G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Wakuu, hali ya uchumi wa nchi ni mbaya kuliko kawaida. Sekta binafsi zimeachisha watu kazi kwa zaidi ya asilimia thelathini tangu kiongozi huyu alipotwaa madaraka.
Mbaya zaidi hatuoni dalili yoyote ya ahueni kwa siku kadhaa zijazo.
Nakumbuka kwenye kampuni yangu kuna vijana wengi walipendezwa na ujio wa rais Magufuli na wakawa mstari wa mbele kupiga chapuo kuwa kiongozi huyo anafaa. Ila kwa masikitiko makubwa vijana hao ambao baadhi yao walikuwa wa Lowassa na Magufuli takribani 37 (asilimia 35) ya wafanyakazi wote tuliwaachisha kazi kutokana na kushindwa kuhimili kuwabeba kwa zaidi ya miezi minne! Hali ni mbaya na mbaya zaidi!
Sipigii Chapuo ufisadi au ubadhirifu na uzembe! Lah! Naongelea hali halisi ya mzunguko wa fedha, makampuni mengi yamefungwa au kuacha biashara! Makampuni kadhaa yamesitisha uzalishaji, nini tatizo?
Serikali ya Magufuli kwa kweli hatuoni ikija na mkakati wa kukuza uchumi na kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo.
Nitashangaa sana kama watu watanibeza kwani hali halisi inaonekana! Ndugu watanzania tutumie fursa hii kimshauri rais Magufuli na kumpa ukweli kuwa taifa lipo katika hali mbaya kiuchumi! Kwa maana hiyo ni lazima kuna pahala lipo tatizo tena la msingi kabisa.
..................................................
Naomba kuweka kumbukumbu sawa; Sisi ni sekta ya uzalishaji tena inayotoa huduma muhimu kwa watanzania wengi. Hatujawahi kuwa na kashfa yoyote ya ukwepaji kodi. Tatizo ni hali mbaya ya masoko ya ndani, masoko ya nje kushuka kwa hali ya juu na ucheleweshaji wa malighafi na vifaa vingine pale bandarini (Kwa sasa siyo chini ya miezi mitatu na kuendelea). Mambo haya yanagharimu kampuni nyingi kwa kiasi kikubwa sana. Wengine wanapiga kelele kwa kuwa athari hazijawafikia moja kwa moja ila wao bila kujua tayari baadhi ya athari zimeanza kuwakuta! Mambo haya ukikaa chini ukafanya hesabu vizuri ndiyo unaweza kugundua kuwa kuna tatizo.
Nimetembelea pia viwanda vingine kadhaa vikubwa na vidogo vya uzslishaji mambo ni hayahaya. Wakati serikali ikijitutumua kuweka mambo yao sawa pia ni lazima iliangalie kwa umakini jambo hili vinginevyo tunaweza kuzalisha janga lingine.