea Central africa, ikajikuta ni nchi yenye jiji moja tu la maana. Matokeo yake yanalazimisha uhamiaji wa nguvu sana, watu kuzidi kuingia Dar kwa wingi sana kwa ajili tu ya kufuata huduma zinazorundikwa Dar badala ya kuzitawanya nchini kote.Wabunge wa Dar walishajiaminisha kwamba Dar ndo inaingiza kipato kikubwa cha nchi, kitu ambacho ni uongo. Utalii, madini, kilimo, vyote ni nje ya Dar.
Maoni yangu kwa Rais Maufuli. Tafadhari tawanya utajili wa nchi. Tawanya miradi nchini kote. Jenga barabara na skyover nchini kote. Jenga hospitali za rufaa nchini kote, tembelea akina mama wanaolala chini nchini kote. Sihitaji kuja Dar kwa ajili tu ya MRI machine au CTscan.