Rais Magufuli huwa anamaanisha nini anaposema anachomekea?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,260
Nimemsikia mara kadhaa mheshimiwa Rais anapohutubia anasema "nachomekea tu" Miongoni mwa mara nilizomsikia ni pamoja na wakati wa mkutano wa wakuu wa Afrika Mashariki ambapo baada ya kuongea kiingereza chake akasema "in swahili we say nachomea tu" Leo pia baada ya kuwapisha wakuu wa mkoa ameongea nao na kusema tena "nachomekea" Mara nyingi anasema anachomekea. Maana yake nini?
 
Kuchomekea ni kuongea kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba. Kingereza huwa wanasema "by the way", yaani sikutaka kulizungumzia hili suala lakini nimeona ngoja niliongelee. Lakini ni katika kujifanya mswahili wa pwani, yaani anafikisha ujumbe kwa mtu fulani lakini anakuwa anataka aonekane kana kwamba hakuwa na lengo baya, lakini ujumbe uliokusudiwa unakuwa tayari umeshafika kwa mlengwa.
 
Hili neno lilikuwa maarufu sana kipindi cha nyuma kabla ya 'Mambo poa halijawa maarufu'.Maana yake ni kuongelea suala ambalo liko nje ya maada. Mtaani ndugu raisi tungemuita mzee wa kuchomekea.
 
Nimemsikia mara kadhaa mheshimiwa Rais anapohutubia anasema "nachomekea tu" Miongoni mwa mara nilizomsikia ni pamoja na wakati wa mkutano wa wakuu wa Afrika Mashariki ambapo baada ya kuongea kiingereza chake akasema "in swahili we say nachomea tu" Leo pia baada ya kuwapisha wakuu wa mkoa ameongea nao na kusema tena "nachomekea" Mara nyingi anasema anachomekea. Maana yake nini?
Ustaadh Mwinyi, hujui maana ya kuchomekea? Sisi tusio na MABUSHA tunajua maana yake! Ni kuchomekea tu
 
Kuchomekea ni kuongea kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba. Kingereza huwa wanasema "by the way", yaani sikutaka kulizungumzia hili suala lakini nimeona ngoja niliongelee. Lakini ni katika kujifanya mswahili wa pwani, yaani anafikisha ujumbe kwa mtu fulani lakini anakuwa anataka aonekane kana kwamba hakuwa na lengo baya, lakini ujumbe uliokusudiwa unakuwa tayari umeshafika kwa mlengwa.
Pole mkuu jina lako kwenye udc na u rc halipo
 
umekosa kabisa jibu ukaona uulize hku tena kwa kuanzisha thread??!! Au unajibu lako?nmeona nchomekee kidogo
 
Phillipo Bukililo ina maana wewe ni mtaalamu wa kiswahili?
Hayo ni maoni yangu. Kuchomekea maana yake ni kuingiza suala ambalo halihusiani moja kwa moja na mada au hotuba inayokuwa ikitolewa katika muda fulani. By the way, yaani ni kama vile mtu anakuwa amekumbuka kitu fulani hivyo anaamua kukiongelea hata kama hakihusiani na kile kinachoendelea kuongelewa. Magufuli hutumia msemo huo kwa makusudi kabisa, anakuwa amepnga kuongelea lakini anajifanya mswahili, eti ameongea kwa bahati mbaya!, lakini ujumbe unakuwa umefika kwa mlengwa.
 
Unajuwaje kama anafanya makusudi kwanini wewe unaamua kuusemea moyo wa rais magu?
 
Unapoongea na maneno yako yakasomeka dunia nzima, jitahidi kutumia akili za kawaida, wakati mwingine weka masuala ya siasa pembeni. Unaweza kudharaulika kwa watu wengi, kupitia sentensi moja tu unayoipost hapa jamii forum.
 
Unaidharau wewe,ebu jibu swali ni kwanini umeamua kuusemea moyo wa mh rais?we ninani kwake?
 
Back
Top Bottom