Rais Magufuli hakurupuki juu ya maamuzi yake

shilatu

Member
Apr 18, 2015
58
30
Wakuu na siku mingi sana sijaandika nakuwa napitia sehemu za maandiko ya watu tu... Nawasalimu.

HOJA: Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli hajawahi kukurupuka katika maamuzi yake kwa sababu watu wengi hawajajua ni aina gani ya uongozi anayotumia (leadership style).

Kuna aina kadha wa kadha ikiwemo za kidemokrasia (democratic leadership style), ki dictator, kufuata misingi ya kisheria, red tepism, charismatic n.k.

SASA JPM YUPO UPANDE GANI?
Huyu mheshimiwa rais yupo ktk mfumo wa half charisma half autocratic leadership style. Kwa maana ya 90% ni mtu wa kufuata sheria inasemaje na kwa msingi huo ukiangalia autocratic leadership style huwa ina top down structure ktk decision making. Mara chache sana aina hii ya uongozi husikiliza subordinators wake.

Athari za Autocratic leadership style:

1: Mara zote first line managers husubiri maagizo kutoka kwa wakuu wao wa kazi na si vinginevyo.

2: Hujenga hofu katika utendaji wa kazi

3: Hupunguza ubunifu na uvumbuzi (innovation and creativity)

4: Hupunguza mahusiano mazuri kazini.

Faida zake Autocratic leadership style

1: Endapo kutakuwa na usimamizi mzuri wa misingi ya sheria, huongeza ufanisi wa kazi.

2: Huongeza uzalishaji.

Sasa kwa msingi huo rais wetu hakurupuki, ni aina tu na hulka yake ya uongozi anayotumia. Tutamwelewa..

Shilatu wa Sengerema Mwanza Tanzania. Tunasubiri daraja la Busisi to Kigongo liwake mataaa kama ya Kigamboni.
 
Kabisa bulldozer JPM Kawaweza this time whenever they try to put him down yeye anasonga na impact inaonekana pesa inapatika ktk shughuli za umma. Viva JPM
 
Nenda kawadanganye watoto uko!! Kukurupuka kwa tunao mfahamu magu ndiyo tabia yake! Ina mana ww ujui kama kalitia hasara taifa mabln kwa mabln, wakat mwingne tuache unafk tuwe wakweli
 
Watanzania aliyeturoga amekwisha kufa, uRais ni taasisi, hivyo rais anavyochukua maamuzi anakuwa na taarifa za kutosha juu ya hilo jambo, tofauti na wengi wetu tunavyodhani.
 
Amekaa serikalini miaka ishirini kama waziri, anaijua serikali vyema.......wabingo wamemjua juzi tuuu alafu wao wanajifanya kuijua serikali kuliko yeye! Gadeeeeem!
 
Kama tulimchagua tukijua ni Mkurupukaji basi pia tuliupigia kura ukurupukaji tutulie tuliii!
 
''Muheshimiwa raisi hakurupuki na hajawahi kukurupuka'' na ndo mana alitoa agizo Sukari isiagizwe kutoka nje, lakini baada maji kumfika shingo sasa ametoa vibali iingizwe nchini. CCM Oye.
 
Mi naona hasara za mfumo wa uongozi wake (kama jinsi ulivyoelezea) zitaubomoa zaidi utendaji wa serikali yake ikiwa watendaji wa chini yake wataishi kwa hofu na kustukiana mwisho wa siku hatadeliver kitu kwa wananzengo zaidi ya sarakasi za kutumbuana kila kukicha!

Halafu hapo kwenye hitimisho lako "daraja la busisi" sidhani kama inawezekana na kama aliahidi basi ni danganya toto tu! Labda baada ya miongo mitano ijayo ndo pengine inaweza ikafikirika kujengwa daraja hilo na halitakuwa na tija yoyote zaidi ya kuvutia sura ya Nchi.
 
Naona na wewe unajaribu kumuelewa. Kesho unaweza kuja na mawazo tofauti. Kila la kheri.
 
Nenda kawadanganye watoto uko!! Kukurupuka kwa tunao mfahamu magu ndiyo tabia yake! Ina mana ww ujui kama kalitia hasara taifa mabln kwa mabln, wakat mwingne tuache unafk tuwe wakweli
kwa hali ya nchi ilipokuwa imefika ni bora tuendeshwe ki-dictator for good will,ukicheka na nyani unavuna mabua
 
''Muheshimiwa raisi hakurupuki na hajawahi kukurupuka'' na ndo mana alitoa agizo Sukari isiagizwe kutoka nje, lakini baada maji kumfika shingo sasa ametoa vibali iingizwe nchini. CCM Oyee
Acha masihala wewe, wewe ndio unakurupuka sana...nenda kasikilize tena ile speech ya rais...hausema isiagizwe bali alisema haiwezi kuagizwa bila idhini yake au waziri mkuu..

Hivi inakufurahisha sana unapoona tuna import vitu kutoka nje?? Wewe haikuumi hata kidogo? Ni lini nasi tutaanza ku export vitu vingi nje? Kwani tukifika hapo tutaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi!
 
''Muheshimiwa raisi hakurupuki na hajawahi kukurupuka'' na ndo mana alitoa agizo Sukari isiagizwe kutoka nje, lakini baada maji kumfika shingo sasa ametoa vibali iingizwe nchini. CCM Oye.


looser!

what was their intention? was it wrong or right???

grow up div.5 alumni
 
''Muheshimiwa raisi hakurupuki na hajawahi kukurupuka'' na ndo mana alitoa agizo Sukari isiagizwe kutoka nje, lakini baada maji kumfika shingo sasa ametoa vibali iingizwe nchini. CCM Oye.
Mkuu huko siyo kukurupuka. Ni simply kufanya wrong decision based on unresearched information na kudisregard maangalizo ya watu wengine. Alikuwa na haja gani ya kusema sukari inatosha? Mama Kilango alienguliwa, sasa sijui yeye atajiadhibu vipi? Inashangaza Rais na watanzania wengine wanavyofikiri sukari ni ya chai peke yake. Kuna wamama wanaotegemea biashara zao za upishi, kuna viwanda vya juice na biscuit, vya ice cream na vya kuoka. Viwanda vya tomato sauce, chilli sauce. Sina uhakika decision yake inawacost watanzania hawa shilingi ngapi? Ninachojua lazima itawaumiza.
 
''Muheshimiwa raisi hakurupuki na hajawahi kukurupuka'' na ndo mana alitoa agizo Sukari isiagizwe kutoka nje, lakini baada maji kumfika shingo sasa ametoa vibali iingizwe nchini. CCM Oye.
Hapo umeona kama umemdhihaki mtoa mada, lakini kihalisia unajidhihaki mwenyewe. halafu ni upinzani ndiyo walikua wa kwanza kuiomba serikali iliyopita izuie utoaji wa vibali soma hii extraxt kutoka ITV website:
Chadema waitaka serikali kusitisha kutoa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje.
mbowe06.jpg





Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mh. Freeman Mbowe ameitaka serikali kusitisha kutoa vibali kwa wafanyabiashara wakubwa vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani ambavyo vimetoa ajira kubwa kwa watanzania.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mwamala, Bukene, Choma, Igurubi na mjini Igunga mkoani Tabora katika mikutano ya hadhara, mwenyekiti huyo wa Chadema amesema hatua ya waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kutoa vibali kwa wafanyabiashara wakubwa kuagiza sukari nje ya nchi huku akijua kuwa fika kuwa viwanda vya sukari vya hapa nchini vinayo akiba kubwa ya sukari kwa mahitaji ya ndani inalenga la kuviua viwanda hivyo.

Akiwa katika kijiji cha Choma wilayani Igunga, mwenyekiti huyo wa Chadema ameilaumu serikali kwa kushindwa kusimamia bei ya mazao ya wakulima ikiwemo pamba na tumbaku na kusababisha wakulima kuwa maskini huku mwenyekiti wa taifa wa baraza la vijana wa Chadema ( Bavicha ) Patrobas Katambi akisema laiti utajiri wa raslimali za gesi na madini uliopo nchini ungetumika vizuri, hakuna mwananchi ambaye angebaki katika lindi la umaskini uliotokea.

Naye mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Tabora Francis Msuka amepiga marufuku michango isiyokuwa na tija kwa wananchi inayofanywa kinyemela na baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji na kusema wananchi wanachohitaji ni kuona kodi zao wanazozilipa zinatumika kuwaletea maendeleo hasa katika sekta za maji, afya, elimu na barabara.
 
looser!

what was their intention? was it wrong or right???

grow up div.5 alumni
Kufahamu kwamba viwanda vyetu kwa sasa havina uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha haiitaji kuwa na PhD. Dhamira ya rais haikuwa mbaya lakini ALIKURUPUKA kama kawaida yake.

Rais alitakiwa kuvijengea uwezo wa kutosha viwanda vya sukari vya ndani ili viweze kuzalisha sukari ya kutosha kukidhi mahitaji ya wananchi. Anayeumia na maamuzi yake ni wananchi wa kawaida sababu bei ya sukari imepanda

Haya, alianza na kupiga marufuku kabisa uagizaji wa sukari kutoka nje, sasa analegeza msimamo wake anasema hadi kibali maalum . Mwisho wa siku ataruhusu uagizwaji uendelee kama kawaida.
 
Back
Top Bottom