MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,500
Uchaguzi umeenda uzuri tu na mambo yamekuendea poaa kabisa umeukwaa uheshimiwa sana. Sasa! Ninajambo nakuuliza kutokana na maelezo yako katika kujielezea kwa wananchi kuwa utawatendea haki haswa wananchi wa chini ambao ndio wanateseka na hali ngumu ya maisha.
Je.. Ni kweli umedhamiria kutawala kihaki ukiwa ni amiri na jemedari mkuu kutawala nchi hii tanzania iliyounganisha nchi mbili yani tanganyika na zanzibar katika hali tuliyonayo hivi sasa?
Huko tanganyika mambo yamekunyookea ni poa na unaendesha nchi tanganyika kiulaini tu. Sasa jemedari wewe tukuelewe ni wa tanganyika tuuu au tanzania?????? Mbona hujitoi muhanga kama unavojitoa kwa mafisadi wanaoitafuna tanganyika ??? Ukishughulika na ufisadi wa kisiasa unaoendelea upande wa pili na wewe sio ukiwa.. Bali ni jemedari mkuu wa upande huooo???
Ufisadi wa jecha hivi huusikii au umeamua kuuchuna tu liwalo na liwe??
....LIWALO Na liweee aka ya jamaaa yetu fulani
au umejiandaa na tim yako kuwa lolote litakalotokea mtapambana ili muradi tu ccm iendelee kutawala upande huo wa pili kimabavu???
Hivii uvumilivu wa maalim huutambui??
Hiviii tuseme hao makamishna wa tume waliojitangaza kwenye vyombo vya habari nadhani sasa wamefikia wanne.. Kuwa maamuzi yaliyofanywa na jecha hawayatambui na hawajui katumwa na nani kufuta uchaguzi halali?
Jee hili nalo unalinyamazia kimya mpaka kiwake ndio utaonyesha ujemedari wakooo??
Baba baba baba magufuli chondechonde baba!!
Chama chako ccm kinatupeleka tusikokutaka na kitakapo waka si wana ccm wala wapinzani ndio watadhurika bali watanzania wote tutaathirika na janga hili la kubumba.
Wewe ndio amiri na jemedari mkuu wa nchi yote ya tanzania sio upande mmoja tu maana hata huko upande wa pili ambapo kura zako zimefanywa ni halali ndio zimekuweka hapo ulipo.na zile nyingine tulizopiga kumchagua yuleee zimefutwa. Sio mbaya tutaheshimiana tu muda ukifika.
Usijifanye huwaoni waliokupigia kura na waliokunyima wote ni wako hao.
Umesema wewe ni msema kweli na msema kweli ni mpenzi waaaaa?...
Nasubiri kuuona usema kweli wako.