Rais Magufuli azindua rasmi mradi wa Magari ya Mwendokasi kwa awamu ya kwanza

masatujr1985

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,980
781
Ndugu wanajamvi,

Leo Mh. Rais atafanya uzinduzi wa mradi wa Mabasi yaendayo haraka almaarufu UDART. Mradi huu ni mzuri na umethibitika kusaidia haswaa katika kuondoa adha za foleni kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam hasa maeneo unapopita mradi huu.

Mbali na umuhimu wake na faida zilizokwisha oneshwa, tunaomba Mh. Rais anapofanya uzinduzi wa mradi huu asiaite kupata majibu ya kero za abiria tunaotumia mradi huu.

Kwa kuwa kero zipo na zinaweza kuwa zinatofautiana kati ya kituo na kituo pamoja na mtu na mtu kadri alivyokutana nazo, ningeomba uzi huu utumike kuziainisha kero zinazoambatana na mradi wa UDART ili Mh. anapofanya uzinduzi aweze walau kusaidia kupata majibu ya kero hizo.

Ni yangu imani Rais anapata wasaa wa kupitia maoni na hivyo yaweza kuwa forum nzuri ya kufikisha changamoto zetu kwake.

Karibuni.


Rais Magufuli anazindua Mradi wa mwendokasi unaosafirisha abiria 200,000 kwa siku, utasafirisha abiria 450,000 kwa siku ukikamilika.

Simbachawene: Mradi wa mwendokasi unasafirisha abiria 200,000 kwa siku na unaweza kusafirisha abiria 450,000 kwa siku ukikamilika.

Mbarawa: Mradi umetekelezwa kwa mikataba saba na kugharimu bilioni 403.5, serikali imetoa bilioni 86.5.

Mbarawa: Awamu ya pili itakua Gerezani-Rangi tatu, magomeni hadi jitegemee na kutengeneza fly over Changombe.

Rais Magufuli: Nashukuru kwa heshima kubwa ya kushiriki nanyi na ni kweli naufahamu vizuri huu mradi tangu umeanza.

Rais Magufuli: Moja ya kumi ya watanzania wanakaa Dar es Salaam, athari za msongamano tunazifahamu ikiwemo ajali, kuchelewa makazini.

Rais Magufuli: Natoa shukraan zangu nyingi sana kwa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwa kufanikisha mradi huu.

Rais Magufuli: Awamu ya kwanza ndio tunaizindua leo, Bilioni 23.5 zilitolewa kama fidia. Nawashukuru sana benki ya dunia na kandarasi.

Rais Magufuli: Namshukuru sana ndugu Simon group kwa kuwa flexible kwenye mradi huu, na mimi nilimtegea hapahapa nimtumbue, amekwepa.

Rais Magufuli: Interchange ya Ubungo itakuwa na ghorofa tatu, matrafiki waliozoea kupanga wanavyotaka wao, ikimalizika hawatakuwepo.

Rais Magufuli: Awamu ya pili itakuwa kutoka Gerezani kuelekea barabara ya Kilwa itakuwa na kilometa 19.3.

Rais Magufuli: Sambamba na mwendokasi, miradi mingine ya miondumbinu itaendelea ikiwemo kujenga flyover kwenye maeneo mbalimbali.

Rais Magufuli: Michakato ya kupata express road mpaka Chalinze ya njia sita na imeshakamilika, imebaki kujadiliana na wakandarasi.

Pia, Rais Magufuli amesema magari ya watu binafsi yatakayopita katika njia mabasi ya mwendo kasi yakamatwe na kutolewa matairi na kusisitiza kwamba sio lazima kufuata sheria, wakati mwingine tutumie akili.
=====

Tazama Mjadala kuhusu habari hii ukisomwa JamiiLeo
 
CCM oyeeeeeeeeeeeeee! Ilani inatekelezwa, acha nimsubir Mh. Rais wangu mie:)
Hiii nchi hii ina viumbe wa ajabu sana kumbe ilikuwa hata haijazinduliwa watu mshaanza kuchakachua miundo mbinu yake kwa kuvunja vizuizi ili mchikue nondo, pale magomeni hosp katika kingo za mwendo kasi kuna bonge la mshimo wazungu hawaishi kujionea maajabu ya watanganyika viumbe wazito sana
 
Hivi zile bana matumizi za mwanzo wa utawala wake zilikuwa porojo tu?
 
Teh teh teh teh
Sio kwamba yanajaa mpaka kero.
Nakuonaga unavyotaabika kila siku.
mkuu licha ya kujaa tu kam mizigo y nyanya pia gari za kuhesabu ,jna ynyewe imebidi nipande 0002 then ubung pale nichkue jengne..
 
Wanazindua extension ya mradi (kwenda Mbagala/Gongo la Mboto) au uleule!? Maana sielewi kama ulikuwa unafanya majaribio hadi sasa!
 
Nasubiri vijembe na leo..sjui atakuja na mpya gani Leo..
Maana mukulu kila akiongea anajibu hoja kwa kebehi na mbwembwe
 
Back
Top Bottom