Rais Magufuli azidi kuiandama mitandao ya kijamii

Rais Magufuli azidi kuiandama mitandao ya kijamii

Ndo hapo sasa, mke wake akiumwa anatibiwa muimbili na alishasema vigogo wote watatibiwa muimbili iweje katibu wa Chama aende india kwa matibabu
 
Possibly ameenda kufanya matibabu au checkup ya ugonjwa wake ambao timeframe ya matibabu/checkup inajulikana

na ameambiwa aende ss ili aje kufanya kazi flan after recovery yake. so this window kuna vitu vitafanyika under his (JPM) authority

shukran.,
 
sasa
Akiongea leo wakati anaapisha wateule wapya Ikulu. Amesema mitandao yetu ni ya ovyoovyo na inaandika mambo ya ajabu ajabu.

"Jana nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa eti Mwakyembe hawezi kuja kuapishwa, na mimi nilikuwa nasubiri asifike nione. ''Sasa si huyu hapa amefika"

Ameongeza kuwa..... "Jana kuna mwingine kapost Kinana kuongea na waandishi wa habari kesho, wakati ukweli Kinana nimemtuma India Kwa siku kumi na mbili"

Amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuzipa nafasi habari mbaya mbaya tu, "mfano kuna tv habari za migogoro ya wafugaji ndio wanaipa nafasi kubwa zaidi, amesema hayupo tayari kuvumilia hayo mambo.

Ameshangaa magazeti ya leo kujaza mbele picha ya mtu mmoja, na hata kurasa za ndani kujaza habari hiyo hiyo.

Amemwambia Mwakyembe akasimamie kwa umakini hasa tasnia ya habari, amesema hayupo tayari kuona nchi ikichezewa..l

Ameshangaa kutangaza kutoandika habari za mtu, wakati huo huo wanaandika mbaya tu.... "Kama hamtaki kumwandika si masiandike yote mazuri na mabaya"


sasa alitak wamwongeree yeye
 
Kama ni za hovyo si aache tusome wenyewe,nani kamlazimisha asome au na yeye ni wa hovyo.??!
 
Yy pia anapenda mambo ya hovyohovyo....anawakumbatia watu wa hovyohovyo.....hata huyo alomteua alimkana hadharani...yaan nngekua mwakyembe niaingekubali....uroho wa madaraka....ccm yenyewe ya hovyohovyo...so achape kazi..aache mitandao....
 
Rais Magu haaminiki hata kidogo maana alishasema kuwa vyeti bandia ktk serikali yake ni mwiko viongozi wote watatibiwa muhimbili
Possibly ameenda kufanya matibabu au checkup ya ugonjwa wake ambao timeframe ya matibabu/checkup inajulikana

na ameambiwa aende ss ili aje kufanya kazi flan after recovery yake. so this window kuna vitu vitafanyika under his (JPM) authority
 
Hajui hata Benki kuu ya Dunia (WB) ineundwaje eti ana amini Marekani na Ulaya wanakopa humo wakati wao ndio wenye hizo fedha za WB .... asome mambo yanayo mhusu asitutie aibu kuongea madudu hadharani mbele za wageni.... mbona hatumsemi alipotoa "definition" ya catalyst ya chemistry kwenye mkutano wa Wa kuu wa EA ... madudu yote haya mbona hayaandikwi kumlinda yeye... hata ktk hotuba hii kachapia watu tunamstahi...! Vyombo vya habari vina zaidi ya miaka 20 vinadumisha amani ya taifa hili yeye ana miaka mi2 tayari anatambua genocide ni nini mbona hajui WB ni nini?
 
Nashangaa Ilani ya Uchaguzi ndani ya CCM inabadilika na kufuata mambo mengine kabisaa kwani mpaka sasa naona giza tu
 
Kama vile ana bifu na wananchi aisee, hivi usipoingia kwenye mitandao ukapiga kimya ukafanya majukumu yako ya mitandaoni utayajuaje, aendelee na Tanzania ya viwanda
 
Anavipangia vyombo vya habari vitu vya kuandika?
 
hakuna jambo zuri au baya. tafsiri anayoitoa mtu, mahali mwafaka, ndio maana husika ya jambo. maneno yanayosemwa na wawili chumbani na kucheka, nje watu huziba nyuso. mh rais mitandao kwa sasa ndio kila kitu. yamo ya ukweli, udaku, tetesi, vichekesho, ya kuudhi nk nk. msomaji ndie wa kuchagua la kumeza na kutema.
 
2017-03-25_17.55.54.jpg
 

Attachments

  • 2017-03-25_17.55.54.jpg
    2017-03-25_17.55.54.jpg
    270.2 KB · Views: 50
Back
Top Bottom