Deo Shy
Member
- Oct 18, 2016
- 98
- 300
Hii nalo ni kituko cha dunia. Majina ya wagombea ubunge afrika mashariki jana yamevujishwa na sekretariate inayoket leo kwa ajili ya kufanya usahili kwa wagombea wote 425. Majina yalivujishwa jana yamepunguzwa kutoka 425 mpaka 18. Hili linatendeka wakati leo tarehe 28.03.2017 ndio siku ya kufanya usahili. Sasa mmetuleta hapa Dodoma kufanya nini kama mlikuwa na majina yenu mfukoni...
Mbaya zaidi hao waliopitishwa wajumbe hao wa sekretariate wanasema ndio Mzee kawapendekeza. Kitu ambacho sio kweli. Magufuli hana mgombea na yuko very fair.... Ingawa inasemekana wajumbe hao waliopitishwa walitembeza mkwanja kwa wajumbe hao wa sekretariate tokea mchakato ulivyoanza Lumumba!...
Tumehuzunishwa sana na hii hali. Hatukutegemea kama watu wangeendeleza mchezo wa ovyo kama huu.
Tafadhali sana Rais Magufuli, Comrade Mangula na Kinana ingilieni hili suala kati. Majina yenu yanatumika huku vibaya!